Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
Wivu ni sehemu ya mahusiano ila ukizidi huleta ugonjwa wa kihisia na matokeo yake ni muathirika kujikuta anafanya maamuzi ya ajabu na yenye kushangaza Dunia.
Ukiona mtu anafikia hatua ya kumfanyia unyama mpenzi wake mpaka kumtoa uhai mbali na sababu nyingine nyingi ila kubwa moja wapo itatajwa kuwa ni wivu wa mapenzi na nyuma ya wivu wa mapenzi ni mmoja alishindwa kuwa na kiasi katika kumuanini mwenzake.
Mahusiano ya kimapenzi ni muingiliano baina ya watu wawili yaani unakuwa ndani ya mtu mwingine na yeye anakuwa ndani yako ndio maana ikitokea kakusaliti inakupa wakati mgumu kupokea kwa sababu tayari ulikuwa ndani yake hivyo unafikiri utaweza bila yeye .
Kosa kubwa ni kumuamini zaidi ya anavyostahili yaani kumuona kama hawezi kukuacha wala hawezi kutoka na mwingine ila wewe tu , kama umefikia viwango hivyo jua upo kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa wivu kwa sababu utajiingiza kwake 100% .
Madhara ya kuingia kwake 100% ndio pale akikupiga tukio moja kwanza huamini na hata ukiamini basi hukubali matokeo na usipokubali matokeo ndio mwanzo wa matukio ya kushangaza Dunia yanaanza kama sio kujidhuru basi utamdhuru yeye na mwisho wa siku maisha yanharibika na kuacha wengine wakifurahia.
Acha kabisa kuzama kwenye kina usichokijua kwa miguu yote miwili , weka imani naye kwa sababu usipomuamini maisha hayaendi ila usiingie kwenye mtego wa kutokuwa na kiasi yaani ishi naye ila uwe tayari pia kutoishi naye endapo mazingira yatalazimisha kuwa hivyo.
#Mwanasayansi Saul kalivubha
Mitandaoni, fikia ndoto zako.