Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Mahusiano kati ya wapendanao hujengwa zaidi na hisia za moyo (Feelings), zikipotea hakuna mapenzi yanabaki mazoea!!
kati ya mambo ambayo yanavuruga mapenzi kati ya wanaume na wanawake ni majibu ya kifidhuli ambayo wanaume huyatoa kwa wake zao. Kuna mwanamke mmoja aliwahi kumnunulia mume wake shati jeusi la mikono mirefu pale mnazi mmoja Dar es salaam mwaka 1974. Kwa bahati mbaya yule mwanaume hakulipenda lile shati kwani mashati ya mikono mirefu si stahili yake ya mtindo.
Sasa badala ya kujibu kistaarabu jamaa likamtoka la kumtoka " wewe ina maana ni kipofu huoni mashati ambayo huwa navaa?" binti wa watu akanyong'onyea asijue la kufanya na shati lake mkononi. Miaka 30 baadaye wakiwa wazee jamaa aliletewa shati nyumbani na wauza mitumba, kwa bahati mbaya hakuwepo ila mkewe alikuwepo. Wauza mitumba walishindwa kuuza kwani mkewe akajibu mwenyewe kulihitaji hayupo.
Mzee kurudi anauliza kama kuna wauza mitumba walikuja kuleta mashati, akaambiwa walikuja. Alipouliza ni kwa nini mkewe hakumchukulia akajibiwa kwamba " tangu lini nikajua aina ya mashati unayovaa?" Mzee akakumbushwa kisa cha miaka 30 iliyopita. Wajukuu zake kusikia ilivyokuwa wakabaki na butwaa kumbe babu yao aliwahi kununuliwa shati na bibi yao akalikataa!!
Wanawake wanaweza wasiwe na kinyongo lakini wana uwezo wa kuweka mambo mioyoni mwao kwa muda mrefu sana. Kwa mfano kama mkeo akikuuliza "nikupikie nini leo" anatarajia umjibu kwa staha. Na kwa bahati mbaya sana wanaume wengi hawaelewi maana ya hili swali. Wanawake hawawezi kusema leo nimetamani kula na wewe chakula cha jioni kwa hiyo wahi kurudi badala ya kwenda kwenye pombe. Wao swali la nikupikie nini linabeba maana kubwa sana.
Wanaume tujifunze kutokuwajibu kifidhuli wake zetu!!