Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
USILETE MBWEMBWE KWENYE HARUSI, UTALIA.
Na, Robert Heriel
Leo Taikon sitakuwa na maneno mengi maana kuna wadau wangu hupenda ndizi kisukari, hupenda fupi fupi.
Haya, usilete mbwembwe kwenye Harusi tadhani wewe ndio mtu wa Kwanza kufanya Harusi, utalia.
Usilete mbwembwe kwenye Harusi ikiwa mahari ulitoa Kwa mbinde😜😜 Kama ulibargain na Wakwe usije ukaleta mbwembwe zako za kipuuzi.
Tutakuwa tunakuchora tuu Sisi Wakwe zako. Utalia baadaye.
Usilete mbwembwe kwenye Harusi ikiwa Harusi yenyewe umekamua watu na tumichango ya kushikana mashati. Utalia.
Usilete mbwembwe kwenye Harusi ikiwa Bibi Harusi uliyemuoa hujaikuta bikra. Ex za mke wako tunakudere tuu unavyoshongondoka. Utalia baadaye, utake usitake.
Usilete mbwembwe kwenye Harusi ikiwa unajua kabisa bila mundende ganzi mujarabu huwezi kumridhisha Bibi Harusi wetu. Utachapiwa, wewe jichekeleshe na suti yako.
Usilete mbwembwe kwenye Harusi ikiwa unajua kabisa huna maajabu ya viuno feni, mwanamke hujafundwa ukafundika hujui A wala Ba za chinua Achebe kwenye sebene la seremala. Utaletewa mke mdogo.
Usilete mbwembwe kwenye Harusi wakati Harusi yenyewe imefungwa Kwa mbinde, mtu mpaka umegombana na rafiki kisa kukuchangia.
Usilete mbwembwe kwenye Harusi ikiwa unajijua Una Mkono wa birika, hujui kumhudumia Mkeo. Wadhamini waliokudhamini Harusi yako ndio hao hao watakaokusaidia majukumu ya ndoa.
Ukifika kwenye ukumbi wa sherehe ya Harusi yako.
Cheza Kwa staha, usiruke ruke Kama njeree ya makaa, Kama ni Bibi Harusi cheza Kwa maringo ya staha, macho yako yawe ya aibu muda mwingi yawe chini sio ung'aze macho huku na huko Kama Askari anayetafuta washukiwa wa dawa za kulevya.
Kama ni Bwana Harusi, cheza ki-gentlemeni. Usirushe rushe miguu, wala usikate mauno Kama mwehu.
Usilete mbwembwe, utagongewa, ulie Kama Mbuzi meee baadaye.
Muda wa kula, Kula Kwa adabu, usichote lisahani likajaa machakula mengi Kama mlafi. Kula chakula huku ukitafakari michango ya wote waliokuja ukumbini. Tafuna huku ukisema; mchango! Mchango! Mchango! Kimoyo moyo.
Sio unatafuna Kwa sifa mbele ya watoa michango, watu wanakudere, wanasubiri sherehe iishe.
Harusi haihitaji mbwembwe, Harusi inahitaji utulivu, burudani zenye staha.
Sio upigie watu kelele na mbwembwe zisizo na maana, nakuhakikishia kadiri unavyoleta mbwembwe ndivyo utakavyolia Kama Mbuzi.
Anyway nilisema sitaandika pakubwa. Niishie hapa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro