xfactor
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 1,511
- 1,289
Heshima zenu nyingi sana wakuu
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu aliyeniongoza mpaka nikajiunga JF hasahasa hili jukwaa letu tukufu maana nimejifunza mengi japo mengi yamenipita sababu wadau mmeshaweka hadi kempu za kilimo,nahisi kupitwa sana.Pili niwashukuru wote wenye moyo wa kutoa taarifa ili wengine wajifunze.
Nije kwenye mada yangu.Baada ya takribani mwezi sasa wa kupitia threads mbalimbali za kilimo humu ndani nimehamasika na kudhamiria kuingia kwenye kilimo,taarifa ni nyingi sana ambazo zimetolewa hivyo imeniwia vigumu kufanya maamuzi ya zao gani nianze nalo,matarajio ya huu uzi kuleta harmonization ya taarifa hizi ili watu wapate mwanga wa kilimo gani cha kuanza nacho.
Baada ya kusoma maoni nikajifunza kuwa kuna factor kuu zifuatazo ambazo natakiwa kuzingatia kabla sijachagua zao la kuanza nalo,mtanikosoa kama nitakuwa sipo sahihi:
1. kufanya kilimo sehemu ambayo nitaweza kufika mara kwa mara,kwa maana iwe karibu na dar mfano: chalinze,kibaha,mkuranga,mlandizi,Ruvu,bagomoyo ili iwe rahisi kusimamia sababu naishi Dar
2. Kufanya kilimo ambacho hakihitaji maji sana maana mvua haziaminiki au kama kitakuwa cha kuhitaji maji basi eneo liwe na mto au water table iwe karibu kwa ajili ya visima
3. Upatikanaji wa masoko
Kama nilivyosema awali taarifa ni nyingi mno humu maana kila mtu analima kitu tofauti,Hivyo lengo langu ni kutaka msaada wa yafuatayo
1. kulingana na factors zangu mbili hapo juu, je ni zao gani ambalo lina soko na limaweza kustawi maeneo hayo na wapi naweza kupata taarifa kamili kuhusu zao hili? Kwa maana ya kuandaa shamba,mahitaji ya utunzaji shamba na masoko
2. Mtaji wa kilimo cha hilo zao ni kiasi gani roughly achilia mbali gharama za kununua ardhi
3. Wapi specifically miongoni mwa hayo maeneo naweza kupata eneo ambalo lipo karibu na mto au water table ipo karibu,na bei zinaendaje?
Naamini huu uzi utawasaidia na wengine kama mimi ambao wamekuwa wakiwaza waanze na kilimo kipi.
Natanguliza shukurani wakuu
"Shika elimu ila usimuache kilimo aende zake"