Mkuu mimi niliwahi kupatwa na vidonda hivyo vya tumbo mwaka 2006 na mpaka sasa nahisi ninavyo ili nikianza kupata dalili tu huwa najua nini cha kufanya.
Kwanza kabisa hivi vidonda viko aina kuu mbili, deodenal na peptic ulcer. Ya kwanza ikikupata hua ukila chakula ndio inazidi na ya pili ukila cha kula ndio unapata nafuu. Sasa sijui huyo dada yako ana ulcer ipi. lakini kwa ufupi mimi nilikabiliana nayo kama ifuatavyo.
1.Mara ya mwanzo viliponianza nilikuwa kila chakula ninachokula basi kama baada ya nusu saa tumbo hua kama linawaka moto. Sasa namshukuru Mungu nilikuja kubaini kitu kimoja. NIkila maziwa jagi moja na tende kokwa tatu kila ninaposikia njaa basi maumivu ya tumbo kuwaka moto yanaondoka. Hivyo nilikaa kama wiki moja nikishindia tende na maziwa tu.
Angalizo: Kitaalamu Maziwa yanaweza kuongeza tatizo la vidonda, hivyo ni vyema kunywa kiasi tu.
2.Mgonjwa anatakiwa asikae na njaa kabisa yaani kila baada ya muda ale kitu lakini kiasi kidogo tu.
3.Aepuke kula vyakula vinavyoongeza tatizo mfano Nazi, mafuta mafuta, pilipili, vitu vikali, SODA hususan wakati wa kulala.
4.Inashauriwa anywe maji kwa wingi.
MAONI: SUALA LA KUPONA KABISA SI JAMBO LA KUWA NA MATUMAINI NALO. MAUMIVU YATAONDOKA ILA KAMA AKIWEKA MIKO YATACHELEWA KURUDI.