Ushuzi uloujamba

X-PASTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
11,605
Reaction score
1,843
USHUZI ULOUJAMBA

Ushuzi ulotandika, ndugu sikunjiye puwa
Ukajifanya kumaka, samahani ukapawa
Mja ukahuzunika, mithili ya alofiwa
Ushuzi uloujamba, puwa waikunjiyani?

Waikunjiyani puwa, na kumbe ndiwe aswili
Udaku ulidakuwa, tukashindwa kuhimili
Ukajifanya mjuwa, waja wasikukejeli
Ushuzi uloujamba, puwa waikunjiyani?

Kamwe sitokusitiri, kukoma usipokoma
Kujifurisha kidari, kujidai mwenyi ngoma
Kuwarukiya mahiri, kuwafanyiya shutuma
Ushuzi uloujamba, puwa waikunjiyani?

Kibwebwe wajifunganya, na kujifanya Imamu
Malenga wawasengenya, kwamba ni waso timamu
Kumbe wausaka mwanya, unyiye mastakwimu
Ushuzi uloujamba, puwa waikunjiyani?

Kula siku kigaroni, wafurisha matukano
Ushajileta weleni, ndiwe mwenyi farakano
Kumbe ndiwe majununi, mawele wacheka ngano
Ushuzi uloujamba, puwa waikunjiyani?

Bure kujifanya seti, eti u Kadhi Mkuu
Ukawapima kwa futi, wenziwo kuwanukuu!
U kibanda cha makuti, kidebe kikuukuu
Ushuzi uloujamba, puwa waikunjiyani?

Mesha ya kukukosowa, Manju nenda piga mbizi
Usite kutuzuzuwa, kwa mambo tusomaizi
Ya mnuko kukohowa, kutushutia mashuzi
Ushuzi uloujamba, puwa waikunjiyani?
 
Nidhamu wazee hayo mashairi yaimbe kimoyoyo wewe na kichwa lako.
 
Nidhamu wazee hayo mashairi yaimbe kimoyoyo wewe na kichwa lako.
Ndio kitu gani hii mkuu!

Tatizo la kutosoma Fasihi, leo hii unapata tabu kutambua kilicho andikwa.
 
Nidhamu gani mkuu,au mwenzetu haujambi?

Mkare_wenu polezo, fasihi kutoijuwa
Alosema X-Paster, siyo hayo ulodhani
Aongea kisanii, lughaye i pichani
Ushuzio ushatoa, tena kwa wako mdomo.

Wanatamba wanomudu, lugha hii kiundani
Tembo wanamwita simba, hayawani taelewa
tafsiri sichukue, sisisi kama ilivyo
Tafrani tataka leta, kwa wako ulimbukeni

Ushuzi ukiutoa, utolee 'kishuzio'
Ikibidi kuutoa, utolee jalalaani
Utanuka kama taka, kwa watu kuutambua
Kwa mdomo siutoe, utanuka mara mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…