Usikute Mayele anafanya kusudi Ili Kuwaaminisha Wachezaji wa Kibongo kuwa nao Wanaweza

Usikute Mayele anafanya kusudi Ili Kuwaaminisha Wachezaji wa Kibongo kuwa nao Wanaweza

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Habarini wana jamvi nimetumia siku nzima ya leo kutazama game zote 4 za Yanga SC zilizopita ili nipate kufahamu jambo lililo nje ya macho yetu mawili.

Kwa uwezo wa Mkongomani huyu Fiston Kalala Mayele wa kupachika mabao pasi na ku-struggle alikuwa sio wa kukukosa kwenye clear chances.

Kuna namna katika baadhi ya mechi anaonekana dhahiri kuwa ana muda na wakati wake wa kufunga bao. Yaani ni kama amajiamulia tu.

Hivi hatushtuki kwanini tangu George Mpole amfikie kwa idadi ya magoli, Mayele amekuwa kama ni mshindani anayefanya kazi ya kusawazisha tu idadi ya mabao ili gawe sawa!!!

Yaani George Mpole hajapewa nafasi ya kukaa kilele kwa zaidi hata ya wiki 2.

Yaani leo akimpiku kwa tofauti ya bao moja basi game inayofuata lazima Mayele achomoe. Yaani umekuwa kama mchezo hivi.

Inachoonekana ni kwamba Mayele ametambua wazi kuwa watanzania wana tatizo kubwa sana la kuwa na washambuliaji maridadi.

Hivyo anatumia mwanya wa mbio za ufungaji bora kama eneo pekee la kuwapa imani kuwa hata washambuliaji wa kibongo wana uwezo wa kushindana nae na siku moja waka mshinda.

Mayele sasa hivi hafungi kama hapo awali kuisaidia timu bali anafunga ili kumpa nafasi anayemfuata kuwa na matumaini na hamasa ya kushindana naye.

Imagine George Mpole angezungumziwaje na wapenda soka endapo Mayele angekuwa amempita kwa tofauti ya mabao 6?

Tunayo sababu ya kila mmoja wetu bila kujali Ushabiki wa timu zetu KUMSHUKURU Mayele. Maana mpaka akija kuondoka atakuwa amewagundisha mengi washambuliaji wetu.

Asante MAYELE. Kalala Fiston.
 
IMG_20220523_183206.jpg
 
Back
Top Bottom