Usilazimishe penzi hata kama umependa

Anold

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2010
Posts
1,456
Reaction score
615
1. Ukipenda sipopendwa, adhabu wajitakia,
Moyo utapondwapondwa, maradhi wajitakia,
Utachekwa na watawa, aibu itatukia,
Usilazimishe penzi, hata kama umependa.

2. Usilazimishe kupenda, majuto yatakujia,
Mtima utakupinda, ubovu utaingia,
Wajuzi watakuwinda, wakubeze kwenye njia
Usilazimishe penzi, hata kama umependa.

3. Mpende mwenye kupenda, mwache asiyekupenda,
Usishindane mshinda, dhalili itakudenda,
Ghadhabu itakuwinda, kama kamanda wa kanda,
Usilazimishe penzi, hata kama umependa.

4. Meseji utazituma, vocha nazo hupeleka,
Utabaki uyatima, faida hutaidaka,
Utaingia gharama, ukose hata nafaka,
Usilazimishe penzi, hata kama umependa.

5. Mtaani utabezwa, vijiweni utangazwe,
Hutakosa kubatizwa, buzi jina utawazwe,
Wataikosa na dawa, ili japo utulizwe,
Usilazimishe penzi, hata kama umependa.

Nimeandika shairi hili kuwaonya wale wanaolazimisha kupenda/kupendwa kwani majuto, kuvunjwa moyo, kukatishwa tama na hata kudhalilishwa na kupotezewa muda na pesa ni sehemu ya adha wanazokumbana nazo siku hadi siku. Lazima ujenge utaratibu wa kutathmini mahusiano yako na mpenzi wako kama yana ufanisi na faida kwako.
 
Anold ongeza size bana nimeshindwa kusoma kabisa macho yangu mabovu
 
Umenigusa mkuu,
saingine ukipenda hata alama unashindwa kusoma vizuri.
Sasa unapotendwa mhhh!
 
Tumekusikia, tumekusoma, tumekukubali!!
 
imenigusa, hakika ukipenda usipopendwa, loh! Kaka nimekupata!!
 
Mkuu yalinikuta hayo niliteswa nikaliwa hela zangu mpaka kuja kushtka nilishafilisiwa vya kutosha ila malipo ni hapa hapa duniani n i kno god is there.bt stay in touch mkuu shairi fundishoni
 

Ni kweli mkuu. Huwezi kulazimisha maji yapande mlima. Hata ukitumia pump, siku ikiharibika yatafuata mkondo, nawe utabakia kulia 'maji yangu, maji yangu' wakati yatakuwa yanatumiwa na wengine kwenye bustani zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…