DLRider
Senior Member
- Mar 5, 2019
- 134
- 143
Wote tumekuwa katika mapenzi. Kwa bahati mbaya mapenzi huwa yanaumiza na watu tunaumia sana hadi baadaye ndio hayo maumive yanatupa mafundisho. Tusaidiane kwa kuandika visa mbalimbali vya tulivyoumizwa na wapenzi wetu.
Mimi Nitaanza:
Mwaka juzi nilimpenda sana mdada mmoja Arusha. Tukawa na mapenzi motomoto kwa mwaka mzima. Kwao nikaenda kujitambulisha na zawadi kabambe nilitoa mara kwa mara. Huyo msichana nilimpenda kweli yani mtu ungeniambia anakasoro nisingekuelewa. Kitandani na kwingineko mambo yalikuwa moto balaa. Alikuwa anajua kupika balaa. Alikuwa anachapa kazi hadi magari anaosha. Japo kuna wafanyakazi, ila na yeye alikuwa anafanya hizo kazi sana.
Huwa naenda abroad kuangalia mambo yangu huko sababu niliishi huko miaka mingi. Tukawa tunawasiliana kila siku kwa wiki 2 za kwanza baada ya mimi kuondoka vizuri tu. Kisha ikawa kwamba nikimtafuta mara nyingine sio kama mwanzo. Nikaamua huyu cha kufanya ni siku narudi waa simpi taarifa. Alikuwa amehamia kabisa kwa nyumba yangu. Siku nimerudi hata sikutoa taarifa kwa mtu yeyote aje airport kunipokea kama kawaida ilivyo siku nyingine. Siku hiyo nikakodi texi. Nafika home usiku saa tano hivi, nikaona mlinzi kama anasua sua kufungua anasema funguo ameiacha ndani nyumba kubwa wakati siku zote kuna jengo la gereji karibu na geti na funguo zote za geti zinakuwa hapo. Nilishaanza kuhisi kitu. Nikasema kimoyo moyo kuna mwanaume ndani kwangu. Tuna tools mbalimbali pia kwa gereji, nikawa mkali nikasema akate kufuli. Akaenda gereji akaleta bolt cutter, akakata kufuli.
Mimi kuingia tu getini, roho juu juu nikawahi nyumba kubwa kwenda kupata vidhibiti. Na siku hiyo hata mlango wa nje haukufungwa. Nikaingia tu bila hodi nikiwa nimejiandaa kumkuta mpenzi anapigwa vitu. Nilipoingia sebule, nikamkuta bibi yangu yuko mwenyewe akiwa amenawiri kweli kweli. Nikamkumbatia vizuri na kumbusu. Kaperfume kazuri kabisa yani amenawiri haswaa. Na ni mrembo balaa. Nikajifanya naenda chumbani kuweka vitu. Nikakuta hamna kitu. Nyumba ina rooms kumi, nikafikiria ninaanzaje kukagua hizi rooms nyingine? Lazima kuna mwanaume katika hizo rooms nyingine. Ila Namwambiaje sababu sikutaka ahisi ninamhisi?. Pia badala ya kufurahi nimerudi, akawa kama anashangaa kuniona. Basi nikaona anamendea simu yake. Nikajua hii simu ina kitu.
Nikamwambia leo ndio nataka kujua kwamba wewe ni mwaminifu au hapana naomba nikague simu. Akakataa kabisa. Nikamwambia utanipa tu leo, na niko nawe bumper to bumber, haufuti kitu. Unakataa sababu kuna bomu hapo. Nikamwita mlinzi awe kidhibiti changu. Kwa hiyo hapakuwa na mtu getini. Baada ya muda kama nusu saa, gari inapiga honi getini. Kwa ukali nikamwambia mlinzi, ufungue hilo geti na huyo mtu umlete hapa, usipomleta leo kila mtu anakula bstola. Nishachukia mimi. Hapo bado simu sijafanikiwa kuipata, ilatayari nimewasiliana na rafiki yagu polisi. Nikamwambia mlinzi fungua hilo geti na usiseme kitu, huyo mtu aje kama anvyokuja siku zote.
Muda si muda, jamaa akaja wala hakuppiga hodi akafungua mlango akaingia. Funguo ni moja ya ndani nikafunga mlango, nikaweka funguo mfukoni, kisha nikaendea bastola kwa safe place naiweka chumbani nikasema mtu akileta vurugu namfyatua. Wote mko chini yaulinzi hadi polisi waje. Polisi akaja na rafiki yake ndio chini ya amri ya polisi, nikapata simu nikakuta mabomu ya kutosha. Ningeweza kumnyanganyakwa nguvu, ila sikutaka kuonekana mkatili.
Msichana akaamuriwa kuondoka kama nilivyoamuru. AKAONDOKA NA GARI LA JAMAA. IMAGINE!. Ila usiku mzima akawa ananipigia na anatuma meseji za samahani. Kumbuka mwanzoni alikuwa ni mchapa kazi sana, sasa NIKAAMBIWA NILIVYOONDOKA ALIKUWA ANAANGAIA TV SIKU NZIMA. Ile kupiga kazi ni kujipendekeza tu kwangu kumbe nikiwepo. Baadaye nikajua mambo ya ajabu sana ya kumhusu huyo mdada aliyonificha kwa mwaka mzima wala sitayasema hapa. Ila nikajua usifikirie unamfahamu mtu.
Nilijifunza kufanya utafiti sana kuhusu mwanamke na pia kutomleta kwako hadi umjue kabisa sababu baada ya kumfukuza aliwahi kuja usiku wa manane anatuma meseji anasema najiua hapa getini kwako. mara tatu usiku tofauti tofauti.. anabisha getini akijua nitamruhusu aingie. Ila sababu mimi si mkatili, kila usiku nilita tu polisi wanakuja wanamchukua. Siku ya tatu nikafanya restraining order akaambiwa ukienda tena unaishia mahabusu. Hakurudi tena. Huo ni mkasa wangu wa 3 na baada ya hapo nimepoteza kabisa matumaini ya kuoa sababu huyo ndio nilijuwa ni yeye tu. Ila nikadungua ni muuaji na mnyama kabisa. Jamaa aliyekuwa anamkula ni ex wake.
TAFADHALI NA WEWE TUPE KISA CHA YALIYOKUKUTA KATIKA MAPENZI. SIO LAZMA UANDIKE KIREFU HIVI. Hata maneno ya sentensi chache tu yanatosha. Asanteni wana jumuia. Hii itatupa fursa kujifunza kwa makosa ya mwingine.