Ushuhuda wangu juu ya biashara ya kuandika proposal inalipa 100%

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Habari za jioni wapambanaji, Nawasalimu kwa jina la jamuhuri.

Mimi ni kijana mtafutaji, lakini tokea nipo chuo(Mzumbe) nilijikuta napenda tu kuandika proposal za biashara, kipindi hicho tulikuwa tunaandika wakati wa zile party za kukaribisha wanafunzi wapya maarufu kama freshers Bash. Basi tulikuwa tunapeleka kwenye makampuni ya vinywaji, kama bia au soda na wadau wengine, zile proposal bwana zikawa zinajibiwa na sisi kupata mkwanja wa kuendesha maisha ya chuo.

Aisee tumeandika proposal nyingi sana, mpaka naingia mtaani nilikuwa sina kazi yoyote ila dili zangu zilikuwa ndio hizo. Baada ya miaka kadhaa leo hii nimejikuta nmefungua ofisi yangu mwenyewe ambapo nafanya shughuli zangu za Mwanasheria lakini proposal ndio zinanipa pesa zaidi.

Karibuni sana GETRICH BUSINESS CONSULTANTS, Buguruni rozana kwenye jengo la Rozana Complex frame namba Moja na simu 0710 782874. Ahsante.
 
Kwa hiyo wewe ndiyo Get Rich, Mzee wa kufukua makaburi ya watu, au ni majina tu yamefanana?
 
Hapana mkuu ni majina tu yamefanana mimi ni GETRICH BUSINESS CONSULTANTS ningefukua makaburi ya watu BRELA wasingenipa Cheti mkuu, Karibu sana tufanye kazi
Kwa hiyo wewe ndiyo Get Rich, Mzee wa kufukua makaburi ya watu, au ni majina tu yamefanana?
 
Hahaha Hapana bwana, Ukija ofisini au ukinipigia utajua mimi sio huyo bwana, Kwanza yeye haandiki proposal anaandika Assignment za chuo.
Ni mwijaku huyo usiumize kichwa
 
Hahaha Hapana bwana, Ukija ofisini au ukinipigia utajua mimi sio huyo bwana, Kwanza yeye haandiki proposal anaandika Assignment za chuo.
Ni mwijaku huyo usiumize kichwa
 
kuna mtu amenitumia email leo, nami nimemtumia sample mbili. so kama na wewe unataka nipe email yako nikutumie boss.
So hauna ata sample work yoyote kuonesha soko lako la mtandaoni
 
Eti ni mwandishi wa proposal[emoji23][emoji23][emoji23]
Samahani mkuu kwani ni dhambi gani nimefanya hapo ? Nimekubali ndio hapo nimekosea grammar na nimerekebisha boss, kunikebehi, kunidharau, na kunidhalilisha si jambo jema, najua inawezekana umenipita elimu, kipato, wadhifa, na hata weledi lakini nia yangu kuu ilikuwa ni kuwapa moyo vijana wengine ambao hawana ajira na labda wana kipawa cha kuandika proposal. Anyway Mungu akubariki sana katika shughuli zako na ukafanikiwe sana kwa kuwa wewe ni bora sana na mweledi katika kazi zako.
 
Kila siku nasisitiza.... Unapoandika Tangazo acha porojo..
Weka Biashara yako mwanzo kabisa kisha uendelee na motivesheni zingine.....

Kuna watu wengi hatusomi mabandiko hadi mwisho... Hvyo utakosa fursa...
 
Naona umechanganya proposal na issue nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…