Usimhukumu adui yako, huenda yeye ndio sababu ya uwepo wako

Usimhukumu adui yako, huenda yeye ndio sababu ya uwepo wako

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
384
Reaction score
658
Leinwandbild Dinner Is Served.jpeg

Siku moja Nyani waliposikia kwamba mtu aliyekuwa akiwafukuza kwenye shamba la mahindi amefariki, walisherehekea kwa furaha kubwa na Shangwe wakijipongeza na kuamini hakuna tena atakae weza kuwazuia kuiba Mahindi.

Lakini mwaka uliofuata, hakukuwa na mahindi. Hapo ndipo walipogundua kwa uchungu aliyekufa alikuwa ndio mkulima wa yale Mahindi na hapo wakajua kuwa furaha ingekoma kwa huzuni kwa maana wasingeweza kupata Mahindi kwa mala nyingine'.

Mazingatio:

Watu wanaweza wasione manufaa ya matendo yako leo lakini watatambua umuhimu wako wakati haupo tena.

Kumbuka, sio maadui wote ni maadui.

Baadhi ya vitendo vyetu hutupatia dhihaka tukiwa mbele ya halaiki lakini baadae huleta furaha kwa watu walio tudhihaki.

Tunaishi na watu ambao mioyo yao imekwisha tuhukumu hatuwezi kujitetea mbele yao kwa kuwa fikra zao kwetu ni za uovu.

Asante kwa kusoma na unastahiki heshima.

Soma Pia: Kuwapenda Adui Zetu Katika Maisha ya Kila Siku
 
Back
Top Bottom