Usiku Jiji la Dar es salaam ni full enjoyment and comfortability

Usiku Jiji la Dar es salaam ni full enjoyment and comfortability

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Mchana Dar es salaam ni mateso juakali na msongomano wa watu sehemu za masoko na vituo vya daladala eg Kariakoo, karume, Ilala boma, Manzese etc unapotembea lazima mgusane gusane na kupigana vikumbo na watu na wakati huohuo usumbufu wa bodaboda, bajaji, na magari.

Mchana hewa inakuwa nzito harufu za vinywa, jasho, ushuzi, mimoshi ya magari ongezea kelele za singeli kwenye bodaboda kelele za matusi na honi Kuna madereva hawana uvumilivu kitu kidogo kashapiga honi yaani kimsingi mchana Dar es salaam hakuna ustaarabu.

Ustaarabu Dar es salaam unaanza saa nne usiku ambapo utapita mtaani comfortable hata kama upo kwenye gari foleni zinakuwa zimepungua kama sio kuisha kabisa.

Zile harufu mbaya zinakata hewa inakuwa safi kaubaridi kwa mbali ambako kanakuwezesha kupiga zako t-shirt na pensi ukafeel the moment.

Kwenye starehe usiku ndio balaa lingine sehemu Kama Sinza most of the time usiku nikikosa usingizi basi nitaenda kupotezea muda ukanda wa Sinza.

At night Dar es salaam is Best.
 
Bila picha ni sawa na miziki ya singeli au taarabu za uswahilini.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Ukiwa kama mjasiriamali makini unaweza Badili masaa ya kazi na ukaufaidi usiku ulio mwema na tulivu sana!
 
Back
Top Bottom