Usiku wa Ulaya leo!!

Kimatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
286
Reaction score
271
Natumai wadau kila mmoja wenu ni mzima wa afya na poleni kwa Shughuli za leo katika kulijenga taifa katika kutamatisha siku kama ya leo kuna kitu kimoja unachoweza kufanya kama mdau wa soka ili kupunguza uchovu na kusahau maswahibu yaliyokukuta kutwa ya leo.Kama kichwa kinavyojieleza twende moja kwa moja kwenye mada;

Mechi za leo katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu ni Lyon vs Juventus na Real Madrid vs Man City.

Kwa mtazamo wangu Juventus wakiwa ugenini watachagizwa na uwezo wa Ronaldo kupata ushindi lakini pia Lyon wakiwa na Depay sio wa kubeza kwani wamekua moto sana sio tu msimu huu bali hata misimu kadhaa iliyopita, mechi hii naitazama kuwa na mvuto na magoli hasa endapo Juve watamuanzisha kipa wao mkongwe, Button ambaye akili yake inafanya kazi zaidi ya gloves zake kwa sasa. Ikumbukwe kwamba Ronaldo akifika hatua ya mtoano anakuwa mnyama, hata hivyo Lyon sio wa kubeza nguvu ya mashabiki wao itawapa sana hamasa wachezaji wao, Juventus pia hawako vizuri sana msimu huu, halitakuwa jambo la kushangaza kama Lyon wakiwaduwaza Juve, mechi za UEFA hasa hatua hii hutoa matokeo yasiyotegemewa kabisa.
HINT: wazee wa mikeka, Ronaldo anytime goalscorer ✅


Game nyingine ni Real Madrid wakiwa nyumbani kuwakaribisha Man City ambao wana hatihati ya kutoshiriki mashindano haya kwa misimu miwili ijayo kutokana na adhabu waliyopewa na UEFA!!
Mechi hii inaweza kuwashangaza wengi kwa kutokutoa magoli mengi kama inavyotegemewa kutokana na mwenendo wa timu zote mbili kutokua wa kueleweka, (ikumbukwe Madrid walipoteza mechi yao ya ligi kwa kipigo cha bao moja kwa nunge kutoka kwa Levante, Man City walichomoza kwa ushindi wa taabu wa bao moja dhidi ya Leiceter City).
Timu zote mbili zitacheza kwa tahadhari sana hasa zikizingatia umuhimu wa mechi zao zijazo, Madrid itacheza na Barca jumapili, siku hiyohiyo Man City wakikipiga na Aston Villa kwenye fainali ya Carabao.

Timu tatu kati ya nne kutoka England zimepoteza mechi zao za kwanza kwenye hatua hii ya kumi na sita bora 🤔 hii inaweza kuwa habari mbaya kwa Man City, kwa timu za Spain Atletico ilishinda nyumbani huku Barca wakilazimishwa sare ugenini! habari inayoweza isiwe mbaya sana kwa Madrid.

Eneo la kiungo litaamua zaidi mechi hii, umahiri wa makipa pia utachagiza matokeo kwa timu husika, rekodi zinawabeba Madrid wakifika hatua ya mtoano wanakuwa habari nyingine, Nategemea Madrid kushinda lakini sio zaidi ya magoli matatu.

Vipi mdau, utabiri wako ukoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…