Mwakawasila
Member
- Oct 23, 2024
- 23
- 20
HATIFUNGANI/BOND/AMANA
Ni aina ya dhamana inayotolewa na serikali au kampuni kwa lengo la kukopa fedha. Mkopaji anaweza kuwa serikali au kampuni na anaekopesha ni mwekezaji.
Mwekezaji anaponunua hatifungani, anaikopesha serikali au kampuni fedha yake kwa kipindi flani cha makubaliano.
Serikali au kampuni humlipa mwekezaji riba (isiyobadilika) kila mwaka kwa kipindi chote cha mkopo.
Baada ya kipindi kufika ukomo, mwekezajI hurudishiwa hela aliyowekeza mwanzoni.
Kuna hatifungani za aina mbili; Hatifungani za serikali na Hatifungani za makampuni.
ILA TUTAANGAZIA HATIFUNGANI ZA SERIKALI
FAIDA ZA HATIFUNGANI ZA SERIKALI
1. Uhakika wa Mapato: Hatifungani za serikali zinajulikana kwa kuwa na uhakika wa mapato.
Riba inayotolewa na hatifungani hizi ni kiasi ambacho hakibadiliki na kinajulikana hivyo inafanya hatifungani za serikali kuwa chaguo kwa wawekezaji wanaotafuta mapato ya uhakika.
2. Usalama: Hatifungani za serikali mara nyingi zinachukuliwa kuwa na kiwango cha chini cha hatari kuliko uwekezaji wa hisa au hatifungani za makampuni.
Hii ni kwa sababu serikali ni ngumu sana kutokulipa fedha kwa wawekezaji.
3. Hatifungani za serikali zinaweza kuuzika na ukarudishiwa fedha yako kabla ya kipindi Kuisha
4. Hatifungani za serikali zinaweza kutumika kama dhamana kuchukulia mkopo kwenye taasisi za kifedha kama benki.
Hatari za hatifungani za serikali*
1. Mwekezaji anaweza asirudishiwe riba au kiasi chake cha uwekezaji endapo serikali itashindwa kulipa mkopo huo.
Hatari hii huwa ni ndogo sana na hutokea kwa nadra sana hasa kwenye nchi zilizojaa malimbikizo makubwa sana ya madeni au uchumi kuyumba kwa kasi sana.
Kwa Tanzania, serikali haijawahi kutokuwalipa wawekezaji wa hatifungani za serikali hata mara moja.
Kwa hiyo usiwe na shaka
JINSI YA KUSHIRIKI KWENYE MNADA WA HATIFUNGANI ZA SERIKALI*
1.Fungua akaunti ya uwekezaji (BOT CDS ): Ili kufungua akaunti hii mwekezaji anatakiwa aambatanishe vitu vifuatavyo.
a. Picha 3 za passport
b. Copy ya TIN certificate
c. Copy ya kitambulisho cha taifa
2. Baada ya kuhakikisha viambatanisho vinavyohitajika, mwekezaji anatakiwa Kujaza fomu ya kufungua akaunti ya uwekezaji.
3. Akaunti ikiwa imeshafunguliwa hatua inayofata, mwekezaji anabaini aina ya hatifungani anayotaka (miaka 2, 5, 7,10,15,20 na 25)
pamoja na tarehe ya mnada wa hatifungani iliyochaguliwa kupitia kalenda inayopatikana kwenye tovuti ya Benki kuu ya Tanzania (BOT)
4. Mwekezaji anatakiwa Kujaza bid application form ambayo ataiwasilisha ofisini Kwa wakala aliyemchagua kwenye soko la hisa na kusubiria matokeo ya mnada huo
5. Matokeo hutolewa jioni ya siku ya mnada ambayo hutokana na bei ambayo mwekezaji amejaza kwenye form.
Mwekezaji anapaswa kufanya malipo siku ya kazi inayofuata. Ambayo malipo hayo hufanywa kupitia benki anayotumia muwekezaji.
6. Kiwango cha chini cha kuwekeza ni TZS millioni 1.
*Ikiwa unataka kuuza hatifungani ulionunua kabla haijafika ukomo wake(maturity), wasiliana WAKALA uliye mchagua kwa msaada Zaidi.
Mfano wa jinsi unavyoweza kupata FAIDA
Mfano wa milioni arobaini 40,000,000
Ukiwekeza ambayo utapata interest ya 15%
Tupate asilimia 15% ya 40,000,000
40,000,000÷100=400,000 ni laki nne
Zidisha Kwa 15×400,000=6,000,000 milioni 6 Kwa mwaka
Hiyo milioni 6 zidisha mara miaka 20
6,000,000×20=120,000,000 milioni mia moja ishirini
Hiyo ni faida unakuwa umezalisha Kwa miaka 20 Kwa mtaji wa milioni 40
Siku Miaka 20 ikiisha unapewa milioni 40 yako kama ilivyo
Ukipata Hela kubwa usifanyie matumizi wekeza alafu tumia
Hizo uliyowekeza kama amana ya kukopea mkopo
Kwa hiyo faida ndo inalipa deni lako
Kwa masomo zaidi unaweza I save no yangu
(255744980339) Whatsap and normal