Usikate tamaa, kuna siku bahati yako nawe itang'ara

The622

Member
Joined
Mar 5, 2023
Posts
55
Reaction score
111
Mambo wakuu,

Tunafanikiwa kwa kuhangaika kila moja ajuavyo katika Maisha yetu.

Kuna wakati unahisi kukata tamaa na kujiona si mtu mbele ya watu, ila nikwambie Ndugu yangu, Mungu hana choyo wala kukusahau, bali ni suala tu la muda.

Tumia ulichonacho kufika utakapo.

Una cheti Cha form four, Usione huna lolote unaeza fanya kupitia cheti chako, Kuna ajira mtaani zinahtaji utayari wa mwili wako na akili tu ili uajiriwe jumlisha na elimu uliyoipata darasani.

Jiambie unaweza, jione nawe ni mtu miongoni mwa watu Dunia hii,amka Kila siku na nenda kapambane kupata pa kujishkiza.

Kuna siku iso na jina wala tarehe Ile bahati yako nawe itang'ara.
 
Ahsante kwa encouragement mkuu...
kukumbusha tu Yosefu alipitia changamoto nyingi kwa miaka 13 kabla mambo yamuendee sawa.
So tujitume ila tuwe na subira.
 
Kuna Hope halafu kuna False hope.

Hapa umakini unahitajika.. kuna mambo ambayo inabidi tu ukate tamaa u move on.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…