Shanily
JF-Expert Member
- Nov 4, 2024
- 856
- 1,662
Mwanamke akishapenda sehemu, Cha kwanza huwaza kuzaa( kumzalia huyo mwanaume) akidhani kwamba akimzalia ndo atamtuliza na mwanaume anazidisha mapenzi kwake kwakua wamezaa.
Zaa ukiwa na Utayari ndani ya nafsi Yako wa kumlea huyo mtoto, ukiwa na Utayari hata kama ikitokea mmetengana huwezi kuweka chuki dhidi ya mtoto wako , utamlea kwa mapenzi, hata upitie vikwazo gani utapambana ukiwa nae , huwezi mtupa Wala kumgawa kwakua ulimhitaji kutoka nafsini mwako.
Wazazi wengi siku hizi hawana mapenzi na watoto wao, Moja ya sababu Huwa ni hii, alizaa kwakua mwanaume alitaka au alizaa akijua mwanaume atazidisha mapenzi , ikitokea mwanaume kamtelekeza hasira zote anahamishia kwa mtoto, mtoto anakuwa kama mtumwa kwa mama yake wa kumzaa.
Watoto ndo hujenga jamii ya baadae , ili kujenga jamii yenye maadili tunahitaji watoto waliolelewa kwa upendo.
Usiambiwe tu nakupenda basi ukajiachia na mimba juu. Na kama umeamua kuzaa kwaajili yake , swali la kujiuliza, je, ana Utayari wa kuhudumia?, Kama ukiona ana Utayari wa kuhudumia hapo angalau maana hata ikitokea kutengana hawezi telekeza damu yake.
Yangu ni hayo, nimeona tukumbushane hili.