Ndio nakumbuka leo ni Ijumaa ile tunayoiita Ijumaa kuu yenye amri, Usile nyama siku ya Ijumaa kuu.
Just imagine ndio uko na mning'inio wa ziada 'hangover' na umeambiwa usile tu nyama siku zote kama ya leo Ijumaa kuu
C&P
Habari za leo wapendwa wangu katika Kristo.
Kuna kitu kinaitwa mapokeo katika madhehebu yetu. Madhehebu yetu huwa yana mapokeo. Sina maelezo mazuri sana kueleza nini maana ya mapokeo. Lakini kwa maelezo marahisi mapokeo ni taratibu za ibada na namna ya kuenenda katika kanisa. Mapokeo ni desturi za madhehebu. Kila dhehebu huwa lina desturi na taratibu zake. Taratibu hizi pamoja na imani ndizo zinazotofautisha madhehebu duniani.
Ndo maana kuna madhehebu mengine hawali baadhi ya vyakula si tu katika pasaka bali wakati wowote. Au hawanywi baadhi ya vinywaji fulani wakati wowote. Lakini si kwamba wale wanaokula vyakula hivyo watenda dhambi au hao wasiokula ni wadhaifu katika imani. La hasha. "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato....Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili" - Kol 3:16-20
Kwa hiyo wapendwa tusiwakwaze wale wasiokula au wale wanaokula nyama katika Ijumaa kuu ya sikukuu ya pasaka au siku iwayo yote.
Nami siko tayari ndugu yangu aingie huzuni kwa sababu ya chakula, nitakuwa nimeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula changu sitaki nimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake pale msalabani.
Kwa ajili ya chakula sitaki niiharibu kazi ya Mungu. Maana vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza. Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yangu hukwazwa. Ile imani niliyo nayo nafsini mwangu mbele za Mungu. Paulo asema "Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali. Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi" - Rum 14:22,23
Amani ya Kristo na iwe nawe