Johnkitime Blog
Member
- Mar 4, 2015
- 13
- 12
YAMEMKUTAjamaa yangu wa karibu sana, hana raha kabisaa. Ile methali ya kusema usilolijua halikusumbui, ndugu yangu kaigundua kuwa ni ya kweli. Mimi kwa kweli namuonea huruma. Naomba na wengine mtakayoisikia jifunzeni kutokupekua mambo yaliyopita, au kuuliza maswali magumu unaweza kupata majibu magumu. Sasa angalia jamaa yangu yuko hapa kwangu analia kakonda kwa muda wa nusu siku tu na hajui maisha yataendeleaje.
Jamaa yangu yuko vizuri sana kimaisha ukifika kwake uwe una uhakika utakaribishwa na juisi ya boksi, tena boksi unafungua mwenyewe unakunywa mpaka unamaliza peke yako.
Kwake kuna TV flat skrini kubwa ukutani, watoto wake utawakuta wamelala sebuleni kwenye zuria wakiwa na rimoti wanabadilisha chaneli, wengine wanachezea gemu huku wanazungumza kingleza utadhani wako Ulaya, wote wanasoma intaneshno, kasoro mmoja tu, mtoto wane. Huyu ndie alikuwa msalaba wa familia, ukisikia nunda basi ndie huyu, mtoto alikuwa mwizi, shule hataki, mchafu mchafu, hashindi nyumbani, kila siku kesi mara kapigana, mara kaiba kuku, kulikuwa na taarifa kuwa bangi pia anavuta. Hiyo ndio shida peke yake katika familia hii iliyokuwa na utulivu mkubwa.
Mke wa jamaa yangu ni mama mmoja mtulivu mkarimu halafu mzuri, yaani wakati wowote akiamua kucheza muvi zetu hizi atakuwa kivutio, shem kaumbika bwana.
Jamaa yangu kayataka mwenyewe, jana usiku alimtoa out mkewe wakaenda kula chakula cha jioni na mkewe kwenye hoteli moja kubwa wakasindikiza na mvinyo kisha wakaenda muziki, mambo yalikuwa raha sana, vijana wa kileo wanasema walikula bata kwa raha zao. Kwa furaha sana wakarudi kwao mapenzi yakiwa yamechangamshwa upya. Wakiwa wamepumzika ndipo jamaa yangu katika hali ambayo yeye mwenyewe hajui ilimtokeaje si akaanza kumuuliza mkewe, Mke wangu, niwe mkweli pamoja na kuwa kwa sasa tuna watoto sita mimi bado nakupenda sana. Na hakuna kitu kitakachoweza kunifanya niache kukupenda, I love you honey. Nina swali moja tu, huyu mtoto wa nne mbona yuko tofauti na hawa wenzie sita, mkorofi, hataki shule yaani tabu tupu? Mke wangu nambie tu kama ana baba tofauti na wenzie kiukweli halitabadili mapenzi yangu kwako. Ilikuwa kama vile yule mama kapigwa na shoti kwani kwa sekunde kadhaa alikuwa kama kaganda vile. Shemeji akamuuliza jamaa, Jamani mbona sikuelewi kwani umesikia nini? Kumbe kunitoa out ulikuwa una neno la siri moyoni, nasikitikika sana mume wangu. Jamaa yangu ikawa lazima ajitetee maana ilikuwa kama kuna ugomvi umetaka kuanza. Mke wangu usinielewe vibaya nilikuwa namuongelea huyu mtoto sikuongelei wewe, naona mtoto anatusumbua mno huyu, mpaka naona aibu kumtambulisha kuwa ni wangu Jamaa yangu akajitetea haraka, lakini tayari machozi yalionekana yakimtoka shemeji kwa uchungu, jambo ambalo kwa kweli lilianza kumshtua jamaa yangu. Mke wangu unajua nakupenda sana, hata kitokee nini mimi sitaacha kukupenda sielewi kwanini swali ambalo nilitegemea tutachangia wote kutafuta jibu limeanza kuwa na machungu hivyo kwako mke wangu Shemeji alijiinamia chini akilia sasa tena bila kificho sasa. Jamaa yangu akamkumbatia mkewe akamuuliza mke wangu kuna nini?, kwa mshangao shemeji akaanzia kulia, Nisamehe mume wangu nisamehe, Jamaa yangu sasa akawa anashangaa tu, kisha akamuuliza mkewe, Kuna nini kwani? Shemeji kwa uchungu akamwambia mumewe, Mume wangu nisamehe, ni kweli huyo mtoto wa nne ni wa baba tofauti na wenzie. Kimya kikubwa kilitawala, jamaa yangu alijiona kama vile kazibwa pumzi ghafla. Mume wangu nisamehe huyo mtoto kweli baba yake ni tofauti na wenzie. Huyo mtoto wewe ndie babake
Nimeichukua kwenye blog inaitwa Gazeti la JK