SEHEMU YA KUMI NA SITA
Ilipoishia,,,,,,,,,,
Mara nikapigwa na kitu sjui ni nini, kuanzia hapo ndo sikujua nini kiliendea tena, nikawa nimefloot,
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,
Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nipo wodini, Nimelala kitandani nimetundikiwa drip, nimepigwa bandeji karibu kila mahali, Sa najiuliza nimefikaje fikaje pale ,Kumbu kumbu haziji kabisa, Naona tu manesi wanapita pita, watu wana pitapita,
Basi nesi mmoja akaja kwenye kitanda changu, akaangalia angalia ile drip, anataka kuondoka nikamuuliza, Nesi hapa ni wapi? Akasema pale ni Majengo hospital, Nimefikaje hapa? Akasema uliletwa hapa na polisi ukiwa na hali mbaya sana, basi akaondoka,
Sasa pale ndo kumbukumbu zikaanza kunijia, nikaanza kukumbuka matukio, Nikakumbuka wale vibaka, nikakumbuka nilivyokuwa napigwa, Daah machozi yakawa yananitoka, Nikakumbuka begi langu walichukua wale vibaka, mbaya zaidi lilikuwa na vyeti vyangu vyote kuanzia vya shule paka cheti cha kuzaliwa,
Ahhhah niliumia sana, nikasema sasa yote haya ni nini, kwanini yanitokee mimi, Basi nikamkumbuka Sity nikasema lait angekwepo angenisaidia, Nikakumbuka maneno ya Da J siku ile namwambia kwamba nataka kuondoka niende Arusha, alisema "Usiende huko Utakufa" Nikahisi Da J alifunuliwa yatakayokwenda kunikuta huko,
Basi nikakaa pale hospitali, kumbe polisi bado wananilinda, Wanakuja pale kitandani wananiangalia wanaondoka, Basi nikawa nasikia watu pale wodini wananong'onezana huku wananinyooshea kidole, Wanasema yule pale ni mwizi, Aliletwa hapa hafai ila saivi kapata nafuu, Moyoni nikawa naumia sana maana mi najua mi si mwizi, sema ndo hivyo nani ataniamini,
Basi badae nilikuja kufahamu kilichotokea siku ile, Kumbe wakati wanataka kunipiga kibiriti pale chini kumbe polisi wakatokea, Watu walivyoona polisi wakakimbia wakaniacha ndo ikawa ponea yangu, Kumbe kituo cha polisi cha majengo hakipo mbali na pale uwanjani kwaiyo polisi walipopata taarifa wakaja fasta, Basi nikatiwa kwenye gari yao wakanileta pale hospitali, kumbe hospitali yenyewe ilipo na pale uwanjani imetenganishwa na barabara tu,
Basi nilikaa sana pale hospitali, paka majeraha yakaanza kupona, polisi wapo tu na mimi hawaniachi, basi siku ya siku nikapewa ruhusa, basi polisi wakanichukua paka pale kituoni, Nikaandika maelezo pale badae wakanitia ndani kwenye kiselo chao pale kituoni , mzee baba maisha ya huko selo sitaki hata kuyasimulia,
Basi siku ya pili nikapandishwa mahakamani pale moshi mjini mahakama ya mwanzo, nikasomewa shitaka langu la kutaka kuiba kwa kutumia nguvu, Akaja askari mmoja wa kituo cha majengo kutoa ushahidi, akaelezea jinsi walivyopata taarifa, na jinsi walipofika pale wakanikuta napigwa, pia akasema dada ambaye nilitaka kumuibia pia walimpata na yeye akatoa maelezo yake,
Badae akaitwa dada aliyetaka kuibiwa na yeye atoe ushahidi, basi akapanda yule dada, akasema yeye alikuwa anakatiza pale uwanjani huku anaongea na simu, mara ghafla mimi nikatokea nikaanza kumkimbiza nataka kumnyang'anya simu, alipoona vile ndo ikabidi ajitetee kwa kukimbia na kupiga ukunga,
Basi na mimi nikaambiwa nijitetee na kama nina mashahidi pia nilete, Mi nikasema sina mashahidi nitajitetea mwenyewe, Basi nikaileza mahakama kila kitu, kuanzia nilipoenda pale shule, nilivyokimbizwa na wale vibaka, nilivyopigwa mpaka nilipojikuta hospitali,
Basi hakimu akasema kesi imeahirishwa mpaka kesho kwa ajili ya hukumu, kwa sasa nitaenda mahabusu ila milango ya dhamana ipo wazi, Nani sasa wa kuniwekea dhamana, ikabidi nipelekwe mahabusu gereza la Karanga lilopo pale moshi,
Mzee kwa mara ya kwanza natimba gerezani, wacha kabisa!! Siku hiyo sikulala kabisa, niliwaza mambo mengi sana, Nikakumbuka maneno ya Sity " Ebu jichunguze ni wapi ulipo mkosea Mungu", Nikakumbuka sana kijijini kwetu, Nikasema bora na mimi ningesepaga home kama Kidosho, Nikamkumbuka Happy na Mwanamgu Joyce, toka nimwone kwenye picha sijawahi kumwona tena, nikawaza saivi atakuwa mkubwa, sijui kama nitawaona tena,
Itaendelea