Ushukuriwe uchawi/wachawi kwa ujumla

Ushukuriwe uchawi/wachawi kwa ujumla

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
Wachawi japo tunawakemea vikali sana, lakini mimi nashukuru uwepo wao kwa kiwango kikubwa!

kusingekuwepo uchawi, sijuwi hali ingekuwaje?!

wote tunajua Mungu yupo lakini si wote wanaomwamini & kumtii ipasavyo;

UUNGU & UCHAWI yote yapo kiimani, lakini kubali usikubali: wanaoamini uchawi ni wengi kuliko wanaomwamini Mungu.

*ukiona mtu anaogopa kukufanyia mabaya, si kwasababu anajua ni dhambi bali anaogopa kwa kuhisi utamroga!

*ukiacha mali yako sehemu ambayo unahisi si salama na ukaikuta salama, basi mtu kaogopa kurogwa wala si vinginevyo

Uchawi una faida nyingi ambazo siwezi kueleza hapa, lakini elewa kwamba uchawi unasaidia..(nazungumzia faida kwa jamii sio kwa mchawi)

Kama unakubaliana na mimi, ongeza faida moja hapa;
 
Shida ni pale mtu anapolazimisha faida kwa jambo lenye hasara tupu.

Na hapo wala hakuna faida ya uchawi uliyoitaja.

Ukiona mtu ameacha kukuibia kwa kuhofia kuwa utamroga ilhali wewe sio mchawi kweli, basi hapo kilichomfanya asikuibie ni ujinga wake wa kutokujua kuwa wewe si mchawi, na wala sio uchawi.

Hivyo kilichokunufaisha ni ujinga wake na sio uchawi.
 
Wachawi japo tunawakemea vikali sana, lakini mimi nashukuru uwepo wao kwa kiwango kikubwa!

kusingekuwepo uchawi, sijuwi hali ingekuwaje?!

wote tunajua Mungu yupo lakini si wote wanaomwamini & kumtii ipasavyo;

UUNGU & UCHAWI yote yapo kiimani, lakini kubali usikubali: wanaoamini uchawi ni wengi kuliko wanaomwamini Mungu.

*ukiona mtu anaogopa kukufanyia mabaya, si kwasababu anajua ni dhambi bali anaogopa kwa kuhisi utamroga!

*ukiacha mali yako sehemu ambayo unahisi si salama na ukaikuta salama, basi mtu kaogopa kurogwa wala si vinginevyo

Uchawi una faida nyingi ambazo siwezi kueleza hapa, lakini elewa kwamba uchawi unasaidia..(nazungumzia faida kwa jamii sio kwa mchawi)

Kama unakubaliana na mimi, ongeza faida moja hapa;
Kuna baadhi ya mikoa mtu akikwambia utajuta ehhh utashangaa mvua inanyesha kwako tu siku nzima na ndani yanatokea mafuriko
 
Wachawi wanaroga watu wadhaifu wenyewe wanajua nguvu ya Mungu ndani ya watu wake. .
 
Mungu ana watu ambao ni wake na sio wake ?

Na yule anayeomba kila siku ili so called mchawi apate shida aangamie sio mchawi ?

Uchawi ni nini ?
 
Back
Top Bottom