Huu Uzi imebidi niufatilie Hadi mwisho kutokana na kisa cha jamaa mmoja ambacho kilinipa funzo la maisha.
Jamaa anakofanya kazi Ni jirani na carwash. One day anatoka job mchana anakutana na mrembo mmoja wa grade za juu kabisa akipaki gari kwa ajili ya kuoshwa, jamaa akabaki amesimama akijiuliza huyo mtoto amemuona wapi.
Dada alipomaliza kupaki na kushuka jamaa ndo akachanganyikiwa kabisa kumuona alivyokama amechorwa kwa uzuri alio nao. Nadhani Binti aliligundua Hilo la jamaa kuchanganyikiwa.
Binti akamfata na kumuuliza samahani Kaka hapa jirani Kuna sehemu naweza kukaa na kupata Chakula wakati nikisubiri gari kuoshwa,, jamaa akaona Kama zali limemuangukia akamwambia hata yeye anaelekea huko. Wakaongozana mpaka kwenye Chakula. Huko jamaa akarusha ndoano zake kirahisi kabisa zikashika samaki bila upinzani.
Binti akamwambia amekuja jijini akitokea mkoa mwingine anaflight na anatarajia kupaki gari kwa rafiki yake jione aende airport kwenda jijini. Jamaa mbio kujipendekeza na kumwambia huna haja ya kuhangaika unaweza kupaki hata hapa ofisini kwangu. Demu kakubali na kufurahia msaada maana Ni jirani na Airport.
Kufika karibu na muda dada aliosema ndege yake ndo ingeondoka dada akasema hembu niangalie vizuri ticket kwanza. Akahamaki na kusema nilichanganya muda kumbe Ni SAA moja Asubuhi sio jioni. Sasa akamuomba jamaa amtafutie pa kulala jamaa akajiongeza na kumwambia anaomba demu alale kwake Kuna nafasi.
Demu bila kipingamizi akakubali. Sasa Kama Ada mabaharia hawapotezi pweinti. Jamaa katafuna kabonda. Tena na ujuzi wa kupiga deki kauonesha ili kumfanya mtoto atulie na kurudi Tena kwake akirudi anakokwenda.
Baada ya kubonda na kumaliza jamaa akili ndo zikaanza kumrejea kuwa mbona sijakapima haka katoto na katamu hivi katakuwa kazima.
Basi bwana jamaa akaona Bora nusu Shari kuliko Shari kamili, akaona ahakikishe anajua afya ya mtoto usiku ule ule kabla hajaendelea na game nyingine.
Tabu ikaja kwenye kupata vipimo. Jamaa ikabidi aigize kichwa kinamuuma ghafla ili waende hospitali na wakifika huko aintroduce wazo la kupima wote wakiwa kwa daktari.
Kweli igizo likatiki demu naye akafunguka kuwa yeye Ni muuguzi wa Afya anafanya hospitali moja huko kwenye mkoa anakotoka hivyo naye akamsihi waende hospitali kucheki Ni kwa Nini kichwa kinamuuma kiasi hicho labda anamalaria.
Kufika hospitali mida ya usiku jamaa wakaingia kwa daktari na kujielezea. Dokta akamwandikia akapime mkojo na damu kujua tatizo lake. Jamaa akaongezea na kumwambia dokta anaomba pia ampime na HIV wote wawili na mtoto. Dokta akamwambia Ni wazo zuri hata yeye anashauri hivyo.
Demu akawa Kama na kigugumizi lakini kauli ya dokta ikawa Kama imemfunga na kuondoa uhiyari wake. Basi vipimo vikachukuliwa.
Wakaambiwa wakakae nje wasubiri majibu yote kwa dk 20. Muda wote huo wakiwa wanasubiri majibu demu hata stori zikakata na kukawa na ukimya.
Mara akaanza kuona movement zisizoeleweka za daktari na Mara kaingia maabara katoka, Mara kamuita demu wakakaa muda wakiongea Mara wamerudi Tena maabara. Jamaa akaona avunje ukimya akawafata na kumuuliza dokta Kuna tatizo mbona majibu hutupi pamoja na tulikuja kwako pamoja. Dokta kaanza kujikanyaga kanyaga jamaa akaanza kuwa mkali Basi dokta ikabidi awe mpole na kuwauliza je mngependa majibu niwape kwa pamoja, jamaa akaitika kwa nguvu ndio lakini demu akagoma.
Dokta akamsii Sana jamaa asubiri nje mpaka atakapoitwa kwa ajili ya majibu yake, Basi bwana jamaa akakubali akatoka huku roho yake ikianza kupoteza imani na kila mtu mule ndani.
Badae akatoka yule dada na kumwambia Ni zamu yake aingie kwa dokta apewe majibu yake. Jamaa akaenda kwa dokta akapewa majibu yake yakiwa fresh Hana anachoumwa.
Basi jamaa Akauliza kuhusu majibu ya demu dokta akamwambia dada atampatia mwenyewe majibu yake. Jamaa akatoka shingo upande. Kufika nje kamkututa demu hayuko Tena.
Jamaa akajiuliza na kuamua kurudi kwa daktari baada ya kuona mapicha picha. Dokta akamwambia naomba tuongee Kama wanaume Sasa kaa chini. Akamwambia ukweli Ni kwamba yule dada wamemkuta Ni HIV positive.
Jamaa akili zilimruka ghafla. Dokta akawa na kazi ya kumtuliza. Dokta amuuliza kuhusu uhusiano wao Basi jamaa akamwambia ndio kwanza wamekutana mchana wa siku hiyo na hatimaye kula tunda kimasihara Tena kwa madoido yote uliyowahi kuyasikia mjini.
Daaaah dokta akamwambia Sasa sio mwisho wa maisha siku hizi Kuna PEP ukiweza kuinywa kwa kuizingatia utaweza kuepuka maambukizi uliyokwisha yapata.
Jamaa akaona Kama dokta ametumwa na Mungu kumuokoa akamwambia hata Kama Ni vidonge kumi kwa siku Yuko tayari kuvimeza pamoja na madhara ya dawa dokta aliyomueleza..
Dokta alimpatia vidonge 30 na kumwambia anatakiwa ameze jumla ya vidonge 28 na akimaliza arudi kupima Tena.
Basi jamaa na kopo lake huyo Nyumbani akamkuta yule demu mlangoni kwake akiwa analia kupita maelezo......
Itaendelea mkihitaji muendelezo. Ngoja Nile kwanza
Sent using
Jamii Forums mobile app