Usimdharau mwanamke, yeye ndiye ufunguo wako wa mafanikio

Usimdharau mwanamke, yeye ndiye ufunguo wako wa mafanikio

Sanyambila

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2018
Posts
378
Reaction score
510
WAKATI MWINGINE VIJANA WENGI WA KIUME HATUPOKEI BARAKA KWA SABABU HII KUBWA. UKIACHA TABIA HIZI, UTAJIRI NI SEHEMU YAKO

Ni ujinga kumdharau Mama yako aliyekuzaa amekusaidia umefika hapo ulipofika leo hii na bado leo unakosana na mtu mwingine kazi kutaja viungo vya aliyekuzaa.

Ni ujinga kumdhalilisha Mwanamke wakati umezaliwa na Mwanamke.

Ni ujinga pia kumdharau Mwanamke wakati unatarajia kumuoa Mwanamke.

Na ni Ujinga zaidi kumchezea Mwanamke wakati unatarajia kuzaa mtoto wa kike.

Unakuta Mwanaume mzima anapigana na mwanamke bila hata woga au hofu ya MUNGU.
 
Nadhani ungesema ni ujinga na vibaya kumfanyia yote hayo binadamu mwenzio regardless ni mwanamke au mwanaume.

Utajiri na mafanikio huja kwa kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu watu wote (bila kujali jinsia) na kumtumikia Mungu. Acha kudanganya watu!

Kuna faida gani kuwa mshenzi kwa wanaume wenzio kama shetani alafu kuheshimu wanawake pekee?
 
Sababu inayonifanya nisidharau mwanamke ni ule utamu aliobeba, mengine mwanamke ni pasua kichwa
 
Kichwa na yaliyomo haviwiani, namaanisha kichwa cha juu.... kichwa cha siredi.
 
Unaambiwa ukikasirika zuia ghaghabu utoke sehemu hiyo na kwenda kwingine kwa mda kiasi hasira zinapoa
Mtu mwenye nguvu ni yule anaeweza kuvumilia


Sent from my iPhone using Tapatalk
nadhani hayajawahi kukukuta, siku yakikukuta ( ila naomba yasikukute) nadhani utatuelewa ….hawa wanawake hao Mungu anawaona hao.
 
nadhani hayajawahi kukukuta, siku yakikukuta ( ila naomba yasikukute) nadhani utatuelewa ….hawa wanawake hao Mungu anawaona hao.

Nashukuru kwa maombi ila Nina ndoa ya zaidi ya miaka 30 na watoto wakubwa tu
Na ni msaidizi mzuri sana

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
umeandika kimahaba sana , kuna kitu nyuma ya pazia 😂😂😂 anyway kila binadamu anafaa kufanyiwa wema bila kuangalia mwanamke ama mwanaume.Anyway Huo mtazamo wako ...umetoa tamko kama wanauamsho/ushauri...ama ni mada ijadiliwe usahihi wake 😁😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom