Usiache kujifunza hata kama unahisi umefanikiwa

Bodhichitta

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
315
Reaction score
762
Aslaam

Wahenga walisema elimu haina mwisho, ni kweli kabisa elimu haina mwisho, haina mwisho, haina mwisho.

Imekuwa kawaida katika Maisha watu hupenda na kutaka kufanikiwa lakini cha ajabu ni wavivu wakujifunza juu mambo mbalimbali eidha yawe mapya au yale ya zamani ambao kwa wao hawajahi kujifunza.

Elimu ni kama maji kwenye bustani, hata kama maua yapendeze vipi bado yataendelea kuhitaji maji ili yaendelee kupendeza zaidi

Hiki kisa kitakusaidia kuona umuhimu wa kujifunza katika Maisha:

Mchezaji mmoja (top score) siku moja alienda mapumzikoni katika hoteli moja ya kifahari, sasa akiwa pale ghafla akaona matajiri wanakuja na magari ya kifahari, baadae wakaingia miongoni mwa chumba kimoja cha mikutano kwenye ile hoteri, baada ya muda kidogo wakatoka.

Siku ya pili walikuja tena wakatumia masaa kadhaa wakatoka, wakaja tena siku ya tatu, yule mchezaji ikabidi amfuate mmoja wa matajiri na kumuuliza

Mchezaji: Habari, nimewaona kama siku tatu mnakuja na kuondoka hapa, mnafanya nini?

Tajiri: salama, tuko kwenye semina hapa tunajifunza mambo kadhaa.

Mchezaji: wewe si Tajiri mkubwa? Kuna haja gani yakuendelea kujifunza wakati tayari umeshafanikisha na kila kitu unakipata?

Tajiri: kabla hajijibu swali lake nae ikabidi amuulize, wewe si mchezaji? Tena ni mfungaji bora?

Mchezaji: ndio

Tajiri: kwanini kila siku unafanya mazoezi wakati tayari umeshafunga magori mengi?

Mchezaji: nataka niendelee kuwa mfungaji bora, na ukiangalia ligi yetu ina ushindani mkubwa, usipofanya mazoezi ninaweza nisifanye vizuri na nikapitwa na wengine nikakosa hii nafasi

Tajiri: sawa kabisa, nahiyo ndio sababu na sisi matajiri tunatakiwa kujifunza kila siku ili kulinda tulichokuwa nacho lakini pia kujua njia ya kukiongeza ikiwezekana. Ili kufanya hivo tunatakiwa tujifunze mambo kadhaa kwenye biashara zetu ndo maana unatuona tuko hapa.

Mchezaji: Nikweli, nashukuru na kwaheri!

Huu ndio umuhimu wakuendelea kujifunza juu ya kile unachokifanya, tujitahidi kujifunza zaidi kila tupatapo nafasi yakujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…