NGOSHA13
Member
- Aug 30, 2024
- 7
- 7
Miaka kadhaa iliyopita nilifanikiwa kusoma Elimu ya sekondari lakini nilivyomaliza sikubahatika kufaulu kujiunga na kidato cha tano kwani nilipata daraja la 4, hivyo nilikua sina tumaini lolote na nkaona mimi na mambo ya kusoma ndio hivyo basi tena, ikabidi nijiunge na chuo kilichopo chini ya VETA hapo nilipata mafunzo ya uhasibu na kuingoza watalii kwa ngazi ya cheti.
Nilivyomaliza nilikaa mtaani na kwan kupata ajira ilikua ni ngumu sana. Siku moja baada ya miaka mitatu kupita rafiki yangu mmoja ambaye pia nilikua nikisoma nae pale kwenye chuo kilichokua chini ya VETA alinitafuta na kunipa wazo la kujiandikisha kwa ajiri ya kurudia mtihani. Nililipokea kwa furaha sana na nkaona kumbe bado nna nafasi ya kusoma tena na hiyo siku ndio ilikua siku ya mwisho kujiandikisha.
Basi, tukajiandaa pamoja kwenda kutafuta vituo kwa ajilli ya kurudia mitihani bahati nzuri tukapata na tukajiandikisha vyema kabisa. Sasa kazi ikawa kuanza kujiandaa vyema kwa ajili ya kurudia mitihani mimi nilijiandikisha kurudia masomo manne na mwenzangu pamoja na mdada mmoja ambaye alikua ndiye alompa huyo rafiki yangu wazo la kurudia mitihani, basi tukaanza kujisomea bila kufundishwa na mwalimu yeyote yule kwan tulinunua vitabu vya masomo husika na kuanza kujisomea kila siku kwani tulikua hatuna sehemu ya kujisomea zaidi ya kwenda Library ya mkoa wa Mwanza pale tukajiandikisha na kuwa wananchama.
- Usikate tamaa, kuna siku bahati yako nawe itang'ara
Bila kuchoka tulijisomea kwa nguvu zote kasoro siku za ibaada tu, siku zikasogea mda wa mitihani ukakaribia nakumbuka mimi binafsi nilikua napewa sana moyo na mama yangu bila kujali kejeli za ndugu, marafiki pamoja na majirani ambao walijua kua nilikua nimefeli na hivyo narudia masomo yangu upya, kabla ya kwenda maktaba au Library kwa ajili ya kujisomea nilikua ni lazima niondoke nyumbani nikiwa nmemaliza kumsaidia mama yangu kazi zote katika mgahawa wake na nlikua nakunywa chai afu naondoka saa tatu asubuhi mpaka wanafunga Maktaba.
Ilifika muda mpaka tunaambiwa na wafanyakazi wa maktaba kua muda umeisha ndipo tunakusanya vitu vyetu tunaondoka tulijisomea bila kuchoka mpaka siku ya mitihani tukakumbushana tukutane mapema hata kama mtihani tulikua tunafanya mchana. Mungu alijaalia tulifanya mitihani vyema kabisa mpaka tukamaliza tukaanza kusubiria matokeo, matokeo yalivyotoka nakumbuka nilikua natafuta credit 2 ila nilipata credit 4 [MUNGU NI MUWEZA]
Kuanzia siku hiyo toka nifaulu mitihani ile ya kurudia ilikua ni kama mwanzo mpya katika maisha yangu ya Elimu kwa mara ya pili kwani sikuwahi kuruhusu kufeli tena mtihani wowote ule niliokutana nao mbele yangu katika levels nyingine za elimu kwani niliweza kuendelea na masomo ya Advance kwa mchepuo wa sanaa [HGL] Na Mungu alinipa kibali cha kufanya vyema mitihani yote niliokutana nayo mbele yangu na nikawa daraja kwa wengine kwa kuwafundisha kupitia discussion mara baada ya kutoka shule na siku za weekend.
Kufanya vyema katika masomo yangi nilivyokua Advance kulinifanya nijulikane shule nzima na kwa waalimu walinipenda sana na waliniaminisha kua naweza kufanya vyema zaidi. Mungu alijaalia nikafanya vyema katika mitihani yangu ya Advance ndani ya shule na NECTA pia nilipata daraja la 2 na ukawa mwanzo mpya kwangu kwani niliweza kujiunga na elimu ya juu [CHUO KIKUU] nikiwa mwenye furaha zaidi kwani Mungu alinitendea mambo makuu sana na hakuniacha kamwe kwani aliniwezesha kusoma kozi yangu ya ELIMU kwa miaka mitatu bila kupata supplimentary katika somo lolote lile mpaka namaliza masomo yangu kwani nimefanyika mbaraka kwa familia yangu na nmewagusa wengi waliodhania siwezi kufanikiwa tena kwa kupitia elimu.
Kisa hiki ni cha kweli na kimenitokea maishani mwangu daima siwezi katishwa tamaa tena na mtu yeyote yule kwani kila mtu ana uwezo mkubwa sana ndani yake aliopewa na MUNGU.