Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Hii stori niliifatilia yote mpaka ikaisha, nimeanza tena kuisoma naiona kama mpya vile
 
Kwa hapa nishaona unafurahidha genge
 
Sehemu hii ya mwisho hakika imenitoa Chozi....
 
Nabaki na wewe
 
Kwa wageni wa fasihi, suspense ni kileleni. Mtakumbuka tu, kileleni hakuishi hamu. Mi sijui ni maneno tu ya darasani. Wana KLF tulipotezwa
 
Hii story jaribu kuisummarize uimalize haraka ILI usiingie kwenye majaribu ya kusema uongo. Mfano Sity kufukuza basi n.k
Ni ushauri tu mkuu!
Kuna watu wanajua kupenda,hili la sity kufukuza gari ni dogo. Amini bure. Vipo viapo vya mapenzi kutoka kwa wadada nadhani hata paradizo uta-imagine kubaya kuliko kumkosa sity and the likes.

Kobwa wangu ni mmojawapo ijapokuwa nilipata kuiishi falsafa ya Achebe Chinua, 'a strong man never trust a woman'
 
Nimesoma title na sehem yakwanza nimegundua kichwa cha habari hakiendani na maelezo ....... labda ni some kama stori tu lakini hakuna uhalisia kabisa
Zama ndani mkuu kuna minofu ya kukujenga. Hata km ni fix lakini funzo ni kuwa dogo kaenda kutafuta bila baraka za wazazi/ndugu (hakuaga ili 'wazee' wafungue njia kwaajili yake. Hapa mshana jr PHD mjuvi wa mambo ya kiroho aweza kutia neno).

Pia ufukuaji wa miili ya wamama tofauti tofauti si kitu kizuri. Mingi ina mikosi na laana. Sio tu tunabadilishana nao 'sukari ya hisia' bali hadi kubadilishana nukusi, mabalaa ya magonjwa na roho za makataa. Yumkini nisimwasee wahanga. Mfanowe uzi huu.

Here we go!!
 
HUYU MTOA POST NIMEANZA KUPATA MASHAKA NAYE, UKITUMIA AKILI UTAGUNDUA AMEANZA UTEGEVU NA KUJIVUTA VUTA KAMA MPWAYUNGU.!

ANA KILA DALILI ZA KUTOMALIZA UZI HUU. YETU MACHO, NGOJA TUONE.

NB: NI MTAZAMO WANGU TU!
Msamehe leo yuko mahakamani majengo baada ya kupata dhamana[emoji23][emoji23] Kidding
 
Kama nakuelewa vile mkuu. Yaani pros & coins
 
Kwanza story ni ya uongo,miaka ya 80 Sikonge yote ilikuwa haina sekondari hata moja
Ufafanuzi
Kuzaliwa 80' kamaanisha
1980-198-1...9.
Chukulia kazaliwa 1988 mpe miaka ya utoto 7.
Akiwa na miaka 8 aanze s/msingi
Kwaio kaanza 1996
Je ni kweli 1997.....2000 hakukuwa na sekondari bado?

Njoo katikati ya story
Kasema pugu sekondari kwaajili ya kidato 5&6. Ingia maktaba kumnukumbu ya mabomu Mbagala na gongo la mboto miaka gani ndio utoe alianza form I meaka gani!?

Yumkini ulipendezwa tu kumtaja muongo.

Ngoja stupe raha, tunaumiza akili kusoma siasa. Ngoja tukineemeshe kwa hizi kashata
 
Chukua na pepsi kwa bill yangu
 
Mwanzoni katika makuzi yangu nilikuwa naambiwa watu wengi ni wachawi, sikuielewa kauli hii. Kumbe hata kuwa na roho mbaya tu ni uchawi pia.

Hajawaza jamaa katishirikisha life experience yake pasna malipo. Tena kwa utashi na kwa gharama ya bando. Linakuja jitu na roho ya sumu kumkosoa.

Hawawazi tamthiliya za tv zina mengi tunajifunza vikiwemo vitabu vya fasihi sekondari, hadithi za mababu na simulizi za visakale na rarihi. Je ni ya kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…