Ushuhuda: Hasara inauma asikwambie mtu

Usikate tamaa, nimepoteza vingi zaidi ya 100mil za kitanzania ila maisha yanasonga, nataka anza upya

Usije dangamywa na mtu kwenda kwa waganga wakuwekee ulinzi. Muombe Mungu atakulindia
 
Ni wale wenye kazi nzuri ndio wanaopiga upatu mujiajiri, mujiajiri, mujiajiri, huku watoto wao wakiwaajiri
 
Habari?
Wanajamvi,nimenunua mashine ya kutotolesha vifaranga hivyo napata changamoto ya malighafi yaan MAYAI. Hivyo nanunua mayai YA KIENYEJI yawe yanatokana na kuku halisi wa KIENYEJI.
Mwenye nayo au anaemjua supplier yeyote anayeweza niuzia mayai 500 kila mwezi kwa miezi 4 tuwasiliane PM kwa makubaliano ya bei na mengineyo.
Mimi napatikana Mbeya na vizuri kama supplier atakuwa mbeya na maeneo ya jirani yaan sumbawanga,tunduma,songwe,mbalali,makambako,njombe,iringa,na morogoro
Asanteni!.
 
Usikate tamaa, nimepoteza vingi zaidi ya 100mil za kitanzania ila maisha yanasonga, nataka anza upya

Usije dangamywa na mtu kwenda kwa waganga wakuwekee ulinzi. Muombe Mungu atakulindia
Nashukuru kwa ushauri wako.
 
Sijui naweza sema hofu yangu inaniokoa au inaniangamiza nimekuwa na tabia ya kusitasita kuanzisha biashara yoyote kwa kuhofia kupoteza mtaji wangu kwa maana mtaji nimeupata kwa msoto mgumu. Mpaka sasa nipo njia panda ya biashara gani niifanye kwa mtaji wa laki 3.
 
Kwenye kujiajiri ktk kilimo tunakabiliwa na changamoto ya wataalamu waliobobea ktk kutafiti na kupambana na magonjwa ya mazao, wadudu, udongo na kujua madawa yenye uhakika wa kukinga na kutibu

Kuna jambo la kutaka mafanikio ya haraka haraka pia ni changamoto hasa kwa vijana wanaoanza. Kilimo kinataka uvumilivu wa hali ya juu sana, sio suala la leo umewekeza kesho ukaamka tajiri

Masoko ya mazao pia hayaeleweki wakati mwingine. Kuna wakati soko linayumba hadi kichwa kinapata moto, lakini ni kukomaa hivo hivo

Misimu pia haitabiriki. Mvua na jua. Miaka ya nyuma ilikuwa inajulikana mvua inaanza lini na inaisha lini, siku hizi ni pasua kichwa
 
Ni aibu serikali kushindwa kutawanya wataalamu wa kilimo japo kila tarafa ili wawazungukie wakulima wa maeneo yao nakutoa ushauri wa haraka bure. Wakulima wengi wanaishi kupata hasara kwakutokujua mbinu sahihi za kilimo mfano wapande mbegu gani, muda gani, dalili za magonjwa mbalimbali na dawa zake za kuzuia au kutibu, udongo, mbolea na matumizi yake sahihi n.k. Matokeo yake mkulima anaishia kununua kila aina ya dawa anayoambiwa na watu hasa wenye maduka ya pembejeo bila kujua kuwa wengi wao wapo kibiashara ili wauze dawa hasa zile ambazo ni ghali hatakama siyo ya ugonjwa huo na pia kipimo hakizingatiwi. Ni aibu kwakweli. Wakati huo kuna wataalamu wa kilimo wapo tuu mtaani wakifanya mambo yao private. Ifike mahali sekta hii nayo iangaliwe kama wanavyoangalia shule ambazo hazina waalimu au vitu vya afya ambavyo havina wahudumu wa afya. Pole sana ndugu.
 
Ni kweli aiseee serikali naona kama haijajitahid sana kuwekeza kwenye kilimo haswa tafiti na namna ya kupambana na wadudu na wagonjwa...
 
You've been knocked out, but you have to stand and keep the fighting alive. Hakuna mafaniko rahisi.
 
mkuu next time jaribu kuwa middle man utafanikiwa mkuu , Ukiwa mkulima usifuate mkumbo kuwa specific and strategicall.Siku zote usifanye biashara ambayo kila mtu anafanya hasa hii ya watu kushauriana ujinga kwenye magroup ya whatsup
 
Kuna msemo huwa nauamin "Mbegu mpka ioze ndio hutoa mmea so usiogope ni changamoto tu hzo Mkuu"
 

ahahhahaah hatari sana kijjana wangu. so una subiri tena kwa mda gani maana kilimo inategemea na eneo. so matikiti yalikuwa vizuri sio
 
Maskini Mdogo wangu pole sana kijana. usikate tamaa ila wakati mwingine fanya utafiti sana, dogo mimi nimelima huu mwaka wa 11 sasa, nimewahi lima mahindi kama hekari 120 zikaja zikaenda na mvua zoote sikukata tamaa niliamka nikalima nikaongeza zikawa hekari 156 nikaja nikavuna balaa, kuja sokoni bei serikali imepanga aisee niliumia sana nikafanya mchakato nikahonga nikapata kibali nikauza nje mahindi yangu na tangu hapo sijataka kabisaa kulima mahindi
ila nakushauri kama legendary wa kilimo usilime bila kufanya utafiti wa kina wa kile unachotaka kulima na pia kamwe usije rubunika na faida au output ya zao wewe fanyia utafiti wako zile changamoto za zao husika na jipime je waweza zi-handle?? kama huwez acha kabisaa

kingine licha ya changamoto fanya utafiti wa soko wa zao lako usije lima kisha ukajikuta unalia na madalali sokoni au kuzorota kwa bei, halafu pia kama ukishapata habari kamili ya gharama za zao lako mfano ni laki 9 ongezea laki mbili ya imejensi. Kilimo hapa bongo huwa hakina fixed costs.
Na mwisho ukitaka kulima mdogo wangu (depending na eneo uliloko) anza na mazao ya muda mfupi kama mchicha, spinachi, mnafu nk hii itakupa picha kamili ya kilimo kilivyo na pia itakutengenezea network na watu kibao ktk field yako

Kila la kheri mdogo wangu Mungu akubariki sana sana
 
Asante sana ndugu yangu kwa msaada wa mawazo,nitayatendea kazi. Nina imani mambo yatakuwa mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…