MABADILIKO KATIKA JAMII
Naomba kidogo tu nizungumzie jamii yetu iliyotuzunguka ila kwa sasa, sitopendelea sana kukizungumzia kizazi kilichopita kwasababu sina uelewa wa kutosha juu ya maisha ya wakati huo yalikuwa yakoje. Lakini naamini na kuwa yalipitiwa na mabadiliko kulingana na wakati pamoja na mwingiliano wa jamii nyengine. Maswali ya kujiuliza ni je?
(1)Athari za mwingiliano huo zilipokelewaje katika jamii husika?
(2)Walishuhulika nazo vipi tabia mbaya/potofu zilizoingia katika jamii zao ambazo hawakuridhika nazo?
(3)Je waliziacha ziwe mwendelezo kwa vizazi vijavyo hadi kutufikia sisi? Tukiachana na jamii zilizopita Tanzania/Afrika Mashariki kwa ujumla, tukikodolee macho hichi kizazi kiliopo sasa (new generation) na hasa hiki tunachokiita kizazi cha taifa la kesho.
Kuna usemi usemao
"asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu". Maana ya usemi huu ni kuwa mama/wazazi ndiyo walimu wa mwanzo wa mtoto. Mtoto hupokea na kuiga kile anachokikuta katika jamii yake kuanzia lugha na mengine mengi anayofundishwa akiwa nyumbani, shuleni na hata katika mazingira mazima yanayomzunguka.
(4)Sasa jamii yenyewe kama haitilii mkazo kufuatwa kwa mila, desturi na maadili mema, kweli huyu mtoto ataongoka?
Tukimuangalia huyu mwalimu wa pili ambaye ni ulimwengu (anayesaidiwa sana na teknolojia) hufundisha mengi na wengi kwa wakati mmoja. Ukweli ni kwamba hakuna chenye faida na kikakosa kuwa na hasara. Kupata faida ndiyo kusudio letu
(5)Bali hizi hasara zinazojitokeza tunadili nazo vipi? Swali jengine.
(6)Hivi huu utandawazi, kila kinachokuja kupitia hili lazima tuige? Zaidi nabaki kuwashangaa wale wasemao "vijana wa siku hizi hao wa sayansi na teknolojia, we waache tu!!". Na vijana nao unawasikia wakisema "madingi wa siku hizi utawaweza, kila kitu kwao kero, yani we achana nao tu".
(7)Jamani tukiwa na mtazamo kama huu kweli tutafika? Jambo baya zaidi linalojitokeza katika jamii yetu kwa sasa ni kurushiana 'kipira', kila mmoja msafi yeye na kwake hana kosa. Wananchi hutupa lawama zao kwa serikali, wanafunzi kwa walimu, waume kwa wake zao, wafuasi wa dini kwa viongozi wao wa dini na hadi katika *jinsia
(gender)*. Na kila anayetupiwa lawama (kuhusu mabaya kuongezeka/mmomo nyoko wa maadili) huzirejesha kule kule zinapotokea.....
Ni kweli kuwa kila mwamba ngoma huvutia upandewe.
(8)Lakini iwe hata katika hili la kutaka kuondosha tofauti na kuipa jamii mwelekeo mzuri?
Ni matumaini yangu kuwa kama jamii itashikamana na kutilia mkazo juu ya kuondoa mabaya yanayoikabili jamii yetu hasa kwa kukiokoa kizazi kijacho (taifa la kesho) basi tutafanikiwa. Hizo ni FIKRA zangu tu ila "katika maisha halisi, changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na potofu, kwani mwisho wa fikra ni matendo, pale fikra hazibaki kuwa fikra...."