Ushuhuda Kuhusu "Njama" za Mabeberu kwa Nchi Maskini

Ushuhuda Kuhusu "Njama" za Mabeberu kwa Nchi Maskini

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
7,745
Reaction score
11,267
Naanza kwa kukiri kuwa mimi sio mwandishi mzuri ila uzi wa Pascal Mayalla umenifanya nijitutumue kuandika.

https://www.jamiiforums.com/threads...a-waanza-uzushi-wa-fujo-baada-ya-jpm-ccm-kush.

Nilitaka nitumie neno wazungu au mataifa ya Magharibi badala ya "mabeberu" ila nikawaza sio wazungu wote wana nia mbaya na sisi, wanatupenda sana na ndio maana tunapata dawa za Ukimwi, chanjo na vyandarua" buree"! wapo ambao dhambi ya kubeba dhahabu, pembe za ndovu na watumwa bado inawatafuna na wanatamani kubeba tena mali ghafi kutoka huku na hao ndio mabeberu kwa tafsiri yangu!

Miaka nenda miaka rudi mabeberu mbinu zao huwa ni zile zile japo kwa miaka ya hivi karibuni jamaa wameadvance kidogo, hii imeelezwa vizuri na mmoja wa mabeberu ambaye aliamua "kuokoka" na kuweka ukweli wote wazi.

John Perkins katika kitabu chake "The New Confessions of An Economic Hitman" ameelezea mbinu zote na wapi zilitumika na zinavyoendelea kutumika. Ujinga wa mabeberu ni kuwa mbinu zao huwa ni zile zile, ukiangalia kuanzia kwa aliyekuwa Kiongozi wa Libya Gadaffi, Sadaam Hussein wa Iraq, na kurudi nyuma mchezo ni huu; Rais au kiongozi wenu atapewa rushwa kubwa, mtapewa mikopo mikubwa ambayo mtashindwa kuilipa (maana riba ni kubwa), wataandaa kibaraka kutoka mingoni mwenu, vyombo vyao vya habari vitakuza mizozo midogo ya kijamii kuwa janga mfano watoto wanaandamana kupinga mabweni yao kuungua moto itaonyeshwa na CNN, FOX n.k. kuwa "nchi nzima imeandamana na polisi wanaua waandamaji n.k.

Mwanzoni nilisema mimi sio mwandishi mzuri hivyo nimeweka kitabu cha mwandishi huyo, najua madhara ya "haki miliki" ila nimejitoa muhanga kwa ajili ya nchi yangu maana naona kila dalili ya Tanzania yangu kuelekea huko. Kwa wale wasiopenda kusoma vitabu nitaweka link ya kupakua documentary ambayo imetokana na kitabu hiki. Pia kama kuna mtu miongoni mwetu yupo karibu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, nk namuomba ampe/awape nakala au jina la kitabu hiki.

Kuna watu wanatumiwa bila kujua hao tuwasamahe ila wengine wanajua ila ni njaa tu na tamaa zao. Hata Hivyo bado wapo watu wema ambao kwao Tanzania ndio mama yao na wanayo mapenzi mema na nchi yao, kwa moyo mmoja tusome kitabu hiki ili tujue mbinu mahsusi za mabeberu.

Untitled.jpg
 
Back
Top Bottom