SoC01 Usilewe Likes na Comments: Simulizi inayoweza kubadili maisha yako kwa zaidi

SoC01 Usilewe Likes na Comments: Simulizi inayoweza kubadili maisha yako kwa zaidi

Stories of Change - 2021 Competition

Lackson Tungaraza

New Member
Joined
Dec 3, 2015
Posts
3
Reaction score
1
SIMULIZI INAYOWEZA KUBADILI MAISHA YAKO KWA ZAIDI YA 79%

▪"Kwa Kweli Mwenyezi Mungu hakukosea Kabisa Kuniumba. Tazama Uso Wangu unavyong'ara, Ngozi Nyororo, Jicho Zuri kuliko la Ray C, Kila Nguo inanikubali hata nikivaa Gunia na Dekio, hakuna kama Mimi hapa Mtaani na Kule Mtandaoni, Mwonekano Wangu nao ni mzuri sana Kiasi cha Kuwavutia hata Waume za Watu na Vijana Mabachela huko Mitandaoni. Daaaah! Sisi ndio Sisi, Wengine Mafisi. Halafu hizi Nyusi Inabidi nizikate ziwe Kama za "Role Model" Wangu, Chuchu nazo nizikuze, Machoni niweke Kope zile Mpya za kutoka Ughaibuni, nivae Nguo za Kubana Makalio ili niwavutie Wapenzi Watazamaji na Marafiki zangu wa Mtandaoni, ikiwezekana niongeze na Uweupe Usoni Ili ning'ae zaidi kwenye Picha. Huku ndiko Kusikia la Mgambo, hahaahaa."

Hayo ni Maneno Yaliyokuwa Yanatoka Katika Kinywa cha Binti wa Pekee wa Mama Ujasi baada ya kufiwa na babaye takribani Miezi Mitatu iliyopita. Alikuwa akijiangalia kwenye Kioo kikubwa cha Sebuleni na "Ear Phones" Masikioni akisikiliza Wimbo wa Mwansasu "Ninatesa kwa Zamu." Na kwa namna alivyokuwa anasikiliza Wimbo kwa Sauti ya Juu hakujua Pia alikuwa anaongea kwa Sauti ya Juu sana Kiasi cha Kusikiwa na Mamaye aliyekuwa anapika Ugali wa Dona na Samaki, Jikoni. Mamaye akaamua Kwenda Kujua Ikiwa ni Sauti ya redio au ya mwanaye wa Pekee. Alipofika, alishangaa kumwona Binti Yake akiendelea Kupaka "Lipshine" Mdomoni na Kujisemesha Juu ya Uzuri wake.

MAMA: We Baby Unafanya nini hicho?

- Lakini Mwanaye hakumsikia kwa Sababu ya Sauti ya Juu sana ya Mziki Masikioni. Mama akaamua ampige Begani kwa Hasira, ndipo akageuka na Kutoa "Ear Phones" Masikioni.

BABY: Mama, mbona Unaniumiza Bega, bega lenyewe hili halina Spea nyingine nikiharibika.

MAMA: Jinga Wewe, Unafanya nini hapa kwenye Kioo Sahivi? Yaani, nahangaika Mwenyewe Jikoni!

BABY: Mama, nilikuwa natengeneza Uso Wangu. Unajua Uzuri Mtu anazaliwa nao Ila Urembo Unatengenezwa!

MAMA: Baba Yako angekuwa hai, leo angekupiga Fimbo za Kutosha na ngumi za Kila Rangi.

BABY: Kwani nimefanya nini?

MAMA; Muda Wote nilikuwa nakusikia kutoka Jikoni, Jinsi unavyojitapa kwa UZURI Wako, Kudatisha Watu Mitandaoni, Pamoja na Mipango Yako Ijayo ya Kurekebisha Mwonekano Wako.

BABY: [Kwa Mshangao] Kwani Wewe Umejuaje!

MAMA: Ulikuwa Unaongea kwa Sauti Kubwa sana, na "Ear Phones" zako Masikioni.

Mara BABY akaishiwa Mapozi na Kukaa kwenye Sofa kwa kuwa SIRI Yake ya Muda Mrefu sana Ilikuwa Imefichuka.

MAMA; Mwanangu, Naomba Unisikilize kwa Masikio Yako Yote Mawili kama ulivyokuwa Unasikiliza Wimbo Wako. Mimi ni mama Yako, ninapatwa na Uchungu sana moyoni mwangu ninapoona Unapotea. Hakuna Mwanadamu mwingine atakayekupenda kama Mimi, Wengine Wote ni Wapitaji tu lakini Mimi Niko Nawe papa hapa.

BABY akaanza Kulengwa na Machozi. Akainamisha Kichwa chake kwa Aibu.

MAMA: Mwanangu, Wewe Sio wa Kwanza kupata "LIKES" na "COMMENTS" huko Facebook na Mtandaoni, mamia na Maelfu ya Watu washakuja na Kupita. Ndivyo ambavyo Ulikuzwa na Marehemu babayo ?

BABY: Hapana Mama...

MAMA: Sasa Umetoa Wapi hiyo tabia! Kuwa makini sana Mwanangu, Dunia haina Huruma kama alivyoimba Bahati Bukuku. Wewe Leo ukipatwa na Ukimwi au Kuharibikiwa, Dunia haitaisha, Dunia itaendelea tu Kuwepo, na tena haitashangazwa kwa UJINGA Wako huo. Walikuwepo Wanamuziki MAARUFU kama Michael Jackson, aliyekuwa anaimba sana na kuwa MAARUFU pande zote za Dunia, lakini Dunia haikuisha kwa Sababu ya Kifo chake cha Kujitakia. "Umaarufu usiokuwa na tija kwenye Jamii Yako ni Uzuzu, kama Sio Upumbavu na Uharibifu."

BABY: mamaaaa....

MAMA: Ndio hivyo. Usipojifunza Kujitunza, hakuna atakayefanya kwa niaba Yako. Kabla ya Kufanya cho chote kile; Jiulize kina Manufaa gani Kwako kwa kuangalia Kesho Yako, Kina Manufaa gani kwa familia Yako Ijayo, na pia Kina Manufaa gani kwa Jamii Yako. Hukuzaliwa ili uishi kwa ajili Yako Mwenyewe, Bali kwa ajili ya Wengine Pia. Sidhani kama Ukifa Leo, Watu Wataongelea "Likes" na "Comments" ulizokuwa unapata Mitandaoni. Hayo Mambo hayatakuwepo Kwenye Risala Ya Marehemu. Ukitaka Kukumbukwa Vizuri basi Uwe Mfano mzuri wa Kuigwa kwenye Jamii. "BINTI wa karne hii ya sasa HAPASWI tena kuwa CHOMBO CHA STAREHE. Anapaswa Kuwa Mpindua Ulimwengu Kiroho, Kiuchumi na Kimahusiano."

BABY: Kwani ni nani alishaharibikiwa kwa Kufanya hivyo ?

MAMA: Bado tu hujaelewa! Unamkumbuka Yule Binti Kipanga aitwae Mariamu? Alikuwa Binti Mstaarabu sana ingawa hakuwa Mwarabu. Alikuzwa na Wazazi kwa Ulinzi wa hali ya Juu sana, alikuwa na Walinzi Kila alipokwenda, kwa lugha ya vijana wa Sasa wanasema "Alikuwa Geti Kali." Walichosahau ni kwamba MAARIFA yana Nguvu kuliko SILAHA. Alipomaliza kidato cha Sita, alipewa Simu Kali ya kisasa ambayo aliitumia kama Apendavyo Yeye. Walidhani wamemjenga vyema, Kumbe lilikuwa Bomu la kuwalipukia Wao wenyewe. Alipojiunga na mitandao ya kijamii, alianza Kuwafundisha VIJANA wenzake wa Kike Juu ya kutoyachochea na Kuyaamsha Mapenzi kabla ya Wakati. Siku zilivyozidi Kwenda, alipata Umaarufu Mtandaoni na kupendwa na Vijana wa jinsia zote mbili. Hakujua vita ya maarifa inapigwa kwa Maarifa yenye Nguvu kubwa zaidi, na Sio kwa Elimu tu ya Darasani na kwa kuangalia Filamu za Kinaijeria. "Likes" na "Comments" zikawa Uwanja wake wa Nyumbani. VIJANA wa Mjini wakaanza Kusifia MIDOMO Yake iliyo Mizuri kuliko ya Beyonce, MACHO Yake kuwa ya Kuvutia, SAUTI ya Kumtoa Mugabe madarakani na Nyoka Pangoni, Pamoja na UMBO lake lenye namba nane. Ghafla akaanza kutuma Picha nyingi kuliko Mafundisho, Ngozi ikaanza kupigwa Msasa utadhani Kitanda cha fundi Seremala, akaanza na Kubana Makalio na Nguo za Kuonesha Maumbile Yake. Unajua kilichofuata ?

BABY: Sijui.

MAMA: Tozi wa Mbagala alikuja akamtoa "Out" na kumpachika Mimba iliyoambatana na Adhabu ya Ukimwi. Tangu Wakati huo Alipoteza dira ya maisha Yake, akaishia Kujinyonga kama Yuda Iskariote kwa kuwa aliona amewaaibisha sana wazazi wake waliokuwa Mawaziri Wateule wa Rais Maximillian Saasita. Huo ndio ukawa mwisho wa Kipanga Mariamu.

BABY akapiga Magoti na Kumwomba Msamaha Mamaye kwa Machozi ya Kutambua Makosa Yake ya Kupenda "Likes na Comments" za Mitandaoni kuliko Kumpenda Mamaye na Mwenyezi Mungu aliyemwumba kwa Sura Yake na Mfano Wake. Na tangu Siku hiyo akatambua ya kwamba "Upendeleo hudanganya na UZURI ni Ubatili. Bali Mwanamke amchaye Mwenyezi Mungu ndiye wa Kusifiwa."

BABY na Mamaye wakapiga Magoti na kukumbatiana, wakainyanyua Mikono Yao na Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Hatua Mpya aliyowapatia kwenye Familia Yao. Nguvu za Mwenyezi Mungu zikawafunika, Kicheko cha Furaha Kikasikika Kati Yao Kiasi cha Shahidi Kuacha Kuandika na Kwenda Kujisomea Kitabu kipya cha MWANACHUO DIARY.

#NewLifeChapter
Fb.com/ltungaraza
📞0764-793105.
.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom