SoC03 Usimamizi Bora wa Sekta ya Michezo unavoweza kupunguza Tatizo la Ajira nchini

SoC03 Usimamizi Bora wa Sekta ya Michezo unavoweza kupunguza Tatizo la Ajira nchini

Stories of Change - 2023 Competition

Wakipekee

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
6,194
Reaction score
10,711
Michezo ni ajira!

Lakini ni ukweli usio na shaka kua hatuna dira maalumu inayoweza kukuza sekta hii. Badala yake kumekua na siasa na mipango ya zimamoto badala ya maandalizi ya muda mrefu yanayoweza kuboresha kiwanda hiki cha michezo. Hii imepelekea michezo mbalimbali kama vile riadha, kuogelea na masumbwi kupoteza mvuto nchini na wizara husika imekaa kimya bila kuonesha juhudi na mipango ya wazi ni jinsi gani wanaweza kuifufua.

Katika hii makala nitaongelea mchezo wa mpira miguu jinsi unavoweza kua tiba ya tatizo la ajira hapa nchini endapo kutakua na mpango mzuri wa kusimamizi kwa serikali kupitia wizara ya michezo kwa kushirikiana na wadau kama vile shirikisho la mpira wa miguu TFF, vilabu na vyombo vya habari.

Jinsi mpira wa miguu unavotoa ajira lukuki kwa watanzania.

Mpira wa miguu una mashabiki wengi kila pembe ya nchi, hivo tayari ni biashara kubwa sana ambayo kama kutakua na uwajibikaji kwa vyombo vilivyopewa mamlaka ya kusimamia ni dhahiri kua utaleta tija kubwa sana kwa wananchi. Mchezo wa mpira wa miguu umekua ukitoa ajira kupitia.

Wachezaji. Hamna mpira wa miguu kama hamna wachezaji. Mtaalamu mmoja wa mashairi aliwahi kusema "huwezi kua fanani bila hadhira". Kwa mfano kwa mujibu wa shirikisho la mpira Tanzania TFF, kuna takriba timu 142 za mpira miguu zinazoshiriki kuanzia ligi kuu hadi ligi ya mkoa. Kwa wastani timu hua na wachezaji zaidi ya ishirini. Hivo ukipiga hesabu za haraka tayari utaona kuna zaidi ya wachezaji elfu mbili wanaoshiriki ligi ya ndani.

Makocha. Kumbuka kocha lazima awe na benchi la ufundi ambapo kuna kocha msaidizi,kocha wa viungo, kocha wa magolikipa,viungo na washambuliaji. Hivo benchi la ufundi hua na zaidi ya watu watano na kuendelea.

Wataalamu wa afya. Kuna vijana wengi sana ambao wameajiriwa na timu Kwa kuzingatia taaluma ya afya. Hivo mchezo wa mpira wa miguu umetoa ajira ambazo serikali na sekta zingine binafsi zimekua zipo Kwa uhaba mkubwa.

Wafanyakazi mbalimbali kwenye vilabu. Vilabu vimeajiri watu wenye taaluma tofauti kulingana na uhitaji. Kwa mfano wanasheria, wahasibu, wanahabari, wapiga picha, wauza tiketi, wafanya usafi, madereva, walinzi, wasemaji pia wakalimani.

Wafanyabiashara na wawekezaji. Mpira wa miguu kwa sasa ni lulu kwani pamoja kua ni burudani lakini pia imegeuka kua ajira kubwa Kwa vijana wengi kupitia biashara za vifaa vya michezo kama vile jezi, viatu, mabegi, kalenda na vifaa vya nyumbani vyenye nembo za vilabu pendwa za hapa nyumbani na hata zile za kimataifa. Pia watu wamewekeza kwa kujenga migahawa, hospitali na nyumba za kulala wageni karibu na viwanja.

Changamoto zinazoikumba tasnia ya mpira wa miguu, ambazo vyombo husika vinapaswa kuwajibika nazo.

kumekua na changamoto na matatizo yalelale miaka nenda rudi ambayo yamekua yakizorotesha maendeleo ya mpira wa miguu nchini. Na hizi ni baadhi ya changamoto zinazoathiri ukuaji wa mchezo wa soka nchini.

Miundombinu ya viwanja. Viwanja vingi nchini vipo chini ya serikali na pia chama cha mapinduzi (CCM), hii ni kutokana na uchumi duni wa vilabu vyetu. Kiukweli miundombinu ya hivi viwanja bado ni hovyo. Kuanzia sehemu ya kuchezea (pitch) majukwaa bado hayakidhi kabisa kuendana na hadhi ya viwanja vya kimataifa. Si ajabu kukuta kiwanja hakina choo, au vyoo ni vichafu kiasi cha kuhatarisha afya za watumiaji.

Pongezi nyingi Kwa Rais wa awamu ya nne, hayati William Benjamin Mkapa kwa kujenga uwanja wa Taifa. Lakini ule uwanja unahitaji maboresho ili uweze kua wa kisasa. Kwanza viti vingi vimeharibika pia vyoo ni vichafu na mfumo wa maji haueleweki. Kumeibuka na tatizo lingine lililotia aibu Taifa pale umeme ulipokatika wakati mechi kati ya timu ya taifa na Uganda zilipokua zikicheza lakini pia mechi Kati ya Yanga na Rivers ya Nigeria.

Nazani wahusika wanatakiwa kuwajibika maana Tanzania imekua ikijaribu kuomba kuandaa michuano ya kimataifa ya AFCON. Lakini Kwa hali hiyo ni ngumu Kwa shirikisho la mpira Afrika CAF kuwapa kibali kama hakuna viwanja vizuri vyenye miundombinu inayoeleweka. Hivo nchi inapoteza pesa na ajira nyingi ambazo zingetokana na uwepo michuano hiyo.

Rushwa. Kumekua na malalamiko mengi ya marefa kupokea rushwa ili kuzipa upendeleo timu flani, au kupanga matokeo. Hii imepelekea nchi kuwa na sifa mbaya kiasi kwamba waamuzi wa Tanzania kukosa nafasi kwenye michuano ya kimataifa. Pamoja na TFF kuwafungia waamuzi wanaonekana kuboronga lakini ni vyema sasa kuangalia nini chanzo cha tatizo na kukiondoa. Moja wapo ni shirikisho hilo kutoa malipo mazuri na kwa wakati kwa waamuzi.

Lakini pia rushwa imekua ikitawala wakati wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo na ngazi ya vilabu, hii imepelekea kua na viongozi wabovu wasio na uelewa na mchezo husika. Hali ambayo imepelekea kua wa viongozi wasiojua wajibu wao.

Ufisadi na ubabaishaji. Utawala mbovu umepelekea vilabu kunyonywa waziwazi na vyombo vinavosimia mchezo wa mpira wa miguu. Kwa mfano mechi ya mkondo wa pili kati ya Simba na Yanga kwenye ligi kuu bara 2023. Simba akiwa mwenyeji wa mechi aliambulia shilingi Milioni 180 tu kati ya zaidi ya shilingi Milioni 400 za kwenye mapato ya mechi husika. Hii ilizua taharuki ingawa hakuna yeyote aliyewajibishwa.

Uhaba wa akademi za kukuza vipaji. Mwanzoni kulikua na akademi iliyoitwa Tanzania soccer academy. Akademi hii iliwahi kumtoa mchezaji nyota Thomasi Ulimwengu lakini baadae ilipotelea kusikojulikana. Serikali ina wajibu wa kukuza vipaji vingi Kwa kushirikiana na vilabu ili kuandaa wachezaji wenye viwango vya kimataifa wanaoweza kucheza kwenye ligi kubwa duniani kama vile ufaransa, hispania na wingereza.

Tujifunze kwenye nchi zilizoendelea mfano Brazil. Kwa ripoti ya may 2022 nchi hiyo ina jumla ya wachezaji 1,219 wanaocheza soka la kulipwa ligi tofauti nje ya Taifa lao. Lakini kuwa na akademi nyingi zilizo bora tutazalisha wachezaji wengi hivo kutakua na vilabu vingi na ajira zitaongezeka Kwani ligi nazo zitaongezeka.

Hitimisho.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo pia shirikisho la mpira wa miguu Tanzania yaani TFF ina wajibu wa kua na dira ya pamoja itakayotoa mipango endelevu wa namna ya kusimamia na kukuza sekta ya michezo. Hivo kuwepo na Sheria zenye meno za kuwajibisha viongozi mafisadi na wapiga dili waliojipachika kwenye michezo ii kujinufaisha wao binafsi. Pia ni muhimu kuboresha miundombinu itakayoharakisha ukuaji wa sekta hii adimu. Kwani inachangia sana ajira na pato taifa Kwa ujumla.
 
Upvote 26
Back
Top Bottom