Usichokijua kuhusu riba (Interest Rate)

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Posts
1,382
Reaction score
513
Mfumo wa Riba umekuwepo kwa miongo kadhaa sasa, mfumo huu ukiashiria kukamilisha kile kisemwacho kua mwenye nacho ataongezewa na asiye nacho, hata kile kidogo alicho nacho kitakwapuliwa.

Riba kama tozo inauhusiano wa jinsi inavyolipwa na kutozwa, Kwa mfano tozo ya riba kwa siku ni tofauti na tozo ya riba kwa mwezi, au mwaka. Tozo ya siku hua kubwa kuliko ya mwezi au mwaka.

Riba hubadillika kutokana na mifumuko ya bei (Inflationary pressure),
Msukumo huu hutokana na fedha ya kigeni kua na nguvu, hii hupelekea taasisi za kifedha kuweka ukomo unaojulikana kama Prime Rate, ukomo huu unapokua juu sana, uwazi kati ya mkopaji na mkopeshaji hua mkubwa.

Ni nini gharama halisi ya Riba inayotozwa kwa mkopaji?
Wengi wa wakopaji hawako makini kuhusu kiwango cha riba inayotozwa, na hatimae kupelekea kulipa zaidi ya kile walichokusudiwa, kwa mfano 5% au 10% kwa lugha ya kitaalam (technical language) yaweza kuwa 0.05 au 0.1 hii yaweza kuonekana ni ndogo sana machoni pa mkopaji ila kwa mwaka 0.1 ya mkopo wa kiasi cha Sh Mil 10 ni Mil 1, huu ni mzigo tayari kwa mkopaji. Cha muhimu na kinachohitaji umakini ni marejesho na muda wa uliowekwa, hapa ndipo mtego ulipo. Kumbuka jinsi muda unavyokua mrefu wa kulipa mkopo ndivyo gharama za mkopo zinavyokwenda juu.

Kua makini unapohitaji kuchukua hatua ya mkopo, ikibidi waone washauri na wataalam kwanza.

Nawasilisha..!
 
kwel we gazka mendieta mtoa mada anadadavua interest rates we unatupia yanga-ngassa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…