Usiku mwema mpenzi wangu

Usiku mwema mpenzi wangu

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Posts
4,201
Reaction score
236
USIKU MWEMA MPENZI WANGU

Mpenzi

Habari za siku nzima ya leo ? Nafikiri siku nzima ya leo kwako ilikuwa salama na poa au sio ? kama ilikuwa nzima na poa hiyo ni furaha yangu kuu , nitapata faraja ya ziada ukinieleza kuhusu siku yako ilivyokuwa njema leo au sio mpenzi .

Mimi siku yangu ilikuwa poa sana , sema tu asubuhi ilikuwa baridi sana nikaogopa hata kuamka kila mara nilikuwa nakumbuka joto lako la asubuhi , nilitamani nisiwe naamka kama ungekwepo ningeendelea kulala juu ya mapaja yako au hizo tits zako ningekuwa na siku njema zaidi kama ingekuwa kweli .

Mpenzi leo nilienda kuangalia afya yangu , unajua sijaenda kuangalia afya yangu kwa kipindi cha miezi 3 iliyopita na nimekuwa na safari za mara kwa mara kwahiyo nikaona nikaangalie afya yangu , sijui wewe huko huwa unaangalia afya yako kila baada ya muda gani naomba unijulishe kama kama una mpango wa kwenda kuangalia siku chache zijazo nijulishe ili nikusindikize au unaonaje mpenzi ?

Baby watu wengi hawapendi kuangalia afya zao mpaka aanze kuumwa au kujisikia vibaya hiyo ni mbaya sana bora uchukue tahadhari mapema halafu wengi hao hao wanaamini kwenda kuangalia afya zao ni suala ya ukimwi pekee , na kwenye kupima ukimwi wengi hawataki mwa maana eti wanaweza kuambiwa sio waaminifu au mmoja wa mpenzi anaweza kuuliza kama unamwamini au la .

Kwa kuogopa haya maswali na mengine basi wanaona bora wasipime waendelee hivyo hivyo tu , lakini fikiria kijana wa kawaida anatembelea na vijana wenzake wangapi kwa mwaka ? ni wengi si ndio kwahiyo kupima ni lazima , hata hivyo ukimwi hauambukizwi kwa ngono tu kuna njia mbali mbali zinazoweza kuambukiza .

Naomba niishie hapa mpenzi ntazidi kukuandikia tena , pamoja na kukupigia simu za kukupa moyo na salamu moto moto

Nakupenda sana - NATAMANI TUPANDE JUU YA MLIMA KILIMANJARO NIKUBUSU AFRIKA NZIMA IJUE NAKUPENDA
 
khaaaaa, wewe mbona hakujibu hizi barua unazoandika??
 
Back
Top Bottom