USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Good lesson...hivi kanda ya ziwa naweza kupata wapi hawa chotara maana nimeangalia makala nyingi za ufugaji kuku wa kienyeji ni kweli hawa ndio wanatija sana... please advise kwa kanda ya ziwa nawapataje
Kama upo Bukoba niPM nikuelekeze
 
Mambo vipi mkuu
 
Safi sana kwa mada nzuri,
Mimi ni mfugaji na ninatotoresha vifaranga wa Malawi (Black), Chotara, na Kloiler nimekuwa nikipitia changamoto nyingi katika masoko wengi hawajafahamu hizo mbegu wanakimbilia kwa kuku wa kienyeji pure ambao ni wazi hawana faida kubwa.
Kwa somo hili litanisaidia kuwafumbua macho wateja wangu.

Kwa yeyote anae hitaji vifaranga wa kuku malawi, kloiler na Chotara pia kanga na bata mzinga asisite kunitafuta napatikana Mwanza Kisesa. simu number 0713 646577 au 0752093038. Tunasafirisha mikoani pia.
 
Safi lakini umeharibu ulivyojiweka wazi kwamba ni tangazo la biashara
 
Kuroiler vifaranga 100 ni sh ngapi unauza?
 

Mkuu upo sahihi kama tu umeamua kufuga kuku kienyeji na sio kibiashara.

Kibiashara hao kuku wanapoangua tu vifaranga wanyanganye au watenganishe na mama zao na kulea hao vifaranga kama vifaranga wa mayai. Mama zao wadumbukize kwenye maji for 2 - 3minutes akitoka hapo kasahau vifaranga ndani ya wiki mbili au tatu ataanza kutaga tena.

Pia unaoption ya kuwatotolesha mayai kwenye incubator na kulea vifaranga kama nilivyosema hapo juu. Hapa utaona faida lakini pia kama unataka kulea kuku kibiashara achana na kuku 10 walau majike 150 kuendelea ndio biashara yenye tija. vinginevyo hao unaofuga 10plus its for home consuption and form of household savings.
 
Nilimzamisha kuku wangu lkn hakusikia, alipokauka katafta tenamayai hadi nikampa nakatotoa vizuri
 
Safii mimi nazidi kuchota maarifa tu nikianza ipo full.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mimi nadhani haujazingatia mambo muhimu kauli zako. Kuhusu kuhifadhi mayai hata kuku wa kienyeji unaweza kuwafuga bila jogoo. Kuku wa kienyeji wananawiri kwa gharama ndogo ya lishe na kuonekana wakiwa smart kila wakati..kupoteza mda kwa kutamia mayai ni uchaguzi wako hata wao ukitaka hawatamii..na wanapo maliza kutaga wanachukua wiki moja tu kutaga tena. Kuku wa kienyeji ni kuku wa kuboreshewa mbinu za juwafuga na kutolewa masomo hasa ya kuwafuga kwani ndio kuku wetu wa asili. Kwanini watanzania tupoteze kila asili yetu? Ngozi tunachubua..nywele tunaweka dawa na kuweka za bandia..basi mpaka kuku? Mimi nadhani ipo haja ya kuzidisha juhudi katika kufuga kuku wa kienyeji.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. I
Naomba nikujuze kwanza hapa kwamba hawa Kuku wa Kienyeji wanafugwa kisasa hawapewi nafasi ya kutamia mayai
 
Mtoa hoja nimekukubali asimilia mia. Ushauri ambao una ukweli ndani yake - safi sana
 
Asante mkuu kwa elimu.
Uzoefu unanieleza kuwa kilimo vitendo kuliko theory. Ufuge kwa muda mrefu huku ukipambana na changamoto. Ulime kwa muda ukikusanya uzoefu. Baada ya muda unaiona faida. Kilimo mchanganyiko ni Bora sana. maana mufugo inasapoti mazao nayo yanasapoti mufugo.
Wengi wamesikia na kukurupuka na mwisho wamekula hasara. Lazima pia uwepo wako uwepo usiregemee watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…