Usiende nao nusu nusu

Usiende nao nusu nusu

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
đź“–MHADHARA WA 28:
SHERIA 1: Mponde kabisa adui yako
Hii ni SHERIA YA 15 kati ya zile SHERIA 48 zilizoandikwa na ROBERT GREENE katika kitabu chake cha "THE 48 LAWS OF POWER"

Mapitio:

Waponde adui zako kisawa sawa, usiende nao nusu nusu wala kuwapa chaguo lolote. Kumbuka ukiacha hata makaa moja yakifuka hatimaye yatawaka.

Historia imejaa mifano ya viongozi waliowashinda adui zao lakini wakawaacha kwa sababu ya huruma. Adui kila mara walikusanya nguvu zao wakizidi kuchukizwa na kuamua hadi walipokuwa na nguvu za kutosha za kulipiza kisasi.

Mara nyingi adui zako hawahisi chochote ila uadui kwako, na wanataka kukuondoa.

Njia pekee ya kuwa na usalama na amani ni kuwafanyia adui zako kile ambacho wangekufanyia wewe. Upatapo nguvu usisite kutoa pigo la mwisho, hii haimaanishi kuwaua lakini angalau kuwatenganisha kwa kuondoa kabisa uwezo wao wa kupigana.

~ Nikuletee mapitio ya sheria ya ngapi katika kitabu hiki?

Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 2, 2024
 
Back
Top Bottom