figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Habari yenu wakuu,
Nmependa nitumie jukwaa hili kutoa angalizo moja ambalo nina ushuhuda nalo.
Mara nyingi watu hupenda kwenda Sokoni kununua Matunda kwaajili ya kutengeneza Juice majumbani kwao. Na ukifika pale Sokoni swali utakalokutana nalo ni:
Unataka matunda ya juice au ya kula Kawaida?
Hili swali wengi huwa wanajichanganya. Wanasema nipe matunda ya juice.
Ukifika nyumbani wakati wa kutengeneza ndo unaipatapata. Sababu matunda yote yaloharibika ndo utawekewa. Siku nmenunua matunda pale Buguruni nliipatapata. Sirudii tena.
Hivyo basi usithubutu kukutwa unaagiza matunda ya juice.
Mwenzenu nmetubu