Tizzo G
Member
- Jun 9, 2012
- 25
- 17
Mimi ni mwalimu na ningependa kutoa mapendekezo ya uboreshaji wa huduma zinazotolewa na walimu Kwa Wanafunzi hasa Kwa shule za serikali ili kuongeza ufaulu na kufikia malengo ya serikali.
Moja:- serikali ibadilishe mfumo wa kuajiri walimu Kwa kubadilisha mifumo ya usimamizi wa walimu na utoaji ajira ili mifumo hii iwe ya kisasa, mfano:- kuwe na mfumo unaotoa taarifa za mwalimu Kwa umma kuhusu utendaji Kazi wake pamoja na mfumo wa kufananisha ubora wa walimu wa Somo mojamoja na ufaulishaji wake Kwa Tanzania nzima na mfumo huu uwe mfumo ambao taarifa yake haiwezi kubadilishwa na mwalimu yeyote.
Pia ajira za walimu ziendane na mahitaji ya shule Kwa kuangalia wingi wa Wanafunzi na uwiano kati ya walimu na wanafunzi katika shule husika ili katika kufananisha mafanikio ya walimu Hawa kuwe na uwiano mzuri wa idadi ya wanafunzi na mwalimu katika shule ili kupunguza malalamiko.
Pia mwalimu apewe ajira katika mazingira ambayo hayatakua ni changamoto kwake katika afya ya akili na afya ya mwili Kwa ujumla ili asijenge hoja kwamba mazingira ndio yamekua changamoto kwake. Na pia serikali iongeze idadi ya vitabu vya masomo viendane na idadi ya wanafunzi au viwe katika uwiano mzuri Kwa kuangalia idadi ya vitabu na idadi ya wanafunzi Kwa kitabu kimoja.
Pili:- Kuboresha njia za ufuatiliaji kwenye utendaji Kazi wa walimu. Kuwe na kuwajibishwa Kwa walimu wataoshindwa kufaulisha Wanafunzi wao Kwa asilimia zaidi ya hamsini. Njia inayoweza kutumika ni serikali kumnyima mwalimu husika ajira kabisa pale anaposhindwa kufaulisha na kuwapa watu wenye taaluma ya ualimu wasio waajiriwa Kwa wakati huo au kumpunguzia mshahara wake pale anaposhindwa kufikia asilia 25 ya malengo ya serikali, maana yake ni kwamba Kila mtu ale alichopanda, sio mwalimu amesababisha Wanafunzi wake wote wamepata F kwenye mtihani wa mwisho yaani Mtihani wa kujipima wa darasa la nne au mtihani wa kihitimu darasa la Saba au mtihani wa kujipima wa kidato cha pili au mtihani wa kihitimu kidato Cha nne au mtihani wa kihitimu kidato Cha sita halafu anaendelea kupata mshahara na kupandishwa daraja wakati amesababisha hasara Kwa Taifa.
Tatu:- Kubadilisha aina ya mkataba kati ya mwalimu na serikali ambao Kwa sasa mkataba kati na ya mwalimu na serikali ni WA kudumu yaani permanent contract, mwalimu wa serikali anapewa mkataba wa kudumu hata kama ufanisi wake ni mdogo kitu ambacho ni hasara Kwa serikali na Kwa Taifa Kwa ujumla. Serikali isiweke mkataba wa kudumu kati ya mwalimu na serikali yenyewe Bali mkataba wa mwalimu uwe ni wa muda mfupi na pia mkataba huo uboreshwe endapo ufaulu wa Wanafunzi wa mwalimu husika utafikiwa kulingana na malengo ya serikali Kwa mwaka husika wa kitaaluma. Na endapo mwalimu huyu atafikia malengo ya serikali Kwa mwaka husika wa kitaaluma basi mwalimu huyo apate nyongeza ya mshahara na kupandishwa daraja endapo akifikia malengo ya serikali kwenye mwaka wa kitaaluma Kwa asilimia 100. Na serikali ikiweka Sheria au utaratibu huu utapunguza malalamiko ya nyongeza yamshahara Kwa kada ya elimu.
Nne:- Ajira za ualimu zitolewe mwezi wa kumi na mbili, mwalimu aripoti januari ili ajira hizo ziendane na idadi ya wanafunzi wa kidato Cha kwanza watakaodahiliwa na kupokelewa Januari. Hii itasaidia katika kuyafikia malengo ya serikali kwenye mwaka wa taaluma, unakuta shule Ina uhitaji mkubwa sana wa mwalimu wa Somo Fulani na hamna mwalimu wa Somo hilo kabisa, serikali inaajiri mwalimu mwezi wa sita Ile Hali siku za kitaaluma Kwa mwaka sinakua zimepungua sana.
Tano:- Maafisa wa elimu wabadili njia wanayotumia Kwa sasa ya ukaguzi Kwa walimu unaoangalia andalio la kazi(scheme of work) na andalio la vipindi(Lesson plan) kwani walimu wengi wanaandaa vyote hivyo bila ya kwenda darasani na kuishia kutuma nukuu za Somo husika ziandikwe na wanafunzi bila kufundisha. Ukaguzi ufanyike Kwa kuangalia uelewa wa Wanafunzi kwenye mada zilizofundishwa na mwalimu. Ikiwezekana hata walimu wa shule X wanaweza wakapelekwa shule Y ili kupima uelewa wa Wanafunzi kwenye mada zilizokwisha fundishwa Kwa kutumia mashindano ya kitaaluma(Academic symposium) ndani ya shule au ndani ya darasa Moja.
Mwisho. Serikali iweke mzimamizi mmoja tuu(Bosi wa mwalimu) Kwa mwalimu ambaye anaweza kutoa mwelekeo Kwa mwalimu sio Kila kiongozi awe na uwezo wa kutoa maelekezo kama ilivyo Sasa.

Upvote
3