Uchaguzi 2020 Usijidanganye kutoa rushwa, unapotea na unapoteza pesa yako

Uchaguzi 2020 Usijidanganye kutoa rushwa, unapotea na unapoteza pesa yako

SUGABOY

Member
Joined
Sep 27, 2010
Posts
13
Reaction score
14
MCHAKATO WA UCHAGUZI MAJIMBONI 2020

HATUA YA KWANZA

-Kuchukua fomu (Kimyakimya bila mbwembwe)
-Kujaza Fomu
-Kurudisha fomu
-Kujadiliwa na kamati ya siasa wilaya (Wanatoa maoni kwa kila Mgombea, kama wagombea wako 10 au 3 au 7 wote wanatolewa maoni)
-Maoni hayo kwa Majina ya wote waliochukua fomu yanapelekwa Kamati ya siasa Mkoa kujadiliwa.

HATUA YA PILI

-Kamati ya siasa Mkoa inajadili majina ya watia nia wote toka Wilayani/Majimbo.
-Kamati ya siasa Mkoa inatoa maoni kwa kila mtia nia.
-Kamati ya siasa Mkoa inapeleka Majina Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

HATUA YA TATU

-Halmashauri Kuu/Kamati Kuu kujadili majina ya watia nia toka wilayani.
-Halmashauri Kuu/Kamati kuu kuchuja majina ya wagombea(Kama walikuwa 3,10 au 7) wanachuja na kubaki majina 3.
-Majina matatu yanafungwa kwenye bahasha ya SIRI na kurudishwa wilayani/Jimboni.
-Kwenye Mkutano Mkuu wa wilaya/Jimbo ambao huwa unakuwa na wajumbe kati ya 800 hadi 900.Majina matatu yatasomwa hapo.
-Kumbuka wakati Majina yanasomwa, watia nia wote wanapaswa kuwepo ili wasikilize kama wameteuliwa au wamekatwa.
-Mkutano Mkuu wa Wilaya utapiga kura kwa Majina hayo 3 yaliyosomwa, kisha matokeo yanatangazwa(Mchakato hauuishi hapo)

HATUA YA NNE
-Matokeo ya majina matatu kama yalivyopigiwa kura yanapelekwa KAMATI KUU ya CCM TAIFA.
-KAMATI Kuu ya CCM Taifa itatangaza jina moja kati ya yale matatu.

-Jina hilo linapelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwaajili ya taratibu za Uchaguzi Mkuu.

CCM MPYA 2020
 
Na mwenyekiti Taifa wa CCM nimemsikia kuwa atakayetaka kugombea Ubunge ni lazima ajitathimini sawa sawa kama anazo sifa nzuri kuliko wengine.Mwaka huu Ubunge wa Mtandao hautokuwapo.Hongera sana JPM kukirudisha chama kwenye misingi yake.
 
Mheshimiwa sugarboy,hata Kama kwenye wilaya au Jimbo Mimi mtia Nia h nimepata kura 300 na y amepata 30 na z kapata 4 kamatia kuu unaweza nikata akateuliwa aliepata 4 kugombea?
 
Kwa mwenye dhamira ya uongozi kuwatumikia watu hana sababu kulalamikia demokrasia kukandamizwa..vyovyote vile uongozi mtu hupewa na Mola kama tu wagombea wote watakuwa kwenye uwanja sawa usiompendelea mtu.
Kwa utaratibu huu Tanzania sasa itapata viongozi wenye nia na dhamira ya dhati kutumikia watu..milango na mianya ya rushwa, ushabiki na ubabaishaji kwa kiwango kikubwa haina nafasi tena..imezibwa! hiyo ndio ilikuwa inaleta viongozi wabovu kila mahali..Mungu ni mwema Tanzania sasa itapiga hatua.
 
Mheshimiwa sugarboy,hata Kama kwenye wilaya au Jimbo Mimi mtia Nia h nimepata kura 300 na y amepata 30 na z kapata 4 kamatia kuu unaweza nikata akateuliwa aliepata 4 kugombea?
Ndio.... Ndio maana baada ya kupigiwa kura majina yanarudi cc ilikuangalia kama kulikuwa na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa utaratibu kwa aliyeshinda.
 
Kishimbe wa Kishimbe,
Una uhuru kutafsiri vyovyote unavyoona inafaa kwako, lakini swali lilikuwa mfumo wa uchaguzi ndani ya CCM ulikuwa mzuri? Ni kweli mfumo ulikuwa unakipa chama candidates wazuri wenye sifa za uongozi? Kwa anayeijua nchi hii na hususan wakati wa uchaguzi ukifika jibu ni HAPANA mfumo uliokuwepo ulikuwa mbovu!! na zaidi ulikidhoofisha chama..ilipaswa ubadilishwe kukinusuru chama na nchi kwa ujumla..haukuwa uchaguzi ilikuwa ni GULIO la Kura!
Maana ya Demokrasia inapatikana kwa kutizama mambo kadhaa..historia ya nchi husika, mila na desturi, msingi wa sheria zilizopo nk..kwa utaratibu huu hakuna aina yoyote kukandamiza demokrasia kulingana na mifumo na maisha yetu watanzania.
 
Hapo rushwa itapigwa sana tu, wale wajumbe watakaopiga kura watajazwa mapesa vibaya.Tatizo LA ccm hats viongozi wao sio waadilifu.Wilaya nyingi wenyeviti Wa ccm wengi wana wagombea wao mifukoni tayari.wako wanaccm wanalalamika kwamba takukuru inawakamata wasio Wa Jpm tu.Mfano kule Mbeya tulia alianza kampeni kitambo sana wala hajakamatwa na takukuru wala kuhojiwa.
 
Kwa mwenye dhamira ya uongozi kuwatumikia watu hana sababu kulalamikia demokrasia kukandamizwa..vyovyote vile uongozi mtu hupewa na Mola kama tu wagombea wote watakuwa kwenye uwanja sawa usiompendelea mtu.
Kwa utaratibu huu Tanzania sasa itapata viongozi wenye nia na dhamira ya dhati kutumikia watu..milango na mianya ya rushwa, ushabiki na ubabaishaji kwa kiwango kikubwa haina nafasi tena..imezibwa! hiyo ndio ilikuwa inaleta viongozi wabovu kila mahali..Mungu ni mwema Tanzania sasa itapiga hatua.
Pole sana Mkuu, subiri mchakato uanze...sioni namna ccm itaondokana na rushwa kwa uchaguzi Wa Mwaka huu.muda utasema
 
Back
Top Bottom