Usimfanye mtoto wako kuwa mtoto wa kambo alelewe na baba au mama ambaye si wake. Atakosa amani, uhuru na furaha kwa miaka yake yote ya utoto

Usimfanye mtoto wako kuwa mtoto wa kambo alelewe na baba au mama ambaye si wake. Atakosa amani, uhuru na furaha kwa miaka yake yote ya utoto

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Usimfanye mtoto wako kuwa mtoto wa kambo, alelewe na baba au mama ambaye sio wake. atakosa amani, uhuru na furaha kwa miaka yake yote ya utoto mpaka atakapojitegemea.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Moja ya matatizo àmbayo hayazungumziwi ndàni ya jamii yetu ni pàmoja na changamoto ya Watoto wa kambo kuongezeka. Taikon kama mwanasaikolojia na mwanafalsafa na mwanasosholojia Mbobevu nimeona nizungumzie hili Jambo na athari Zake Kwa Mtu mmojammoja na jamii Kwa ujumla

Mtoto wa kambo ni Yule Mtoto ambaye analelewa na Mzazi mmoja àmbaye siô wake. Yàani analelewa na Baba wa kambo au mama wa kambo.

Kelele zîpo nyingi Duniani kote Kuwahusu Single Mother lakini ukichimba Kwa ndàni utagundua kuwa Anayelengwa na mwenye athari kûbwa Hapo NI MTOTO.

Watoto wa Kambo hukumbwa na changamoto ya Kukosa Uhuru wa kwèli katika Makuzi Yao.

Mtoto wa kambo Hana Amani awapo nyumbani Kwa Sababu Hapo nyumbani kûna Mzazi mmoja siô Mzazi wake yeye. Hii humfanya akose Uhuru katika Makuzi yake.

Mtoto anauhuru WA kujieleza mbele ya Wazazi wake. Mtoto ana Uhuru wa kukataa Kazi Ikiwa amechoka au Kwa kudeka akiwa Nyumba ya Wazazi wake halisi wôte wawili. Mtoto wa kambo ni nusu Yatima.

Babaako ni Babaako unauhuru kwàke na WA kutenda mazuri na Mabaya. Hii NI tofauti na Baba wa kambo àmbaye ubaba wake inategemea na wanaishi vipi na Mamaako Mzazi.

Au Mamaako ni Mamaako tuu unaweza kumkatalia Jambo na mkasumbuana lakini Wala usiwe na hofu Kwa sababu NI Mamaako, Lakini Mama wa Kambo Huna Uhuru kwàke. Siô Mamaako. Hata ukiwa umechoka au unàtaka kukataa Jambo au kudeka unashindwa hivyo itakupasa ufanye kishingo upande.

Mama wa kambo utaishi naye kutegemeana na jinsi anavyoishi na Babaako. Siku wakigombana Mtoto naye anaingia kwèñye msongo WA mawazo, anateseka kisaikokojia. Yaani Mtoto ataishi Kulingana na mahusiano ya Mzazi wake mmoja na Baba/Mama wa Kambo.

Watoto wa Kambo hupendelea kuishi Kwa Bibi Kwa sababu Huko ndiko wanahisi wàpo Huru. Uhuru ninaouzungumzia Hapa NI ule Uhuru wa Mtoto kuishi Maisha ya kitoto, kuhisi kama Mtoto, kufikiri kama Mtoto, kucheza kama Mtoto, kutendewa n kusemeshwa na kuona mambo ya kitoto.

Baba au Mama WA KAMBO anaweza akawa mzuri na mwema Kwa Mtoto asiye wake lakini hiyo haitamfanya Mtoto huyo kuwa Huru Kwa Asilimia Mia Moja. Hii NI Kwa sababu huyo siô Babaake/Mamaake Mzazi.

Huwezi ku-assume kitu NI chako ilhali siô chako. Vivyohivyo Kwa Mtoto akishaanza kujitambua na kujua Baba au Mama huyu NI wakambo mtazamo wake hubadilika. Ule Uhuru àmbao angekuwa nao Kwa Baba/Mama Ake mzazi huyeyuka na Sasa ataishi Kwa Hofu, kimachalechale, mguu ndani mguu nje.

Taikon nashauri, kama Huna ulazima wa kutengana na mwenza wako na tayari mnam/Watoto ni vizuri mjawekana sawa kwa Maslahi ya mtoto wenu.

Msitengane Kwa ishu zisizo na kichwa Wala miguu. Jambo pekee la kutengana ni Usaliti wa mapenzi na hatari ya usalama WA mmoja wenu, kama kûna kupigana na kuumizana. bUsizae Wala kubeba Mimba ukijijua bado hujaolewa au àmbaye unambebea haeleweki.

Utamtesa Mtoto wako Kwa Miaka isiyopungua ishirini Mpaka Siku atakapoanza kujitegemea unafikiri yatakuwa mateso Makubwa kiasi gani? Yàani Mtoto wako wa Miaka mitano, fikiria asiwe Huru na Amani Mpaka Siku atakayoweza kujitegemea yàani Miaka 20-30 Huko hicho ni karibu kifungo ch Maisha

Hakuna atakayempenda Mtoto wako kikamilifu kuliko Babaake/Mamaake Mzazi Hakuna huyo Mtu. Acha kujidanganya. Hakuna Baba àmbaye Mtoto wako atakuwa Huru naye zaidi ya Babaake. Wala Hakuna Mama àmbaye Mtoto wako atakuwa Huru zaidi ya Mamake Mzazi.

Mzazi NI Mzazi hata awe chizi au ujambazi. Mtoto huwa Huru Kwa Baba au Mamaake hata angekuwa Shetani kuliko Mama/Baba wa kambo.

Kumwambia Mtu ampende Mtoto wako kama Watoto wake ni namna Fulani ya kujifariji na kujidanganya Kwa sababu hata Mtoto wako hawezi kuwa Huru Kwake kama àmbavyo angekuwa Kwa Mzazi wake halisi.

Kabla hamjaachana ni Vizuri kujadili Kwa kina suala la gereza mnaloenda kuwaweka Watoto wenu. Kabla hujatenda Kosa ambalo unajua Kabisa adhabu yake ni talaka fikiria Watoto wako na kizazi chako Kwanza

Je, Upo tayari Mtoto alelewe na Mama au Baba àmbaye siye wake? Wewe Ukiolewa na Mwanaume Mwingine na kutaka Mtoto amheshimu na awe Huru na Baba wa kambo huoni kama NI kumtesa Mtoto? Au je ûkioa Mwanamke Mwingine na kutaka Mtoto amheshimu na kuwa Huru na Mama yake WA KAMBO huoni kama NI mateso na Hilo NI gereza?

Au unafikiri Mtoto atakuambia kuwa anateseka kinafsia na rohoni?

Huwezi kuvumilia kitu ambacho siô chako.
Watu huvumilia Wazazi waô
Watu huvumilia Watoto waô.
Watu huvumilia Wake na waume zào.
Unàtaka Baba au Mama WA KAMBO amvumilie Mtoto àmbaye siô Wake huoni kama NI mateso?

Wakati tunatafakari hayo, tujitahidi Sana kupambana kuepuka Makosa àmbayo yatapelekea uvunjifu wa Familia.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel Tz
Taikon wa Fasihi.
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Mkuu umeandika kwa urefu na uchungu lakini yapasa uelewe kwamba kuna wakati malezi ya mama/baba wa kambo ni mazuri kuliko malezi ya mama/baba. Usikariri vibaya.

Nazungumzia HAKI ya Mtoto kuwa Huru katika Makuzi yake. Sizungumzii Malezi.

Malezi Mtu huweza kuyapata hata Kwa Bibi au gerezani, au Jeshini, shuleni n.k lakini Uhuru w Mtoto upo hundred percent Kwa Baba na Mama yake Mzazi.

Baba au Mama wa kambo huweza Kutoa Malezi na huduma Bora kuliko Mzazi halisi lakini linapokuja suala la Uhuru Mtoto atakuwa Huru Kwa Mzazi wake halisi.

Baba au Mama wa kambo hukoma pale watakapokorofishana na kuachana lakini uzazi haukomi.

Kwa lugha nyepesi Baba wa kambo au mama wa kambo ni kama Refugee camps Kwa Mtoto.
 
Dr gwajima hebu waangalie kwa jicho la pili watu kariba ya taikon wana kitu cha ziada huko kwenye taasisi yako inayohusu jamii zaidi .. asante anayejya kutag naomba anisaidie 🤗🤗🤔

😊😊
Mkuu Kazi yàngu ni kuandika tuu.
 
Sawa tutajitahidi lakini maisha sio rahisi na Mara nyingi changamoto hutuzuia kufikia Yale tunayoyataka

Japo Kuna na ujinga pia unayopelekea hayo Ila rule of nature Ina mabalaa Sana
Imagine mkeo anamichepuko na hataki kuwaacha

Mungu atusaidie sana!
 
Umeandika mambo ya msingi sana. Tunapenda starehe, ila hatutaki kuwajibika kwa matokeo ya starehe zetu.

Na kuna wale waliotelekezwa kwa bibi na babu au ndugu🙆🙆

Hatari Sana. Mungu atusamehe ila nasi tujitahidi kuepuka Makosa
Watoto wengi huingia katika magereza ya vifungo virefu vya Miaka 15 mpka Miaka 30 baàda ya Wazazi waô kutalakiana.

Mtoto yupo Kwa Bibi, Siku za Likizo unasema ngoja nimwite mwanangu au Binti yàngu nikae nae walau Mwezi mmoja afurahie akija anakosa Uhuru na amani Kwa sababu mwenza uliyenaye siô Mzazi wake. Hana Uhuru naye
 
Sawa tutajitahidi lakini maisha sio rahisi na Mara nyingi changamoto hutuzuia kufikia Yale tunayoyataka

Japo Kuna na ujinga pia unayopelekea hayo Ila rule of nature Ina mabalaa Sana
Imagine mkeo anamichepuko na hataki kuwaacha

Mungu atusaidie sana!

Yeah, Mungu atusaidie lakini na Sisi tujitahidi
 
Sasa mtoto anajuaje masikini, yeye anajua hao waliopo mbele yake ndio wazazi wake, siku akijua hapo tena ameshakua na utoto haupo tena
 
Sasa mtoto anajuaje masikini, yeye anajua hao waliopo mbele yake ndio wazazi wake, siku akijua hapo tena ameshakua na utoto haupo tena

Siku hizi Mtoto wa Miaka mitano anajua mambo meñgi sana tofauti na Watoto WA kipindi kile.

Mtoto Kwa Mujibu wa sheria ya nchi yetu NI mtu yeyote mwenye Umri chini ya Miaka 18, na Sasa wanaipeleka Mpaka 21
 
Mkuu umeandika kwa urefu na uchungu lakini yapasa uelewe kwamba kuna wakati malezi ya mama/baba wa kambo ni mazuri kuliko malezi ya mama/baba. Usikariri vibaya.
Mkuu huyu jamaa ameongea mambo ya msingi sana bila shaka ukikaa ukayafikiria kwa kina na kujaribu kuhusianisha na maisha halisi huku nje na utatambua kuwa ni ukweli mtupu.
 
Back
Top Bottom