SoC02 Usimamizi mzuri wa Misingi ya Utawala Bora ni chachu ya mabadiliko na maendeleo chanya katika Jamii zetu

SoC02 Usimamizi mzuri wa Misingi ya Utawala Bora ni chachu ya mabadiliko na maendeleo chanya katika Jamii zetu

Stories of Change - 2022 Competition

Z K Ahmad

Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
29
Reaction score
36
UTANGULIZI:
Kama ilivyo misingi ya Utawala Bora ni Pamoja Na Demokrasia, Utawala Wa Sheria, Haki Na Usawa, Ushirikishwaji Wa Wananchi, na Wajibu Na Uwazi. Yapo mambo kadhaa ambayo iwapo yatasimamiwa makutekelezwa vizuri Itakuwa Chachu ya Mabadiliko na maendeleo chanya Katika jamii zetu.

Katika Pointi hizi za msingi ambazo tutajengea hoja kutokana na mada hapo juu tutaangalia Ni namna gani ambavyo viongozi na wananchi kwapamoja iwapo watakuwa wafuatiliaji na watekelezaji wa Misingi ya Utawala Bora, Jamii zetu nazo zitakuwa Katika mazingira mazuri.

01. Uwajibikaji:
Msingi wa Mambo yote Katika kutekeleza Jambo Kwanza huwa ni kuwajibika, Viongozi ndio viungo wa juu kabisa Kati ya wananchi pamoja na sera mbalimbali za nchi, Katika utekelezaji wa Misingi ya Utawala Bora Viongozi wanatakiwa kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kila hatua inafikiwa ngazi kwa ngazi. Mfano Katika Utawala wa serikali ya Awamu ya sita ya Mh. Raisi Samia Suluhu Hasani Tumeona Raisi akiwa mtekelezaji namba moja wa misingi hii kwakuwajibika Kama Kiongozi wa juu pale alipoamua kiliongelea suala la Demokrasia Na kwa vitendo akalifanyia kazi kwakuungana na vyama pinzani waziwazi kwenye mazungumzo juu ya maendeleo ya nchi ambapo ushirikishwaji wa wananchi ni muhimu pamoja na kusikiliza maoni yao kupitia uhuru wa vyombo vya habari.

Upande wa wananchi nao hawajakaa nyuma kabisa Katika kuhakikisha wanawajibika kwenye kila hatua kwakufuatilia ngazi hadi ngazi wajibu wao katika misingi hii ya Utawala Bora, na kwa asilimia kubwa sana wananchi wanatambua haki na wajibu wao wakushiriki mambo yakijamii na kusimama imara kwenye kutambua sheria zinazoongoza nchi.

02. Utumiaji Mzuri wa Madaraka:

Mifumo yetu ya kiutawala nchi imedhoofisha mamlaka waliokuwa nayo wananchi kiasi kwamba Viongozi hawatambui tena kuwa nguvu walizokuwa nazo pale juu zinatokana na mamlaka waliyopewa na wananchi. Iwapo Viongozi watajitoa na kuendesha Misingi ya Utawala Bora inavyotakikana, basi hata Madaraka waliyokuwa nayo watayatumia vizuri Katika kuwatumikia wananchi na Mabadiliko yatakuwa Ni sehemu yakuleta maendeleo katika Jamii zetu.

Viongozi tuliowapa dhamana yakutuongoza yawapasa kutushirikisha katika maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa jamii na sio kujiamulia wenyewe, kwani kufanya hivyo kutaondoa moja ya Msingi Muhimu wa Utawala Bora. Vilevile Wananchi Bado tunalo jukumu kubwa kuhakikisha viongozi tunaowaweka ili watuongoze tunawatathmini vyakutosha ili wakawe Mfano mzuri Katika utumiaji wa Madaraka tuliyowapatia.

03. Uhuru Wakujieleza:
Hapa tutagusia mambo kadhaa ikiwemo wananchi, wanasiasa lakini pia uhuru wa vyombo vya habari, na ili misingi ya Demokrasia iwe chachu ya maendeleo kwenye jamii, tutaona ni namna gani wananchi na wanasiasa wanaingia katika eneo hili.

Wananchi haswa katika eneo hili wanatakiwa kupewa uhuru wakujieleza katika kuikosoa serikali pale inapokosea na uhuru huu hauji isipokuwa kuwe na viongozi watenda haki na wasiitumia nguvu ya mabavu, kwakutumia vyombo vya habari wananchi wafikishe kero zao mbalimbali zinazosababishwa na viongozi ili kuweza kutatuliwa. Pamoja na hayo vyombo vya habari vinapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha taarifa muhimu zenye kugusa maisha ya wananchi yanawafikia watu wengi zaidi ikiwemo viongozi wa Nchi.

Wanasiasa wanahitajika kuwa mstari wa mbele kueleza na kufikisha kwenye jamii yale ambayo ni muhimu katika kuendeleza gurudumu la maendeleo na hii isiwafanye viongozi waliopo mararakani kuwawekea vipingamizi wanasiasa hao haswa wale wa vyama pinzani. Hii itaonesha ni kwa namna gani Misingi ya Utawala Bora inazingatiwa na kusababisha Mabadiliko kwenye jamii.

04. Vipaumbele:
Tukiliangalia kwa umakini hili tutagundua hakuna Utawala Bora pasipo kuangalia vipaumbele gani muhimu vinahitajika kwenye utekelezaji. Kipaumbele kikubwa cha wananchi katika jamii yoyote inayohitaji maendeleo ni lazima kiheshimiwe na kuzingatiwa na viongozi ili kuwepo na Maelewano ndo maana nasisitiza ufuatiliaji mzuri wa misingi hii, kwani kwakuwashirikisha wananchi kwenye kufanya maamuzi pia tutagundua ni vipaumbele gani muhimu wanahitaji.

Na vipaumbele hivi sio tu kwa wananchi wa jamii flani, Bali nchi pia kwa ujumla ili kuwepo na usawa na haki pia itendeke, na inafaa kila mtu afahamu vipaumbele gani muhimu vitakavyochukuliwa na kufanyiwa kazi. Mfano ni vile vipaumbele ambavyo Mh.Rais Samia Suluhu Hasani Aliviorodhesha kikiwemo cha kukuza na kuendeleza sekta ya Madini, Pamoja na kuzuia uwezekano wa kina mama wajawazito kufariki pamoja na Watoto wachanga, kwakuongea vituo vya afya karibu zaidi na jamii zetu, kuongeza wataalamu wa afya, vifaa tiba na madawa, kutachangia kwa kiasi kikubwa sekta mbalimbali kuleta maendeleo na kuwa na nguvu kazi katika jamii itakayokuza sekta hizo kwa maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Baada yakuangalia hayo, Sasa turudi Kwenye misingi yenyewe ambapo hapa tutaangalia Baadhi kwakutazama ni namna gani hii misingi inaweza kuibadilisha jamii kuwa yenye maendeleo chanya:-

Demokrasia:-
Huu Ni Msingi wa Utawala Bora ambao umebeba sura ya Nchi na Mataifa mbalimbali Duniani, Kwani huu ndo Msingi Mama ambao ukisimamiwa vizuri na Mataifa yanayoendelea basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa Kwenye maendeleo. Kwani Msingi huu unahitaji wananchi kushiriki katika kuchagua viongozi wanaowahitaji na kuwafaa katika safari ya maendeleo, na kila mmoja anao wajibu wakufanya hivyo kwakufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Mwisho Utawala wa Sheria:
Mojawapo ya mambo yasiyofuatiliwa kwa ukaribu ni huu Msingi Muhimu ambapo baadhi ya wananchi na viongozi wamekuwa wakiukaji wa sheria na kutokana nakwamba wana wadhifa fulani au mamlaka fulani katika jamii basi sheria inawekwa pembeni katika kushughulika na makosa waloyatenda. ili jamii zetu ziendelee inatupasa kuzingatiwa kwa msingi huu muhimu wenye kuangalia nini kifanyike ili kuwawajibisha wote wanaovunja sheria. Hakuna anaetakiwa Kuwa juu ya Sheria.

Muandaaji Z.K.Ahmad. Asanteni Sana.
_119154078_adca9b66-3763-4aaa-a441-69ee51bd5d78.jpg
 
Upvote 2
Utawala wa sheria ndio shida kubwa sana .
Implementations yake inawapa ugumu wahusika kufanya hivyo na sheria zipo lakin hazifatwi inavyo takiwa hivyo kudhoofisha dhana ya UTAWALA BORA.

ahsante ndg yangu kitu kizuri.
 
Utawala wa sheria ndio shida kubwa sana .
Implementations yake inawapa ugumu wahusika kufanya hivyo na sheria zipo lakin hazifatwi inavyo takiwa hivyo kudhoofisha dhana ya UTAWALA BORA.

ahsante ndg yangu kitu kizuri.
Asante Sana_ Hakika Serikali Yetu ikijikita katika kusimamia ipasavyo itasaidia
 
Back
Top Bottom