Usiahidi mbingu wakati mawingu huyafikii. Don't promise the sky while the clouds are out of your reach!

Usiahidi mbingu wakati mawingu huyafikii. Don't promise the sky while the clouds are out of your reach!

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
245
Reaction score
314
Tukumbushane ahadi,

1. Serikali ikikamata makenikia itabamizwa mahakama za kimataifa. Hewa!

2. Huu ni mwaka wa kudai demokrasia lazima katiba na tume huru kabla ya uchaguzi. Hewa!

3. Tanzania itatengwa maana dunia ni kijiji. Hewa!

4. Uchumi umevurugwa nchi itaingia matatizo makubwa ya kiuchumi. Hewa!

5. Nchi itaangamia kwa Corona maana Raisi anapuuza maagizo ya WHO. Hewa!

6. Benki ya Dunia imekataa kutoa mkopo kwa Tanzania mpaka iruhusu mimba mashuleni. Hewa!

7. Nguvu ya umma itatumika kuilazimisha serikali iruhusu mikutano na maandamano maana ni haki ya kikatiba. Hewa!

8. CCM itasambaratika ilimfukuza. Hewa!

9. Jumuia ya kimataifa itaingilia kati kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu nchini. Hewa!

10. Tutajenga ukuta. Hewa!

11. Tutaunda Serikali zetu za mitaa na tutaagiza wananchi wasitoe ushirikiano Kwa waliochaguliwa kiharamu. Hewa!

12. Wapinzani tutaungana uchaguzi mkuu. Hewa!

13. Tutaunda kamati za kuorodhesha vifo vya koviki naintinyi. Hewa!

14. Safari hii sio mafuriko ni Tsunami. Hewa!

15. Tutamshitako Raisi lazima tumburuze mahakamani kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria. Hewa!

16. Acacia hawatalipa hata senti moja. Hewa!

17. Tutazuia bajeti isipite. Hewa!

18. Mapato ya serikali yatapungua kwa kuwa wanasumbua wawekezaji. Hewa!

19. Hatumtambui raisi wa Zanzibar na tutamwapisha babu. Hewa!

20. Hatumtambui JPM. Hewa!

Hivi tutaaminije ahadi mpya? Muwe mnaahidi vinavyotekelezeka. Hebu muigeni Mzee Hashim. Ukiacha suala la kurefusha bahari huwa anaahidi vinavyotekelezeka na anaweza kuwafanyia surprise!
 
Lakini Mungu ni mwema Sana, Rais wetu anayemaliza muda wake na huyu mpinzani wake sasa, wote ni kulwa na doto

Tofauti zao ni ndogo Sana, Tanzania tumepatikana aisee, wote wanaochuana wanafanana haswa, wanaweza kutofautiana kwenye uthubutu tu peke yake, nahisi Magufuli ni Jasiri haswaa katika kufanya na kulisimamia Jambo,

Najiuliza hasa kwenye swala la Corona, angelikuwa huyu mpinzani wake angekuwa na maamuzi kama ya Magufuli kweli? Isingewezekana

Kulivumavuma njaa kipindi Fulani Baadhi ya maeneo ya nchi yetu, mgombea Uraisi alilishikia bango la kumtaka Raisi akaombe msaada, naukumbuka msimamo wa Magufuli ingawa sina hakika kama ulikuwa na faida ama athari yoyote kama angeomba msaada wa chakula,

Magufuli alishikilia kile alichokiamini kuwa, hakuna atayekufa na njaa na hataomba msaada, ingawa vitisho vya maneno vilikuwa ni vingi kutoka Kwa wapinzani wake

Bwawa la umeme, kulipita vitisho nje ya nchi na ndani ya nchi,mashirika ya Kimataifa na ya ndani ya nchi, kiasi hata Watanzania wengi walianza kuyumba,wasomi wetu wengi nao walianza kuogopa, lakini Magufuli alishikilia palepale, Magufuli Kwa ujumla anazo Siri nyingi katika ulimwengu usioonekana, ulimwengu wa roho na ndiyo maana aking'ang'ania kitu, tumwamini ni lazima kitakuwa vile alivyokiona yeye

Hata hili la Tanzania si masikini, ni Jambo la Kiroho kabisa, watu wasioijua hiyo siri, hujikuta hawafikii malengo yao Kwa sababu ya Historia ya nyuma, maneno uliyotamkiwa nyuma na wazee, huleta matokeo katika maisha ya mtu, tuliimbiwa Sana huo wimbo wa Tanzania ni maskini na ulituingia vya kutosha,

Binafs huyu Mzee, Kura yangu na watu 15,000 na, naendelea kumpigia Kampeni ili pengine hiyo no iwe kubwa zaidi tutakaompa kura
 
Hiyo ni IQ test kwako, matokeo nasikitika kukwambia kwamba siyo mazuri sana, kwani ni below average, ...

Sijawahi kutarajia lolote zuri kwako, wewe ni mataga uliyekwapuliwa ufahamu (kama ulikuwa nao kabla)... hivyo huwe kuwa standard ya IQ test.
 
Back
Top Bottom