Usimwombee adui yako njaa,mwombee maisha marefu....

NEW NOEL

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
863
Reaction score
408
Msamaha ndio kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu yeyote yule. Hivyo basi tunapaswa kuwasamehe wale wote waliotukosea kwa mwaka uliopita na tuombe kwa Mungu wetu atusamehe. Naye Mungu atatusamehe tu!!
Hivyo basi tunapaswa kuwasamehe wale wote waliotukosea katika miaka yote iliyopita haijalishi ni nani na alikufanyia baya gani.
Kwa nini ni muhimu kusamehe?
1. Unapomsamehe mtu unakuwa unaondoa mzigo mzito moyoni mwako,na unaufanya moyo wako kuwa huru.
2. Na hata yale uliyomkosea Mungu naye anakusamehe tu,kwa sababu umesamehe wengine.
3. Unafungua milango ya mafanikio katika maisha yako.
Hivyo basi wandugu,tusameheane.....msamehe mama,baba,mke au mpenzi wako au yeyote yule ili usonge mbele na uwe huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…