SoC04 Usimamizi wa barabara ya kimataifa nchini

SoC04 Usimamizi wa barabara ya kimataifa nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

John jullai

New Member
Joined
May 28, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Matumizi ya barabara yamekuwa kwa kiasi kikubwa kwa dunia hii ya sasa ambapo makampuni tofauti yamekuwa yakijihusisha na utengenezaji wa barabara na mengine katika kuviunda vyombo vya usafiri na kuviuza kwenye nchi tofauti tofauti. Miongoni mwa barabara zinazotumika kwa asilimia kubwa ni hii inayofahamika kama C2C(CAPE-TOWN TO CAIRO).

Barabara hii iliyoanzia Kusini mwa bara la Afrika katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini mpaka Kaskazini ma bara la Afrika katika mji wa Cairo Misri yenye umbali wa kilomita kumi elfu mia mbili ishirini na nane (10,228km) kutoka kwenye vipimo vya ramani ya google. Barabara imepita zaidi nchi kumi na moja (11) kwenye bara la Afrika ambapo imnapelekea kutumika kwa asilimia kubwa nchini Tanzania.

Barabara hii ina manufaa makubwa katika nchi yetu ambapo inaplekea nchi yetu ikue katika mahusiano baina ya nchi jirani na Tanzania pia na katika sekta mbalimbali za nchini ikiwa ni pamoja na sekta ya uchumi na biashara, elimu, kilimo, usafirshaji, mawasaliano na utalii. ambapo wananchi wanufaika katika kukuza mitaji yao, uchumi kwa ufanyaji wa biashara kwenye vituo wanavyo pumzikia watumiaji wa barabara pia inapelekea urahisi katika upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii kwa usalama katika maeneo husika.
_20240630_210234-jpg.3030090
Moja kati ya chombo cha usafiri wa watalii kikipita kwenye barabara hiyo kijiji cha NTOKELA mkoa wa MBEYA
Uboreshaji wa barabara (lami).
Marekebisho ya sehemu ambazo lami imeharibiwa na matumizi mabaya ya barabara pia ujenzi usiokidhi kiwango cha lami mpaka kupelekea mashimo na kutitia kwa sehemu kubwa ya barabara. Hii ni kutokana na barabara hii kutumika na vyombo vya usafiri vyenye uzito tofauti tofauti na mara kwa mara. Serikali ichukue hatua ya kwakuikagua na kuiboresha mara kwa mara mahali ambapo imeweza kubaini tatizo ama changamoto inayo pelekea uhalibifu wa sehem ya barabara hiyo.

Utoaji wa elimu ya matumizi ya barabara
Elimu juu ya utumiaji madhubuti na usalama wakati mtumiaji anapokua katika kuitumia barabara. Hii itapelekea watumiaji wa barabara kua makini na waangalifu katika utumiaji wa barabara. Na kusaidia kupunguza uharibifu unaotokana na matumizi mabaya ya barabara pia kuhakikisha usalama kati ya watumiaji wa barabara kwa wale walio na vyombo vya usafiri pia hata kwa wale wasiokua na vyombo vywa usafiri.

Ujenzi wa maegesho wa magari ya mizigo.
Hii itaongeza uchumi wa taifa kwa utozaji wa tozo ya maegesho. Ambapo kwa sasa waendeshaji wa magari hayo wanalazimika kuyaegesha kwenye vituo vya mabasi ambapo inakua sio sahihi kwa magari ya mizigo na kupelekea ufinyu wa hudumu za mabasi, japo wengi wao huegesha katika vituo vya ununuzi na uuzaji wa mafuta na wengine katika vituo vya uegeshaji vinavyomilikiwa na watu binafsi ambapo wao ndio hunufaika na sio manufaa kwa taifa kwa ujumla.

Hatua hii pia itaongeza matumizi mazuri na salama ya vyombo vya usafilishaji, na pia watumiaji wa barabara kua na uhakika wa wapi watakapo pumzika na kufanya ukaguzi wa vyombo vyao vya usafili.
Baadhi ya vyombo vya usafilishaji vikiwa vimeegeshwa kwenye kituo cha uuzaji wa mafuta iliyopo pembeni mwa barabara hiyo katika kijiji cha NTOKELA mkoa wa MBEYA. imepigwa na mi mwenyewe.
Usimamizi sahihi ukusanyaji wa mapato barabarani.
Usimamizi sahihi katika ukusanyaji wa kodi sawa na idadi ya mizigo iliyopo kwenye chombo cha usafilishaji husika, kwa kufuata taratibu zilizowekwa na taasisi ya mapato nchini (TRA) pasina ubaguzi wa vyombo hivyo vya usafilishaji. Ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa stakabaadhi za mizigo pamoja na mashine zake za ukataji wa hizo stakabaadh (lisit).

Pia usimamizi huu usimamiwe madhubuti ili kuondokana na ufisadi unao chochewa na utoaji na upokeaji wa rushwa ambapo taasisi ya kuzui na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ihusike kimilifu ili kuondosha aina hiii ya ufisadi katika nchi.

Uwekwaji wa matangazo ya vivutio vya utalii
Uwekwaji huu wa matangazo utaongeza idadi kubwa ya ongezeko la watalii katika nchi yetu ambapo itapelekea nchi kuingiza pesa za kigeni , kuitambulisha katika ulimwengu kwa ujumla na kuafanya uchumi kukua kwa kasi napia hii iatafanya kuepo na upatikania ama ongezeko la wawekezaji kuongezeka katika uwekezaji wa sekta mbalimbali katika nchi ya Tanzania.

Ukaguzi wa vyombo ya usafirishaji.
Ukaguzi wa leseni za madereva pamoja na usalama wa chombo cha uasfiri usafilishaji ikizingatiwa na upimaji wa uzani wa mizigo kufuatiwa tani ya chombo cha usafiri husika. Kwaaijili ya usalama wa miundombinu ya barabara na usalama wasafari kwa watumiaji wa barabara, sababu uzito uliopitiliza unapelekea uhalibifu wa miundombinu husika.
Sambamba na hilo ni pamoja na ukaguzi wa bidhaa husika pamoja na viambatanishi kama kibali husika juu ya maliilizobebwa kwenye chombo hicho cha usafili pia na ufuatiliaji wa malipo na madeni katika chombo husika na kama ni sahihi kupita kweye barabara husika.


Mwisho Serikali inapochukua hatua mbalimbali katika ukuzaji wa uchumi nchini Tanzania, basi ichukue umakini mkubwa katika usimamizi wa miundo mbinu hii maana ina watumiaji wengi; na wengi wao hutoka katika nchi tofauti na Tanzania, usimamizi mzuri utapelekea kuonekana kwa mafaniko wazi katika yale yanayo dhaniwa kuiingizia serikali kipato na kukuza uchumi wan chi kwa ujumla. Ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu juu ya utunzaji salama na matumizi sahihi ya barabara katika jamii ili kuifanya nchi yetu kufikia katika kiwango cha Tanzania tuitakayo.
 

Attachments

  • _20240630_224130.JPG
    _20240630_224130.JPG
    296.2 KB · Views: 2
Upvote 4
Back
Top Bottom