Ushuhuda wa mapenzi makaburini

Ushuhuda wa mapenzi makaburini

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
384
Reaction score
658
Wazazi wangu walikuwa wameoana kwa miaka 55. Asubuhi moja, mama yangu alikuwa akishuka chini ili kuandaa kifungua kinywa cha baba, alipatwa na mshtuko wa moyo na akaanguka. Baba yangu alijitahidi kadiri alivyoweza ili kumnusuru alimburuta hadi alipo lifikia gari lao dogo na kumpakia ndani,

Baba aliendesha gari kwa mwendo wa kasi, bila kuheshimu taa za trafiki au mikono yao ili kumuawahisha mama hospitali kwa ajiri ya matibabu,

Wazazi wangu walikuwa wakihudumiwa na hospitali ya Amana ilioko wilaya ya Ilala japo kutoka gongo la mboto mpaka ilala kulikuwa na mwendo lakini baba kutokana na uzoefu wake kwenye uendeshaji wa magari aliweza kuendesha kwa mfano wa dereva wa Ikulu,

Baada yakufika hosptali na wauguzi kumkagua hatimae mwili wa mama ulikuwa umetengana na roho kifo kilikuwa kimemchukua,

Tukiwa wenye majonzi kwa kuondokeawa na mpendwa wetu mbele yetu alikuwa amesimama baba yetu huku akiinama na machozi yakimtirilika,

Uso wake ulijaa mikunjo na uzee wake haukuhitaji kioo ili kuweza kujua mateso alio kuwa akiyapitia baada ya mrejesho wa kifo cha mama,

Mwili wa mama ulikhifadhiwa katika chumba cha wafu (Mochwari) huku tukiendelea kuomboleza kifo cha mpendwa wetu,

Siku iliyofuata hospital walitukabidhi mwili wa merehemu kwa mazishi hapakuwa na usumbufu kama ilivyo kuwa kwa jamii ya watu wengine ambapo hospitali waliizuia miili mpaka walipwe gharama za matibabu sisi tulitakiwa kulipia kiasi kidogo cha kumsafisha marehemu na gharama kadhaa za kuhifadhi mwili katika chumba kile,


Wakati wa mazishi, baba yetu hakuzungumza lolote mbele ya halaiki kwa kuwa alikuwa ni mtu alietindikiwa kwa majonzi muda wote macho yalimtoka huku kamasi laini zilikuwa zikimtililika pasina kukoma ni wazi kifo kilikuwa kimemuongezea maradhi ambayo hakuwa nayo hapo awali,


Usiku huo, watoto wake waliungana naye. Katika mazingira ya huzuni kwa hakika ulikuwa ni usiku wa mikasa,
tulikumbuka hadithi nzuri siku zote tulizo wahi kuishi na mpendwa wetu,

Ulikuwa umepita ukimia furani hivi sauti nzito ilio toka katika kinywa cha baba ilikuwa ikisikika huku akimwomba kaka aliekuwa ni mhitimu wa mambo ya theoloji,

Baba alimtaka kaka amwelezee kuhusu maisha baada ya kifo ambapo Mama angekuwa wakati huo.

Ndugu yangu alianza kuzungumza juu ya maisha baada ya kifo, na kubahatisha jinsi na wapi angekuwa marehemu mama kutokana na yote alio yaishi kabla ya kifo chake,

Kaka aliashiria utukufu alio kuwa akikutana nao mama huku kwenye ulimwengu wa wafu kadri alivyo mpamba kwa shela na maua ya waridi ni kama faraja ilio jaa tumaini juu yetu ilianza kuzitawala hisia zetu huku tukianza kupata tumaini juu mauti kutokuwa adha ilio watesa wengi,


Baba yangu alisikiliza kwa makini muda wote kaka akielezea kile alicho kiamini,

Tukiwa wenye huzuni miyoni,
Ghafla akatuomba tumpeleke makaburini.

Wote tukashtuka juu ya ombi lile!

Baba!" tukajibu, "ni saa 11 usiku, hatuwezi kwenda makaburini sasa hivi!"


Alipaisha juu sauti yake, huku sura yake ikiwa imejaa ghadhabu akasema tena"

"Msibishane na mimi, tafadhali msibishane na mtu ambaye amefiwa na mke wake wa alie ishi nae miaka 55."

Nasema msinibishie nyanyukeni twende makabulini sasa"


Kulikuwa na muda wa ukimya kwa heshima hatukuweza , kujari kumbishia tena baba juu ya amri yake japo ilionekana kuwa amri kadiri zaidi katika uwanja wa vita,
Makaburi hayakuwa mbali na nyumbani tulitembea katikati ya mbalamwezi kuelekea yaliko kuwa makaburi,

Baada ya kufika makaburini tulielekea lilipokuwa kaburi la mama na hapo tulimshudia baba akipiga magoti nakuiweka mikono yake juu ya kaburi,

Huku machozi ya uchungu yakimtoka alikuwa akiongea kwa sauti ilio jaa upendo na huku akiyataja maeneo yote walio wahi kuyafika akiwa na mama baba akawa anarejea yale maneno ya upendo aliokuwa akimwambia mama enzi za ujana wao huku machozi ya ghadhabu yakimtoka alikuwa akisema na kuimba nyimbo za kale kama ishara ya mwisho ya kumuaga mama,

Baba alikuwa akisema mke wangu umeondoka nakutuacha kama familia tumekuwa wote muda wote tumewalea watoto wetu nao leo wanao watoto wao tumefanya kila jema kwao lakini kifo hakikutaka uwaage kwa kuwapa mkono wa buriani,

Hakika umeondoka mke wangu nifuraha nilio omba miaka mingi iliopita utangulie kabla ya kifo changu ili nisikuhuzunishe zaidi pindi ambapo ningetangulia kuondoka,

Miaka 55 tulio ishi pamoja ninajua hakuna awezae kuhadithia khadithi ya miongo mitano hata kama wino utakuwa bahari na miti ikawa kalamu bado ni Mungu pekee alie jaa huruma ndie awezae kufungua kurasa za mchana na usiku katika miaka 55 tulio ishi mimi na wewe mama Bryani,

Khadithi ya mke na mme walio ishi katika ndoa miaka 55 ni simurizi tamu iwezayo kuwafufua wafu walio lala katika maeneo haya ndio maana nimekuja hapa mke wangu uliko lala ili jirani zako wayasikie mema yote ulio nitendea katika uhai wetu wa ndoa ya miaka 55"

Huenda wafu hawana ujirani lakini nyoyo za wafu hutembeleana nakuunga udugu juu yao'
Simulizi za kuzimu hutupata sisi tulio hai kupitia ndoto nina Imani mke wangu kifo chako kitakuwa ni ushujaa juu yetu ulio tuacha katika uhai wa kimwili"


Kisha baba akatulia na kujifuta usoni.

Na akatugeikia sisi huku akisema"

"Mimi na mama yenu tulikuwa pamoja katika maisha yetu yote.

Nilipo badilisha kazi
Na pindi nilipo uza Nyumba"
na kuhamia nje ya mji bado tulishiriki pamoja furaha ya kuona watoto wetu wakimaliza masomo yao, pindi tulipo ondokewa na wapendwa wetu tuliomboleza pamoja kuondokewa na wapendwa wetu bega kwa bega, tulisali pamoja kila mala kwenye chumba cha kusubiria wagonjwa ndani ya baadhi ya hospitali, tulisaidiana kwa maumivu, tulikumbatiana kila Krismasi, ilipo fika na tulikuwa tunasamehena makosa yetu na kuyaendea mapito mapya pasina chuki mioyoni mwetu"


Kwa sababu mama yenu ameondoka mbele yangu.

Hakupaswa kupitia uchungu wa kifo changu na uchungu wa kunizika,

kuachwa peke yake baada ya kuondoka kwangu.

Mimi ndiye nitapitia hayo, na ninamshukuru Mungu. Ninampenda sana hata nisingependa ateseke…”

Baba alipomaliza kusema hayo, mimi na kaka zangu machozi yalikuwa yakitutirika usoni mwetu.

Tulimlaki na kumkumbatia, nae akatufariji,
"Ni sawa, tunaweza kwenda nyumbani sasa imekuwa siku nzuri kwetu nina Imani itakuwa ni simuri nzuri kwa kizazi chenu"

Usiku huo nilielewa mapenzi ya kweli ni nini;

Pia soma: Ushuhuda wa ndoa ya wazazi wangu, baba aliachishwa kazi ghafla miaka 14 iliyopita. Mama amekuwa ndio kila kitu

Moyo wangu ulipata funzo jipya kuwa mapenzi ni nje ya Ngono, kumbe mapenzi ni utu na kujaribu kujari kwa ukaribu hisia za mwenza wako nikafahamu kuwa mapenzi ni begi la utu na kujali hata kama kujitolea kwako kutapelekea kupata kovu bado mapenzi kwa ulie mpenda yatatakiwa kuwa hai hata baada ya kifo"

Baba aliinua juu macho yake japo ndevu zake zilikuwa ni nyeupe sana bado mikono yake ilijaa hamasa kila alipo inyanyua juu tuliona ufalme juu yetu huku mioyo yetu ikijisemea kifo cha mama ni ushindi dhidi ya dhuruma za kimapenzi"

Niliinama na kulishika kaburi la mama huku nikisikia moyo ukisema"

Mama utadumu milele miyoni mwetu (I love ❤️ mama')

Ndugu msomaji wangu kumbuka Makaburi yanaishi'

Tuwapende nakuwajali wale tulio wachagua kuishi nao katika Mahusiano yetu"

Asante kwa kusoma uzi huu"

aa12f156a7ac4aab95e843377efe3668.jpg
 
Back
Top Bottom