Mie hawezi kunibalasa coz huwa namwazima flash ya gospal songs na leo nimepata nyimbo mpya ndio gia ya kuingilia hiyo kwa vile ndio ugonjwa wake atanasa tu,Usishangae ukatolewa baruti nawe pia. Unajua wengine kwenye huu ulokole ni kama wameegesha tu, wanasilkiliza mtu anavyomuabisha mumewe...........mara sijui mzinzi, mlevi na mengine mengi.......masikini kesho waumini wanamuona huyo mume aliyetolewa ushuhuda wa dhambi, yaani aibu tupu sema tu mume anakuwa hajui alivyoongelewa na mkewe huko kanisani. Kifupi ni kuaibishana tupu!
Slowly this is becoming a social problem in the country!
Na aina ya makanisa na wachungaji wao nayo inachangia kupotosha watu,
Yani utadhani wao wanasalimiana na yesu kwa kushikana mikono naye!
Japo huyu mhusika ni mbishi kwa hili simwachi nitamlainisha mpaka akubali kusoma na ubishi wake wote,
Yani imefika mahali mmewe anakunywa pombe na kurudi usiku sana wakati wala alikuwa hanywi,akirudi mapema mkewe akianza ibada yake hapo mzuka unampanda mpaka anatoka nje akikemea bila hata kujijua na hapo mpaka apoe ni masaa alafu kila anachokemea ni kuhusu dhambi za mmewe na mambo chungu nzima,
Leo nimezamiria kumsalimia kwa salam ya bwana asifiwe mtumishi wa mungu ndio tuanze maongezi.
Asante sana mpendwa,Naomba muelewe kua hapo awali huu uamsho ulipoanza ulokole ulionekana kama namna fulani ya kujitenga sana hasa pale biblia inaposema "tokeni kati yao mkatengwe nao" watu walipokea vibaya andiko hili kwani mtu alipookoka alitamani kuhama nyumbani kwao, waliokuwa shuleni walitamani kuacha shule kwa mtazamo ambao si mzuri...
Kwako wewe unayekwenda kuongea na mwanandoa huyu inabidi usiongee nae kwa jazba bali muelimishe kuwa hata biblia inasema "Na, kama mwanamke Mkristo anaye mume asiyeamini, na huyo mwanamume akakubali kuendelea kuishi naye, basi, asimpe talaka mumewe." - 1 Wakorintho 7:13
Kwa ushauri zaidi sikilizeni Wapo Radio Fm (98.0) kila jumapili kuanzia saa nne kamili hadi saa tano kamili usiku na jumatatu saa sita kamili hadi saa saba kamili mchana
Ubarikiwe