USHUHUDA: Nilisaidia mtu nami nikasaidiwa

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Mwaka fulani, nilikuwa katika wakati mgumu sana, though kidogo nilikuwa na mpunga wa kusavaivu, kuna dogo mtoto mmoja nikakutana naye ameshindwa kuendelea na masomo kwasababu ya ada, niliamua kutoa hela kumlipia ada pamoja na kwamba mwenyewe nilikuwa na uhitaji mkubwa sana. Dogo akaenda shule. MATOKEO YAKE, nilikuja kupata scholarship kubwa sana ya kusoma nchi bora kabisa za Magharibi, kirahisi mno kwa kukuta tu tangazo kwenye mtandao bila kujali kama watakuwa matapeli au la. nililipiwa kila kitu, nikasoma kama mtoto wa kitajiri kumbe nilitoka familia masikini.

Mwaka mwingine, nilikutana na dogo mmoja anajua sana kuimba, alikuwa anaimbisha nyimbo za kuabudu kila siku, hana hela, hana kazi, ni mtu mwenye uhitaji. niliingia mfukoni nikatoa hela yangu ya mshahara, my wife ni mwelewa alifurahia nilichofanya kwa imani, na nikamwambia yule dogo sitaki unitangaze wala unishukuru, (NILIMPA PESA HIYO AKAREKODI KANDA YAKE YA KWANZA YA GOSPEL) mimi nampa Mungu sadaka wewe kamshukuru Mungu.

Matokeo yake, kila ninachofanya kinafanikiwa na anayepingana na mimi kwenye harakati zangu za kutafuta maisha huwa anapambana na Mkono wa Mungu, lazima nimshinde, na pesa sizipati kwa jasho sanaaaa kama ilivyokuwa awali. kuna wakati pesa unaweza kuwa unazipata kirahisi tu, kwasababu katika ulimwengu wa roho, milango imefunguka.

kuna shuhuda zingine kadhaa za ajabu, Mungu alinipa vitu kutokana na mimi kutoa. nikiandika hapa patakuwa parefu mno watu watachoka kusoma. naomba niandike zingine siku nyingine. Nawaasa watu, saidieni watu, na msipende kupata shukurani toka kwao, wakampe shukurani Mungu, na usijionyeshe kama umetoa (hata mimi hapa ni kwasababu sijadisplay jina),ukimpa kitu mtu akakushukuru, hautapata thawabu toka kwa Mungu, umekwisha pata thawabu toka kwa yule mtu uliyemsaidia, ila akienda kumshukuru Mungu kwa ajili yako, lazima Mungu arudishe thawabu kwako.

Hii ndio sheria kubwa sana ya Mungu katika ulimwengu wa roho, hasa ikizingatia kuwa God never shares his glory, na ni Mungu mwenye wivu huwa hawagani utukufu na Mwanadamu, yeye pekee anastahili utukufu wooote. na kipimo kile upimacho ndicho utakachopimiwa.

katika kitabu cha LUKa 6:38, imeandikwa,

Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Ana heri mtu yule, ambaye Bwana ni Nguvu zake, BWanani nguvu zake, Bwana ni nguvu zake, Ana heri mtu yuleee, ambaye Bwana ni nguvu zakeeee, Bwana ni nguvu zakeee,Bwana ni nguvu zakeeee. (I feel in my heart singing this song all day).
 
Amen, somo zuri.!

Naomba Mungu na mimi anipe roho hiyo.
 
Ulichoandika ni kweli kabisa,kuna siku nakumbuka nilisaidia mtu sh mia 2 ila kabla siku hiyo haijaisha nililipwa deni la sh milion 1.4 ad nlishangaa na sikuwa na matumain ya kulipwa hiyo hela..
 
Kuna watu huwa wanapitia kwenye uchungu sana wa maisha, wanakuwa wanamuomba Mungu,na Mungu huwa anajibu watu kwa kupitia watu, akikugusa kwamba msaidie huyo, saidia, nenda zako wala usihitaji shukrani wala kujitangaza, wao watamshukuru Mungu aliyekugusa ukamsaidia, na wewe utajuana na Mungu kwasababu Neno hilo kwamba wapeni watu vitu nanyi mtapewa vingi hadi kumwagika, ni la kweli, halitanenda bure. huu ndio ukweli ambao wengi wanatembea nao na wanafaidika nao.

Ukikutana na mtu ana shida, usimcheke wala kumtangaza au kuona kama ni mvivu asiyejua kutafuta maisha. breakthrough ipo rohoni huku mwilini ni manifestations tu, unaweza kuhangaika mno hadi ukaungua ugonjwa wa moyo kwa mawazo unatafuta maisha, lakini rohoni kukifunguka, unagusa tu kitu kinafanikiwa. hasa pale unapokuwa na backup ya Mkono wa Mungu juu yako. hakuna linaloshindikana.

Huwezi kusaidia kila unayekutana naye, utasaidia yule ambaye umeguswa moyoni kufanya hivyo. ila ukweli ni kwamba, wale ambao umeguswa moyoni kusaidia, ukisaidia haiendagi bure. kwani Neno linaposema, nilikuwa na njaa hamkuja kunipa chakula, nilikuwa mgonjwa hamkuja kuntazama n.k, unafikiri lina maanisha nini? yale unayowafanyia watu ndiyo unavyomfanyia Mungu. dakeni siri hii mtanikumbuka.
 
Ukigusa moyo wa Mungu huwa anafanya jambo. unaweza kugusa moyo wa Mungu kwa kuwatesa sana watu na kuwadhulumu au kuwanyanyasa, wakilia machozi kwa Mungu, huwa anashuka kuwasaidia, atakushghulikikia hakika.

Pia kuna watu wanamwomba Mungu awasaidie, wewe ukitumika kama chombo kuwasaidia, bure wala si kama deni kwamba uwanyanyasie msaada wako, wao watafurahi na kumshukuru Mungu, Mungu atashuka pia na kukubariki kwasababu umefanya jema kwa ndugu/jirani yako ambaye amempa yeye Mungu utukufu. hii ni sheria mojawapo ya roho ambayo inafanya kazi wazi wazi, na haidanganyi.
 
Me nilimnyimaga mtoto wa watu mia mbili na nilikua nayo baadae nikapoteza elf kumi😂😂daah nilicheka lakin yule dg alizngua ndo maana sikumpa kaja kunigongea asubuh geto af me simjui kasema kaka ooh sijui nisaidie mia mbil ya kula shule nyumban wameninyima,,apo me nilikua na mawenge ya usingz
 
Mwaka fulani, nilikuwa katika wakati mgumu sana, though kidogo nilikuwa na mpunga wa kusavaivu, kuna dogo mtoto mmoja nikakutana naye ameshindwa kuendelea na masomo kwasababu ya ada, niliamua kutoa hela kumlipia ada pamoja na kwamba mwenyewe nilikuwa na uhitaji mkubwa sana. Dogo akaenda shule. MATOKEO YAKE, nilikuja kupata scholarship kubwa sana ya kusoma nchi bora kabisa za Magharibi, kirahisi mno kwa kukuta tu tangazo kwenye mtandao bila kujali kama watakuwa matapeli au la. nililipiwa kila kitu, nikasoma kama mtoto wa kitajiri kumbe nilitoka familia masikini.

Mwaka mwingine, nilikutana na dogo mmoja anajua sana kuimba, alikuwa anaimbisha nyimbo za kuabudu kila siku, hana hela, hana kazi, ni mtu mwenye uhitaji. niliingia mfukoni nikatoa hela yangu ya mshahara, my wife ni mwelewa alifurahia nilichofanya kwa imani, na nikamwambia yule dogo sitaki unitangaze wala unishukuru, (NILIMPA PESA HIYO AKAREKODI KANDA YAKE YA KWANZA YA GOSPEL) mimi nampa Mungu sadaka wewe kamshukuru Mungu.

Matokeo yake, kila ninachofanya kinafanikiwa na anayepingana na mimi kwenye harakati zangu za kutafuta maisha huwa anapambana na Mkono wa Mungu, lazima nimshinde, na pesa sizipati kwa jasho sanaaaa kama ilivyokuwa awali. kuna wakati pesa unaweza kuwa unazipata kirahisi tu, kwasababu katika ulimwengu wa roho, milango imefunguka.

kuna shuhuda zingine kadhaa za ajabu, Mungu alinipa vitu kutokana na mimi kutoa. nikiandika hapa patakuwa parefu mno watu watachoka kusoma. naomba niandike zingine siku nyingine. Nawaasa watu, saidieni watu, na msipende kupata shukurani toka kwao, wakampe shukurani Mungu, na usijionyeshe kama umetoa (hata mimi hapa ni kwasababu sijadisplay jina),ukimpa kitu mtu akakushukuru, hautapata thawabu toka kwa Mungu, umekwisha pata thawabu toka kwa yule mtu uliyemsaidia, ila akienda kumshukuru Mungu kwa ajili yako, lazima Mungu arudishe thawabu kwako.

Hii ndio sheria kubwa sana ya Mungu katika ulimwengu wa roho, hasa ikizingatia kuwa God never shares his glory, na ni Mungu mwenye wivu huwa hawagani utukufu na Mwanadamu, yeye pekee anastahili utukufu wooote. na kipimo kile upimacho ndicho utakachopimiwa.

katika kitabu cha LUKa 6:38, imeandikwa,

Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Ana heri mtu yule, ambaye Bwana ni Nguvu zake, BWanani nguvu zake, Bwana ni nguvu zake, Ana heri mtu yuleee, ambaye Bwana ni nguvu zakeeee, Bwana ni nguvu zakeee,Bwana ni nguvu zakeeee. (I feel in my heart singing this song all day).
Nisaidie hela ya kula leo rafiki,elfu tano tu inatosha
 
Back
Top Bottom