Hii sheria ya kijinga kweli, yaani ununue gari ulitumie ndio ukileta upate punguzo la ushuru, badala ya kuhamasisha kuleta gari mpya ndio upewe punguzo la ushuru, serikali yetu na sheria zake zinazotungwa na wachaga wa pale TRA zinatuhamasisha tulete ma-scrap! ajabu kubwa hii.
Ingekuwa, ukitoka nje, kama unasoma au kufanya kazi huko, hakikisha gari lako ulilokwisha kulitumia bovu bovu, liache huko huko na jaribu kuja na jipya au jipya jipya (kama una uwezo) na sisi (serikali) kukuhamasisha na kuhamasisha wengine wafanye bidii ya kwenda nje, tutakupa ahueni ya ushuru asili mia 100. Au mtu kakaa anasoma, ka save vipesa vyake, kajinyima hata kula vizuri huko nje ili akirudi anunuwe gari japo sekeni-hendi aje nalo, naye japo aonekane kweli katoka nje, anaambiwa mpaka awe amekaa nalo huko nje zaidi ya Mwaka, sasa hii ni akili kweli?
Hii mitunga sheria ya nchi yetu inatunga sheria za kiroho mbaya tu, misheria ya kukomoana tu. Hivi lini tutajikombowa japo kwa kuwa na sheria za kusaidiana badili ya hizi za kukomoana. Hiki kipengele cha ''zaidi ya mwaka mmoja'' kina husu nini? na kina faida gani? Hata mtu akienda katika ki semina au ki shoti-kozi cha miezi miwili, akajipatia kigari chake cha dola elfu mbili, ukimsaidia ushuru si umemsaidia maisha yake na usafiri na umehamasisha yeye na wengine kufanya bidii ya kwenda huko nje? Hii fikira ya kuwa magari ni kitu luxury, ililetwa na nani hasa?