USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

mmmmh nashindwa kukubaliana na wewe pia nashindwa kukupinga.
Nadhani kuna kitu muhimu umekiruka kwa bahati mbaya ama kwa makusudi kabisa.
 
Haya sasa tunaamua ku maintain afya za wananchi kwa mfano hivi sasa tupige marufuku mayai na kuku wa kizungu ktk soko hivi tuna uwezo wa kutosheleza soko ktk mayai na kuku kwa ku supply hao organic chicken PROFITABLY
Lets change our minds and think Business katika jamii ya wafugaji tulio nao na hili halipo kwa kuku wa kienyeji tuu liko hata kwa kuku wa kizungu kuna mfugaji hapa anaweza akasema kuku wake from day 1 mpaka siku anaenda kumuuza anakuwa
1.Amekula chakula Kilo ngapi ?
2.Kimegharimu kiasi gani
3.Madawa
4.Chanjo
5.Labour costs
Na vitu kama hivyo hatujiulizi kwa mfano mtu akifuga kuku wa mayai au wa nyama anaweza ku "Break Even" akiwa na kuku wangapi na vitu kama hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mmh? Kumbe kuanza biashara bila utafiti wakutosha ni hatari kiasi hicho? Hao australorp nawapata wapi na vifaranga ni bei gani?
 
[emoji23] [emoji23] sasa ukimdumbukiza si atakuga jaman
 
Asante sana mkuu. Nilitaka niingie kichwakichwa ila umeniokoa.
 
Nadhani mtoa hoja ya uzi huu umekuja chini ya ufadhili wa watu wa Marekani. Kukidhi kwa mazingira ya Tanzania wanaohitaji kuanza anzeni na kuku wa kienyeji kwasababu huvumilia magonjwa tofauti na wa kisasa. Pia gharama zake ziko chini katika kuwahudumia tofauti na wa kisasa . Lakini jambo lililo zuri zaidi ni kuwa bei ya kuku wa kienyeji ipo juu na huwa haipimwi kwa kutumia mizani. Mnajua kwasababu gani?. Siku hizi hadi nchi za Ujerumani, Uholanzi na nyinginezo nyingi wameanza kuikimbilia matunda yasiyopigwa sana madawa na mifugo isiyonyweshwa sana madawa. Hivyo thamani ya kuku wa kienyeji haitakuja kupitwa na kuku wa kisasa. Na Kikubwa katika kuboresha biashara ni kufuga kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa. Uzuri wa kuku wa kienyeji anaweza kutibiwa magonjwa kwa kutumia dawa za asili kama pilipili kichaa, vitunguu swaumu n. k, na pia wanaweza kupewa na milongelonge kwa kuchanganyishiwa kwenye chakula na kumfanya urutubishaji na uboreshaji katika kutaga. Hivi unajua madhara ya mayai wa kuku wa kisasa?, hizo chips zenyewe watu wameanza kubadili direction hakuna kuku mayai labla kwa wale wasioshtuka bado. Na Kuku wa nyama wa kisasa wanajifariji unakula nyama ila usitafune mifupa yake. Lakini mwisho kama uzi wako upo kwa ajili ya chini ya ufadhili wa watu wa Marekani ok bro sikuingilii sana
 
Hakuna kitu hapo.... Ujanja ujanja tu....

Hakuna biashara isiyokuwa na faida....

Ni suala la umakini na kuthubutu tu.

Kuku wa kiemyeji kutaga mayai 7 si kweli!!!!!

Kuku wa kienyeji anayekula vizuri hutaga hadi mayai 15-18.... Inategemea na ufugaji wako na teknik...

Kuhusu ugumu wa kutunza mayai pia si kweli....

Yai la kienyeji linakaaa hata mwezi mzima bila kuharibika...

Kuku hukalia mayai kuanzia 9 na kuendelea... Inamaana anakalia yai viza wakati daily ndio hutaga...?

Kuku wanalipa wadau... Na mimi nafanya iyo busineaa... La msingi ni kuchagua sehem bora ya kufuga... Masokko... Chakula na maji ya kutosha tu.
 
Mkuu
Mkuu acha umesema kumekuwa na watu ambao ni wapotoshaji Kwa sababu tajwa hapo juu.
Kwanza niseme wewe si mbunifuu Kwenye ufugani unaonekana ni mbabaishaji na umelenga kuitangaza hiyo biashara yako yamachotara.
Okey nianze na hoja yako number moja kuhusu utagai wa kuku wa kienyeji.
Kama mjasiriamali ulipaswa kutoa elimu ni namna gani tunaweza mfanya kuku wakienyeji akatutagia mayai mengi zaidi Kwa mwaka.
Kwani Mimi nawafuga wote hao kienyeji na chotara na hakuta tofauti kubwa Kwenye utagaji wao Kwa mwaka.
Kwanza namna yakumfanya kuku wa kienyeji akupe mayai mengi Kwa mwaka yakupasa kufanya yafuatayo.
1:Kama Una kuku tuseme mmoja ndo umeanza nae na ameanza kutaga. Akianza kulalia mpe mayai alalie Kwa hizo siku 21 then akiangua vifaranga mnyanganye vitunze Kwenye brooder. Mama mzazi mchanganye na majogoo.
Hapo ataanza kutaga soon na utaongeaza uzalishaji kidogo.
2: Kama Una kuku wengi kuanzia kumi nakuendelea hapa kuna njia mbili.
i. Kuku wakitaga kusanya mayai Kwa idadi utakayo pata. Theni unashauriwa upeleke mayai Kwenye mashine yakutotoleshea vifaranga aka incubator.
Kufanya hivyo utakuwa umesave mda wa kulalia na mda wakutunza vifaranga.
Kwa kawaida kuku akimaliza taga na ukamnyima kulalia Kwa kumuweka sero Kwa wiki moja Ile Hali yakulia anaisahau na anaanza maisha mengine mapya yakuanza kutaga baada ya wiki mbili au tatu. Hali hii inaweza kukupa wastani mzuri wa mayai Kwa mwaka na ni zaidi ya mayai Mia Kwa kipindi cha mwaka.
2: Vile vile hakikisha kuku wako unawapa vyakula Bora vyenye madini yote ili kuongeza virutubisho vyakutosha mwilili.
Hali hii pia itamfanya aongeze uzalishaji wa mayai.
3: Hakikisha unawapatia chanzo Kwa wakati hapo itakusaidia kupunguza vifo na kumaintain uzalishaji wako.
4: Hakikisha mazingira Yao ni masafi kuanzia mabanda, maji ya kunywa vyombo etc. Kuku wanaathiriwa Sana na magonjwa ya tumbo na kuku akiwa mgonjwa hata uwezo wa kutaga unaoungua.
So kufanya hivyo kutakusaidia kuwa na idadi nzuri ya mayai pia.

Naomba kusema kwamba hata hao chotara unaosema wanataga mayai mengi ukikosea kuwafuga kuanzia mwanzoni utagaji wao unaweza kuwa mdogo kuliko hata wa kuku wakienyeji.

Nasema hayo kwani kuku wote hao Mimi nawafuga.
Nafuga kuku kienyeji pure
Nafuga Kuroila ,Kenbro na saso
Nafuga Kuchi, bata bukini,mzinga ,bata kienyeji na kanga.
Changamoto hazitofautiani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…