Usilipize baya kwa baya bali kwa jema

Usilipize baya kwa baya bali kwa jema

Mitchell

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
904
Reaction score
1,036
Mama mmoja mcha Mungu alikuwa na jirani yake mwenye roho mbaya kupita kiasi, siku
moja akafungulia mabata yake ili yakajitafutie chakula. Bahati mbaya yakaenda
kwa jirani yake, jirani kuyaona akayapiga mabata yote matano na kuyajeruhi
vibaya sana. Yakajikokota yakarudi nyumbani yakiwa hoi sana mama mcha Mungu
kuona vile akaona ni vema ayachinje ili yasije kufa. Basi baada ya kuyachinja
akayatengeneza, akayaweka kwenye friji kisha akachukua mabata mawili akayafunga
vizuri na kumpelekea jirani : Jirani haya mabata yamepigwa huko mtaani bila
huruma na yaliumia vibaya hivyo nimeona niyachinje ila yalikuwa mengi hivyo na
wewe chukua haya upate kitoweo jirani yangu.
 
Bila shaka aliyakataa kwa hofu kuwa anaweza akawa ameweka sumu.
 
Back
Top Bottom