Usinikubali haraharaka!Nisumbue kidogo v/s utandawazi!!!!

kuzungushwa ndo safi inajenga hisia kali ya mapenzi. mbona miez 3 michache sana, mie nilizungushwa 2 yrs, na nampenda mpaka leo!

Duh!Unajiweza!Hata kutafuta kazi sio hivyo!
 
Utaratibu huo bado upo tu, hiyo night stand ni kwa wafanyao biashara lakini kwa mdada wa kisure lazima uswage not less than 3 months at least.

muda wote huo? kwani naomba ajira NSSF,TRA or UDOM? maana maombi ya hizi ofisi yanaweza chukua mwaka.
 
hapo inategemea, unaweza ukamzungusha mtu hata mwaka mzima ila akikupata tu baada ya muda anasepa. siku hizi wanaume nao wamekuwa wajanja sana. anajifanya hana haraka na wewe kumbe anaendelea kukusoma unavyomsumbua. ha ha ha ha ................
 
kuzungushwa ndo safi inajenga hisia kali ya mapenzi. mbona miez 3 michache sana, mie nilizungushwa 2 yrs, na nampenda mpaka leo!
Miaka miwili unazungushwa na wewe umebaki kufatilia kweli unahaki ya kudharauliwa wewe.
 
Ndechumia, wajanja wote siku hizi wanataka mtera maana na haya maambukizi inakuwa kama nafuu fulani
 
Unajua huku kuzunguushana watu wanaelewa tofauti.
Unapozungushwa sababu huweza kuwa
kati ya hizi:
1. Anataka akufahamu vizuri kabla hajaanza mahusiano(hapa anakuwa na hisia ila uoga utawala).

2. Hayupo tayari kuwa katika mahusiano kwa kipindi hicho hivyo anavyokuzungusha muda nao unasogea.

3. Ana hofu na maamuzi ya haraka. Kuna watu ambao ni wazito kufanya maamuzi ya haraka.

4. Hakutaki ila naogopa kukuumiza. Kwa watu ambao walishawahi kupenda kiukweli wanajua maumivu ya kukataliwa na unaempenda yapo vipi. Inawezekana mdada ameshaona kuwa unampenda ile kiukweli ila yeye hayupo tayari kuwa na wewe. Anachofanya ni kukuzuungusha, unapigisha lyrics ila itafikia kipindi wewe mwanaume ndio utachoka na kubwaga manyanga.

5. Anataka akuchune. Kwa wale wadada wachunaji kipindi cha kuzunguusha ni kipindi kizuri kwao kwa mavuno. Mwanaume utaletewa shida na mizinga ya kila aina.

Wanaume wote mnaozungushwa jaribuni kuangalia mpo kundi gani kabla hamjakata tamaa iwapo mmependa kweli. Kama la kuchunwa pole yenu.
 
mambo ya kuzungashana hata hayanogi..muhimu ni kupeana live...mchezo umeisha.sasa kuzungushana haaaaaaaa,si bora ugair tu uende kwa wenye shida zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…