Usibadili gari yako kutoka kawaida kwenda push start

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,238
Reaction score
4,885
Usibadili gari yako kutoka funguo ya kawaida kwenda push start..hii ni kwa sababu unapunguza usalama wa gari lako ambapo ni rahisi sana kuliwasha kwa kuunga waya tu

Kwa kawaida gari inapotoka kiwandani iwe push start ama kawaida imewekewe ulinzi maalum wa mfumo wa ku lock steering unapoizima gari ..ambapo mfumo huo ni mfano wa kufuli la chuma ambapo huwezi kuivunja mpaka ufungue na funguo husika ndipo linafunguka na linapofunguka steering ndipo inakua huru kuzunguka unapokata kona.

Gari zinazokuja na push start zina mfumo wa kufuli la umeme ambalo hufunguka automatically pale ambapo antenna za ndani zinaponasa mawimbi ya kielektroniki ya funguo ama remote ya gari husika na hufunga pale unapozima gari.

Kwa gari ya kawaida kufuli hufunguka unapochomeka na kuzungusha funguo wakati uapotaka kuwasha na hulock pale unapozima gari na kuchomoa funguo

Sasa basi kwa sababu gari ya kawaida isio push start kufuli lake hufunguliwa tu na funguo yake ya mechanic ukitaka kufunga mfumo wa push start utalazimika kuchomeka funguo kwanza kutoka lock ya kufuli.. hivyo kwa sababu hiyo wanaofunga wanalazimika kuondoa kabisa kufuli la ku lock steering na kuiacha ikiwa free .muda wote kitu ambacho kwa usalama wa gari lako umeshapungua kwa asilimia 50

Tatizo la pili ni kua kwa sababu wanaondoa kabisa kufuli na kufuli ndio lina connector za umeme zinazowasha gari na kuweka switch on na acc wanakata waya na kuziunganisha kwenye mfumo?wa push start (kumbuka mfumo huu sio rasmi hivyo una mapungufu mengi) ili mfumo huu uunganishwe na mfumo wa gari..Sasa basi kuna uwezekano mtu asie mwema akatumia zile waya zilizokatwa na akaziunganisha gari itapiga starter na itawaka pia na kuna uwezekano akaondoka nalo kiulaini sana

Kumekuwa na kesi za watu wengi kuibiwa magari sana ,ni muhimu sana kuzingatia usalama wa gari lako na ulizi usifanye mambo kwa kuiga huo ndio ukweli yana gharama kubwa sana za kiusalama. Ushauri Kama unatamani gari la push start ni bora uuze ulilokua nalo ununue lenye mfumo wa push start iliotoka nalo kiwandanani

Kwa ushauri wa mifumo ya funguo tafadhali tembelea page yetu instagram.com/smart_keys_tz
Simu namba 0657587593

Tunafanya programming ya funguo za sensor na remote za push start kwenye mfumo ulokuja na gari.

Kwa waliopoteza na wanaohitaji za spea kwa magari aina zote.

/-

sent from HUAWEI
 
Ahsante kwa hii elimu.
 
Katika upuuzi ambao unakera ni pamoja na wamiliki wa magari wanaofanya modification za kitoto kama kuweka maffler ili gari iwe na mgurumo mzito ile hali engine yake ni ya kawaida, kuweka huo mfumo wa push-start wakati gari haikuja hivyo, kuweka matairi yametokelezea ubavuni na kuinyanyua gari kipuuzi, kuweka weka mataa hovyo hadi gari linakuwa kama club, kuweka weka mastika ya hovyo kwenye gari, sijui kuweka makitu yananing'inia kama antena au bawa la ndege nyuma au juu, kuweka marim ya size kubwa ambayo hayana hata impact kwenye utendaji wa gari.

Yaani haya mambo huwa yananikera sana.
 

Kuna kma rubber flani watu wanaweka kwenye milango ya gari zinakuwa zina rangi kede kede. Hii nayo sijajua ni nin na kila naemuuliza hajui, Ni sound proofing au ushamba gani ule??
 
wanajua fashen kumbe wanaharib gari kabisa
 
Nilijua niko peke yangu.
 
Zinasaidia kutoumiza magari ya wengine unapofungua mlango kwenye parking za kubanana
Najiuliza kama mtu umeweza kuweka ile rubber unashindwaje kufungua mlango wako kistraarabu usiumize wengine.......... Asante kwa elimu mkuu, sikuwa naelewa maana yake kabisa.

Sent from my SM-G930L using JamiiForums mobile app
 
Zinasaidia kutoumiza magari ya wengine unapofungua mlango kwenye parking za kubanana
Bado hai make sense, huu upuuzi uko TZ tu hasa kwa wale jamii ya IST, raum, spacio and the like.

Ni wale wanoingia kwenye ulimwengu wa magari na bado tongotongo la ulimbukeni halijawatoka.

Eti inazuia nini? Hahahaha...

Hebu jirekodi voice clip hicho ulichoandika alafu ujicheke [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna kma rubber flani watu wanaweka kwenye milango ya gari zinakuwa zina rangi kede kede. Hii nayo sijajua ni nin na kila naemuuliza hajui, Ni sound proofing au ushamba gani ule??
Zile rubber zunasaidia mlango wako usikwangue rangi ya gari lililopaki karibu na wewe endapo nafasi ni finyu pale unapofungua mlango...
Pia ni urembo japo sizipendi hata kidogo...
 

Ni kweli lkn inakuhusu nini,mke wangu mbaya ni kweli lkn inakuhusu nini,sema we sema wewe sema we sema wewe hata kama ningekua mimi ningesema mambo yamezua mambo na mambo yamezua jambo.
 

Sasa ukimiliki Discovery 4 nani atakwangua gari yako ukiwa umeipark?
 
Mkuu gari ina reflect personality ya mwenye gari kwa mfano picha za hizi JZX110 hivi ni sawa sawa ila zina reflect personality 2 tofauti...













 
Hahahahahha kwahio mkuu gari yako ina rim za mkokoteni au jiko zile πŸ˜…?

Kiukweli mie ni shabiki wa ku pimp gari sio siri ila sio kwa kiwango kinachozidi muziki mzuri in case gari yangu ina poor sound production na decent rims! Ukiongeza na tinted windows its more than enough to me.

Ile ya kujaza mataa na mastika kama gari ya Wasafi Media naona ni upuuzi pia na kuweka ma offset rim yaliotokeza nje yale ya kichinaπŸ˜… inakuwa kama uluga luga flani bila kusahau ngao kama za ndege πŸ˜…! Vijana wa Subaru na Altezza ndio wanaongoza kwa kujaza mataa mpaka kwenye rim za gari πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…